Alhamisi, 30 Mei 2013

MJINI DODOMA KUMEKUCHA WANAFUNZI (DACICO) KUWASILI BUNGENI KESHO


 Mji wa Dodoma Umeanza kupendeza kutokana na Barabara Zinazoingia na kukatiza Mitaa yote kujengwa Kisasa kwa Rami tofauti na Miaka ya Nyuma Dodoma iliyokuwa Vumbi.
 Barabara za Manspaa ya Mji wa Dodoma Zikionekana Kupendeza 
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Vyombo Mbalimbali vya Habari, wanaoripoti Matukio ya Ndani ya Bunge, wakiwa katika Ofisi za Habari ndani ya Bunge leo.
 Mgeni Rasmi, akifunga Maonyesho ya Asasi za Kiraia kwenye Viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. leo
Waandishi wa Habari wakifutilia kwa Makini Hotuba ya Mgeni Rasmi wakati wa kufunga Maonyesho hayo.(Picha kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania)

Na:Mwandishi Wetu Dodoma.

Wakati wanafunzi wa Chuo cha Dar es Salaam City College kutoka Tawi la Dar es Salaam, wakiwasili Leo Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha Bunge hapo Kesho, Leo ndani ya Bunge kumeibuka Mzozo Mkubwa kati ya Wabunge na Wabunge kwa kile kilichodaiwa kuwapo kwa kuungwa Mkono Chama kinachosema Jinsia Moja kuoana cha nchini Marekani, ambapo inasemekana kuwa CHADEMA wamekiunga Mkono cha hicho ikiwa ni pamoja na kupokea ruzuku(Msaada )kutoka katika Makao Makuu ya Chama hicho. 
Hata hivyo, jumla ya Wanafunzi 56 na Viongozi 6 wa Chuo cha DACICO wanatarajia kuingia Bungeni hapo Kesho, wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa DACICO, Mr. Idrisa Mziray, ambaye amefuatana na Walimu Kilangi Msiba, Vedasto Malima, Saasita, Seif Chomoka, 
Katika Mwaliko huo wa DACICO kutembelea Kikao cha Bunge kwa wanafunzi na Walimu, ni moja ya mikakati ya Chuo kuwawezesha wanafunzi kujifunza masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi, na kitaifa ikiwa ni pamoja na kutembelea Vivutio vya Taifa vya Utalii  hivi Karibuni.
Kwa Mujibu wa Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Company Limited, ya jijini Dar es Salaam, ambao ndio waandaaji wakubwa wa safari hizi kwa Chuo hicho, Msemaji wa Miss Demokrasia Tanzania , Mr.Shaaban Mpalule, amesema kuwa baada ya Safari ya Bungeni Chuo hicho kinatarajia kwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Saadan iliyoko katikati ya Bagamoyo na Tanga, kwa lengo la kutembelea Kivutio hicho ikiwa ni pamoja na kuweza kutathmini Utendaji unaofanywa na Wahusika Wakuu.

Jumamosi, 25 Mei 2013

BUNGE LATHIBITISHA KWA BARUA SAFARI YA WANACHUO DAR ES SALAAM CITY COLLEGE KUINGIA TARHE 31 BUNGENI KUHUDHURIA KIKAO CHA SIKU HIYO.


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
TANZANIA PARLIAMETN
Tele. 022 2112065
Fax No. (255) 022 2112538
E-mail: tanzparl@parliament.go.tz
(All official communication should be
addressed to the CLERK OF THE NATIONAL
ASSEMBLY)
In reply please quote
The National Assembly
P.O.Box. 941
DODOMA
REF.NO.EB. 155/261/02/46 24TH, MAY 2013
Director of Study and Programs
Dar es Salaam City College
P.O. Box 90489
DAR ES SALAAM
RE: STUDY VISIT TO THE NATIONAL ASSEMBLY
_____________________
Kindly refer to your letter dated 22nd May 2013, on the above subject.
We are glad to inform you that, the Office of the National Assembly has granted permission for 55 Students and 5 staff to make a visit to the National Assembly in Dodoma on 31 May, 2013 as requested.
Please be advised that you will be arriving at the Parliament grounds through Gate C at 0800HRS in smart attire while observing environmental friendliness.
Upon arrival you will properly be accorded guidance and assistance towards inside the debate Chamber.
Karibuni.

Owen Mwandumbya
For: CLERK OF THE NATIONAL ASSEMBLY

Ijumaa, 24 Mei 2013

Orodha ya Majina ya Wanafunzi wanaoudhuria Dodoma Bungeni(Study Tour Dodoma) Kutoka Chuo cha Dar es Salaam City College.

1: Yassin Lyambata

2:Frank Bwire

3:Christopher Lyogelo

4:Rauph Majid

5:Minza Mabula

6:Deogratius Sarara

7:Hytham Mushi

8:Jackison Nyoni

9:Abdallah Ramadhan

10:Boniface Peter Mles

11:Frenk Gelard

12:Philemoni Mkuki

13:Eddah Slverster

14:Sharifat Mohamed

15:Mariam Mwakatumbula

16:Juma Sufian

17:Mathias Said

19:Belinda Mussa

20:Yusuph Kipesha

21:Herman Amini
22:Mussa Moses

23:Jesca Anthony

18:Martha Joseph Kaunda

24:Yohana Renatus

25:Restuta Mposindawa

26:Estar Charles

27:Salma Milaji

28:Japhet George

29:Ally Bakari

30:Joseph Lywapinda

31:Ikumbo Kilango

32:Mariam Moha
 33:Muddy Kaombwe

34:Naomi Lucas

35:Wema Nyato

36:Haji Mzee

37:Mathias Haule

38:Faudia Hussen

39:Nassoro Said

40:Heavenson Malisa

41:Elizabeth Michael

42:Jesca Alfred

43:Alexander Elcado

44:Zinduna Mtoro

45:Glory Mushi

46:Salma Mashallah

47:Devotha Katondo

48:Zabibu Urassa

49:Jaqueline Mwita

50:Edward Moses

51:Albert Shimiyu

52:Shaaban Mpalule.

VIONGOZI W DACICO

1:Kisiza Leonard

2:Hillary Mgenzi

3:Oscar John

4:Said Rashid

5:Upendo Mvungi

6:Deogratius Peter

WALIMU WA DACICO

1: Mr. Saasita  Kiboka

2:Mr.Vedasto Malima

3:Mr.Kilangi Musiba

4:Mr.Michael Jackison

5:Omary Mtamike

……………………………………………………
Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa Dar es Salaam City College, Idrisa Mziray, akiwa ameambatana na Mwalimu Saasita Kiboka, na Mwalimu Kelvini Haule ambaye yeye ni mwalimu tawi la mbeya, Leo wameondoka jijini Dar es Salaam Kuelekea Mjini Mbeya kwa ajili ya Maandalizi ya Wanafunzi watakaoungana na Wenzazo wa Dar es Salaam kwa ajili ya huo Mwaliko wa kutembelea Bunge, mwishoni mwa Mwezi huu. 

Alhamisi, 23 Mei 2013

Washiriki wa Miss Utalii waliopata Fulsa ya Kujiunga na Chuo cha Dar es Salaam City College, Baada ya Kuibuka Washindi katika Fainali za Taifa 2013

MSHINDI WA TAJI LA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 HADIJA SAID MISS UTALII MOROGORO  KATIKATI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA LUCY NOEL MISS UTALII DAR ES SALAAM KUSHOTO NA MSHINDI WA TATU KULIA THELESIA KILOMO MISS UTALII VYUO VIKUU.WOTE WAMEJISHINDIA NAFASI YA KUJIUNGA KATIKA CHUO CHA DAR ES SALAAM CITY COLLEGE.
 MSHINDI WA TAJI LA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 HADIJA SAID MISS UTALII MOROGORO AKIVISHWA TAJI LA USHINDI NA MGENI RASMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI KANALI MSTAAFU CHIKU GALAWA,MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA BENDEGO

 KUTOKA KUSHOTO NI MISS UTALII KUTOKA MKOA WA KATAVI ASHA RAMADHANI ALIYE SHINDA NAFASI YA NNE, LUCY NOEL MISS UTALII DAR ES SALAAM ALIYESHINDA NAFASI YA PILI, MISS UTALII MOROGORO HADIJA SAID AMBAYE NDIYE MISS UTALII TANZANIA 2012/13, MISS UTALII VYUO VIKUU THERESIA KILOMO
 KUTOKA KUSHOTO NI MISS UTALII KUTOKA MKOA WA KATAVI ASHA RAMADHANI ALIYE SHINDA NAFASI YA NNE, LUCY NOEL MISS UTALII DAR ES SALAAM ALIYESHINDA NAFASI YA PILI, MISS UTALII MOROGORO HADIJA SAID AMBAYE NDIYE MISS UTALII TANZANIA 2012/13, MGENI RASMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI KANALI MSTAAFU CHIKU GALAWA,MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA BENDEGO ,MISS UTALII VYUO VIKUU THERESIA KILOMO NA MISS UTALII SINGIDA MWAKOMBO KESSY ALIYESHINDA NAFASI YA TANO

Ijumaa, 17 Mei 2013

HABARI KUTOKA GAZTI LA MAJIRA WIKI HII

MAJIRA - GAZETI HURU LA KILA SIKU:



Posted: 14 May 2013 10:39 PM PDT

Na Mwandishi Wetu,
Moshi
 MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri K u u y a Ta i f a , (NEC) wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Bw. Jerry Silaa, amesema kukosoana miongoni mwa viongozi ndani ya CCM na Serikali ni njia mojawapo ya kukiimarisha chama hicho na isitafsiriwe vingine.
Bw. Silaa ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam, aliyasema hayo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, wakati wa hafla ya kuwapokea wanachama wapya 155 wa CCM wa tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara, cha mjini Moshi, (MUCCoBS).
"Ni vyema tukajenga tabia ya kukosoana pale tunapoona
mwenzetu au wenzetu wamepotoka katika kutekeleza ilani ya chama chetu la sivyo ahadi zetu kwa wananchi na malengo ya ilani yetu ya miaka mitano hayatatimia," alisema na kuongeza kuwa makosa anayoyafanya mtu yawe ni ya kwake na kuwajibika nayona si chama wala serikali.
Bw. S i l a a a l i s ema pia haitakuwa vyema k u w a c h u k u l i a w a l e wanaojitolea kukikosoa chama au serikali kama wasaliti na kwamba kwa kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kubariki mabaya ambayo yanakemewa.
"Wanaokosoa mapungufu katika utekelezaji wa ilani yetu wasionekane kuwa ni wasaliti kwa kuwa kwa kufanya hivyo tutakiangamiza chama chetu ambacho bado watu wana imani nacho," alionya.
Alitoa mwito kwa viongozi wa CCM MUCCoBS , kuungana na wale wa Umoja wa Vijana wa CCM, (UVCCM), Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wenzao wa mikoa mingine ili kuangalia uwezekano wa k uwa s i l i s h a k e r o zinazohusiana na mapungufu yaliyoko katika bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu na changamoto zake ili kuzitafutia ufumbuzi.
Awali katika risala yake, kaimu katibu wa CCM MUCCoBS, Bw. David Warioba, alisema kuwa moja
 inayowakabili wanafunzi ni mikopo kwa ajili ya wanafunzi hasa wale wa diploma ambao wanataka kuendelea na mafunzo katika ngazi ya shahada.
"Kuna wanafunzi zaidi ya 700 wa ngazi ya diploma hapa MUCCoBS ambao wangependa kuendelea katika ngazi ya shahada, lakini wanashindwa kutokana na serikali kupitia bodi ya mikopo kutoa kipaumbele kwa wale waliotokea kidato cha sita," alisema.
Aidha alitoa wito kwa CCM kupitia Serikali yake kuwachukulia hatua wale wote wanaotumia dhamana waliyopewa kujinufaisha wenyewe jambo ambalo alisema limechangia watu kuinyooshea serikali kidole pamoja na mambo mazuri ambayo imeyafanya na inayoendelea kuyafanya.
Kwa u p a n d e wa k e Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Frederick Mushi, alitoa wito kwa CCM na serikali yake kuwatumia wasomi katika kutekeleza ilani yake.

Posted: 14 May 2013 10:34 PM PDT
Na Rehema Mohamed

 KIONGOZI wa muda mr e f u s e r i k a l i n i n a m t a a l a m u a n a y e t a m b u l i k a kitaifa na kimataifa katika masuala ya uwekezaji, Bw. Emmanuel Ole Naiko, ameteuliwa kuwa balozi wa heshima wa Botswana nchini Tanzania, ambapo makao yake yatakuwa jijini Dar es Salaam.
Akitangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, jijini Dar es Salaam, juzi Bw. Naiko, aliishukuru serikali ya Botswana chini ya uongozi wa Rais Ian Khama na Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa, Bw. Phandu T.C Skelemani, kwa kumteua kuwa
mwakilishi wao hapa Tanzania.
"Naamini ni Mwenyezi Mungu aliyewaongoza na
 mimi napenda kuwahakikishia kwamba sitawaangusha. Nitawawakilisha kwa ukamilifu wote ulio ndani ya uwezo wangu," alisema Bw. Naiko.
Bw. Naiko alimshukuru Waziri Membe kwa kukubali kumkabidhi dhamana hiyo kubwa. "Wewe ni ndugu na rafiki yangu wa muda mrefu naamini uliona ni vyema ukanipa heshima hii wewe mwenyewe," alisema.
Alisema Botswana ina vivutio vingi vya uwekezaji kama Tanzania na kuwa Watanzania na jumuiya y a Af r i k a Ma s h a r i k i wanakaribishwa kuwekeza katika nchi hiyo.
"Nadhani wakati umefika Botswana nayo kupata wawekezaji kutoka Tanzania kama wao walivyowekeza Mlimani City," alisema.
Nc h i y a B o t swa n a imepakana na nchi za Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Namibia na Zambia. Ina ukubwa wa sq km 58,2000, wakazi milioni 2.
Ni nchi iliyo na amani na utulivu toka uhuru na ina kiwango kidogo sana cha rushwa barani Afrika.
Nchi hiyo imedhamiria kuongoza katika sekta za fedha, madini hasa uranium, shaba na usafirishaji wa almasi na copper na pia kuendeleza uwekezaji katika sekta ya utalii kwani Botswana ina mbuga nyingi za wanyama na hasa Vistoria Falls ambayo iko mpakani na Zimbabwe na Zambia katika mji wa Kasane.
"Watanzania walioko huko wameanzisha chama chao na mimi nilikutana nao nilipokuwa TIC," alisema.
Kodi ya mapato katika nchi hiyo ni asilimia 22; VAT ni asilimia 12 na pia kuna msamaha wa kodi kwa wawekezaji ni kati ya miaka mitano mpaka 10.
Posted: 14 May 2013 10:31 PM PDT
Na Reuben Kagaruki

 BAADHI ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamepinga vikali hoja iliyoanzia bungeni wiki iliyopita kwamba kinywaji cha Konyagi aina ya Kiroba kipigwe marufuku nchini na wameonya kuwa uamuzi huo ukifikiwa watahamia kunywa gongo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao, walisema endapo serikali itachukua uamuzi wa kupiga marufuku kinywaji hicho, itakuwa haijawatendea haki walalahoi, kwani ndiyo wanywaji wakubwa.
Mkazi wa Ukonga Mombasa, wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, alisema
Serikali isipige marufuku kinywaji hicho kwani ndiyo mkombozi wao.
"Tukikubali hilo tutakuwa kama Zambia ambayo ilizuia viroba, lakini nchi nzima imejaa viroba vya Malawi, Zaire na Burundi, lazima tuiadhibu serikali ikose kodi kote kote, bia hatunywi, viroba vya nje tutakunywa, pamoja na gongo,"alisema.
Alisema haiingii akilini kukihusisha kinywaji hicho na ajali za magari. Alifafanua kwamba hata kabla ya viroba kuingia sokoni ajali zilikuwepo nyingi.
"Sisi tuna imani na viroba kwa vile vina ubora wa uhakika tofauti na pombe ya gongo ambayo inapikwa bila kupimwa ubora hivyo ni hatari kwa usalama wa afya zetu," alisema Mwiruka.
Kwa upande wake, Bw. John Kamugisha, mkazi wa Chanika, alisema, wanaotaka viroba vipigwe marufuku hawawatendei haki wananchi wa kawaida ambao kwa asilimia kubwa hawana uwezo wa kununua bia ambazo bei yake ni kubwa.
"Siku hizi wananchi wengi wamehamia kwenye makambi ya jeshi ambapo bia zinauzwa bei nafuu na wengine wanakunywa viroba kwa sababu vinauzwa bei nzuri, wananchi hao wakibugudhiwa watahamia kwenye gongo," alisema.
Wakazi wengi waliohojiwa walisema kuwa jambo hilo inawezekana ikawa njama za wafanyabiashara kutoka nchi jirani ambao hawaitakii mema Tanzania kwa kuwa pombe hiyo kuwepo kwake pia kunakuza pato la Taifa.
Naye, Bw. Mwesigwa Joas alisema hapendi viroba ni pombe ya wanyonge hivyo aliwataka wabunge kuthamini kinywaji hicho na bidhaa inayozalishwa na wazawa.
"Huwezi ukahusisha viroba na pikipiki, kwani nchi hii ina pikipiki nyingi na watu milioni 43, uhusiano wake uko wapi, kwanza hata leseni hamuwapi?" alisema.
Watu walitoa maoni hayo baada ya kuona kinywaji chao cha kiroba kinapigwa vita kupitia vyombo vya habari.
Inadaiwa kuwa kampeni inayoendeshwa na kampuni zenye uhusiano na kampuni kubwa ya pombe duniani yasiyopenda, nchi za Afrika zizalishe pombe zake, bali ziendelee kununua kutoka Ireland, Kenya na Uingereza.
Akizungumza na waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki hii, Mkurungenzi Mkuu wa Konyagi, Bw. David Mgwassa, alisema kuwa kwa kipindi kirefu kumekuwa na mchezo mchafu wa kuharibiana jina kampuni yake sokoni kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nc
Posted: 14 May 2013 10:15 PM PDT
Na Goodluck Hongo

 JUKWAA la Katiba nchini, linakusudia kufungua kesi ili kuiomba mahakama isitishe mchakato wa Katiba Mpya hadi Tume ya Mabadiliko ya Katiba na wadau wakubaliane mambo ya msingi ndipo mchakato huo uendelee.
Lengo la jukwaa hilo ni kutafuta haki za Watanzania ili waweze kupata Katiba Mpya waitakayo si vinginevyo.
Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Bw. Deus Kibamba aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na
waandishi wa habari akidai mchakato huo una kasoro nyingi.
 Alisema hoja walizoamua kuziweka bayana ni mchakato huo ambao unaendelea kushindwa kurekebisha makosa ya miaka iliyopita katika kuandika Katiba ambayo ni uelewa, hamasa na ushiriki duni wa wananchi katika mchakato wa Katiba yao.
Aliongeza kuwa, jukwaa hilo limeunda timu ya mawakili 10 wakiongozwa na Mwanasheria maarufu wa masuala ya Haki za Binadamu, Dkt. Rugemeleza Nshala.
“Hivi sasa tunaandaa hoja mu h imu z a k u z iwa k i l i s h a mahakamani ndani ya siku saba zijazo, tunawaomba Watanzania watuelewe kuwa tunakwenda mahakamani si kuvuruga mchakato huu bali kuurekebisha.
“Mchakato huu umeshindwa kurekebisha makosa ya miaka ya nyuma hivyo Katiba itakayopatikana inaweza kuwa mbaya zaidi kuliko hii tuliyonayo kwa kuligawa Taifa,” alisema.
Alisema sababu nyingine ya kwenda mahakamani ni juhudi walizozifanya kutaka kuonana na Waziri wa Katiba na Sheria zaidi ya mara moja ili wazungumze naye kuhusu suala hilo pamoja na kumuona Rais Jakaya Kikwete kushindikana.
Bw. Kibamba alisema ahadi alizotoa Rais Kikwete kuhusu mchakato huo hazioneshi dalili ya kutekelezwa kutokana na tume kusuasua katika utekelezwaji wake.
“Awali tume ilipoteuliwa, wananchi walikuwa na imani nayo kutokana na watu waliopewa dhamana hiyo...mwanzo walipewa sh. bilioni nane na mwaka 2012 walitengewa sh. bilioni 34, pesa hizi wanapewa wao lakini bado wanachelewa kutoa rasimu yake.
“Tunaitaka Serikali ifungue ma s i k i o kwa k u t e k e l e z a makubaliano waliyoafikiana na vyama vya siasa...Uchaguzi wa Mabaraza ya Katiba umevurugwa na tume kwa makusudi kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM),” alisema.
Aliongeza kuwa, chama hicho kilitoa fomu za kugombea nafasi hiyo wakati kazi hiyo ni ya tume hivyo ni wazi kuwa mchakato huo ukiendelea, katiba ijayo itakuwa ya CCM si ya Watanzania.
Alisema kwa sasa mchakato huo hauna uongozi na mwelekeo madhubuti kutokana na wananchi wengi walitoa malalamiko ya kuvurugwa kwa uchaguzi wa Wajumbe wa Mabaraza ngazi ya Kata na Wilaya, kutosikilizwa.
Bw. Kibamba alisema baada ya kufungua kesi hiyo, jukwaa hilo halitazungumzia mchakato huo wakisubiri uamuzi wa mahakama
Posted: 14 May 2013 10:12 PM PDT
Na Esther Macha, Mbeya

 VIBARUA watatu wa kampuni inayojenga barabara ya China Communication and Construction Company (CCCC), mkoani Mbeya, wamefariki dunia kwenye ajali ya gari baada ya lori walilopanda likitoka kuchukua kifusi kupinduka.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Diwani Athuman, alisema tukio hilo limetokea jana saa sita mchana katika eneo la Iganzo, maarufu kama Mwisho wa Lami, barabara ya Mbeya-Chunya.
Alisema gari hilo lenye namba T 405 BWA aina ya
Zhongji mali ya kampuni hiyo, lilikuwa likitoka kuchukua kifusi katika eneo la Kawetele, ambapo dereva aliyesababisha vifo hivyo jina lake halikufahamika mara moja baada ya kukimbia.
Aliongeza kuwa, lori hilo lilipinduka baada ya dereva huyo kushindwa kulimudu kutokana na mwendo kasi katika eneo lenye kona na mteremko mkali.
Hata hivyo Kamanda Athuman alisema marehemu wote ambao miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani humo, bado hawajatambuliwa.
Alisema katika ajali hiyo kulikuwa na majeruhi watano kati yao watatu walitibiwa hospitali na kuruhusiwa, wawili wamelazwa katika hospitali hiyo.
Aliwataja majeruhi wanaoendelea na matibabu kuwa ni msimamizi wa vibarua hao raia wa China, Don Fung Cheng (38), aliyejeruhiwa kichwani, pamoja na mtu mwingine ambaye hajafahamika jina kutokana na hali yake kuwa mbaya.
Waliotibiwa na kuruhusiwa ni Ayoub Samson (25), Jelicko Apton(18) na Natifa Ngole (23), wote wakazi wa Mkoa huo.
Posted: 14 May 2013 10:11 PM PDT
Na Heri Shaaban

 WATOTO 5,000 wenye umri wa miaka 10 kushuka chini, wanatumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI (ARVs), katika Hospitali ya Amana, Dar es Salaam.
Mbali ya watoto hao, watu wazima 11,000 nao wameanza kutumia dawa hizo katika kliniki iliyopo hospitalini hapo.
 Daktari wa Kitengo cha Kuratibu Wagonjwa wa UKIMWI, Shani Mwaruka, aliyasema hayo wakati kamati ya kudhibiti ugonjwa huo Manispaa ya Ilala, ilipofanya ziara katika hospitali hiyo.
Alisema kwa siku kliniki hiyo uhudumia wagonjwa 250 hadi
300 ambao wanatoka kwenye maeneo mbalimbali na kudai kuwa, changamoto waliyonayo ni baadhi ya wagonjwa kutokubaliana na hali waliyonayo pamoja na uchache wa vitendea kazi.
“Watu wengi hawakubaliani na hali waliyonayo, baba anapokuja kupima afya yake anamficha mkewe na kuanza kutumia dawa peke yake na wanawake pia hivyo hivyo,” alisema Dkt. Mwaruka.
Aliongeza kuwa, kitengo hicho kinafanya jitihada za kuhakikisha wazazi wanawaeleza watoto wanaotumia dawa hizo wanapokua.
Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Said Kitambuliyo, alisema lengo lao ni kutembelea mitandao yote na asasi za watu waishio na ugonjwa huo, kusikiliza changamoto walizonazo na kuangalia kazi wanazofanya.
Posted: 14 May 2013 10:08 PM PDT
Na Mwandishi Wetu
 KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua Mattar Sarahan Said, kuwa mgombea wake wa chama hicho katika Jimbo la Chambani, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba.
Uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha siku moja kilichofanyika mjini Dodoma jana chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.
Pia chama hicho kimewateua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Balozi Seif Idd na Mwenyekiti mstaafu wa CCM ambaye pia ni Rais mstaafu wa awamu ya pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi, kufunga kampeni hizo.
Posted: 14 May 2013 10:00 PM PDT
Na Suleiman Abeid, Kahama
 MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mk o a n i S h i n y a n g a , Khamis Mgeja amekataa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya kwa madai imeandikwa ovyo na kwa dharau.
Mbali ya kukataa kupokea taarifa hiyo, Mgeja alilaani kitendo kilichooneshwa na mkuu huyo wa wilaya baada ya kubainika kuwa taarifa aliyopelekewa iliwahi kukataliwa pia hivi karibuni na
wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilayani Kahama.
Hata hivyo, kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo, Mpesya alikanusha kufanya dharau kwa chama chake na kwamba yeye anawajibika kwa Katibu wa CCM wilayani Kahama na siyo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa na iwapo taarifa hiyo ilikuwa na mapungufu basi ndivyo ilivyoandaliwa na watendaji wake wa CCM.
“Nikiri ni kweli taarifa hiyo mimi ndiye niliyeipeleka kwa katibu wa CCM wa wilaya ambaye ndiye ninayewajibika kwake na siyo kwa mwenyekiti wa CCM wa mkoa, aliyepaswa kuipeleka kwake ni katibu wake wa CCM siyo mimi hivyo makombora niliyorushiwa yalistahili kuelekezwa kwa katibu huyo,” alieleza Mpesya.
Akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Malunga wakiwemo wanachama na viongozi wengine juzi, Mgeja alisema CCM haitokubali vitendo vya kipuuzi vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wa serikali.
“Nimesikitishwa sana na kitendo cha mkuu wa wilaya, niliomba nipatiwe taarifa ya utekelezaji wa ilani yetu ya uchaguzi upande wa utoaji mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake, lakini nilicholetewa kimenishangaza, kinaonesha wazi mwenzetu huyu anatudharau viongozi wa chama,”
“Taarifa aliyoandika haiwezi kuandikwa hata na DC (mkuu wa wilaya) anayejifunza kazi, sijui mwenzetu huyu kiburi hiki anakipata wapi, nimeikataa na ninaomba iandikwe nyingine ikiwa na uchambuzi kamili kuonesha jinsi gani vijana na wanawake wamesaidiwa kupitia asilimia 10 ya mapato ya halmashauri,” alisema Mgeja.
Mgeja aliwataka watendaji wote wa serikali mkoani Shinyanga kuhakikisha hawafanyi vitendo ambavyo vitasababisha wananchi wakichukie chama chao hivyo kusababisha mpasuko wakati wa uchaguzi.
Kutokana na hali hiyo Mgeja aliahidi kupeleka nakala ya taarifa hiyo makao makuu ya chama na kwa Mwenyekiti wake wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga ili waweze kuona wenyewe madudu yanayofanywa na watendaji wa chini yao.
Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Isaka aliyekaribishwa katika kikao hicho, Gavana Ally alishauri vikundi vyote vya vijana na wanawake wilayani humo kuandaa taarifa zao mapema zikionesha misaada au mikopo yote waliyokwishapokea kutoka halmashauri ili ilinganishwe na ile itakayoandikwa upya na mkuu huyo wa wilaya.
Posted: 14 May 2013 09:58 PM PDT
Na Rehema Mohamed

 WALIOKUWA wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ma z i n g i r a ( N EMC ) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kushawishi rushwa ya sh.milioni 6.
Washtakiwa hao ni Jerome Kayombo (33) na Milton Mponda (32).
Mbele ya Hakimu Gane Dudu, wakili wa serikali kutoka Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kelvin Murusuri alidai kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo kati ya Mei 4 na 5, 2012 katika Kiwanda cha Kamal Steels eneo la Chang'ombe.
Alidai kuwa, washtakiwa hao wakiwa kama maofisa ma z i n g i r a wa NEMC walishawishi wapewe rushwa ya sh. milioni 6 kutoka kwa Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Sammer Gupta ili iwe k ama k i s h awi s h i kwa Mkurugenzi huyo asiadhibiwe kwa kukiuka sheria ya utunzaji mazingira.
Hata hivyo washtakiwa hao walikana kutenda makosa hayo ambapo upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.
A i d h a , k e s i h i y o imeahirishwa hadi Mei 23, mwaka huu itakaposikilizwa.
Washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya sh. milioni 5 kila mmoja.

Posted: 14 May 2013 09:53 PM PDT
Na Darlin  Said
 kAMPUNI za kufua umeme kutoka nchini Sweden, zipo katika mchakato wa kuzalisha umeme kwenye vyanzo mbalimbali baada ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kutokidhi hitaji la kutoa huduma hiyo kwa wananchi wengi.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akiwakaribisha wawekezaji hao na kuongeza kuwa, lengo la Serikali ni
kuiboresha TANESCO ili iweze kutoa huduma bora.
 Alisema tangu kuanzishwa kwa shirika hilo mwaka 1961 ni asilimia 21 tu ya Watanzania waliopo mijini na asilimia saba waliopo vijijini ambao ndiyo wanaopata huduma ya umeme.
“Kimsingi hali hii inasikitisha, tumegundua kuwa TANESCO peke yao hawawezi kutoa huduma ya umeme kwa Watanzania wenye hitaji hilo hivyo wataendelea kuumia,” alisema.
Prof. Muhongo aliongeza kuwa, Serikali imewakaribisha wawekezaji hao kwa sababu haina fedha za kuwekeza katika sekta ya nishati ili kusambaza huduma ya umeme.
“Pato la Taifa ni dola za Marekani bilioni 28 ambazo tukizigawa, kila Mtanzania atapata sh. 6,000 hivyo lazima tutegemee wawekezaji ili tuweze kujikomboa,” alisema.
Alisema wawekezaji hao mbali ya kufua umeme nchini, pia watatekeleza miradi mbalimbali, k u b o r e s h a mi u n d omb i n u , kusambaza umeme vijijini na kupunguza upotevu wa umeme.
Aliongeza kuwa, vyanzo vyote vya umeme nchini vingeweza kuzalisha umeme wa megawati 1,438.24 lakini miundombinu iliyopo hata kama umeme huo ungezalishwa, wangeshindwa kuusambaza kutokana na ubovu wa miundombinu ambao hupoteza asilimia 23.4 ya umeme.
Alisema kampuni hizo zitafua umeme kupitia upepo, miamba, kinyesi cha wanyama, maji, jua na kusisitiza kuwa ni ndoto ya mchana kuitegemea TANESCO izalishe umeme kupitia vyanzo hivyo.
Kwa upande wake, Balozi wa Sweden nchini, Bw. Gunnar Oom, alisema wameamua kuwekeza Tanzania baada ya kuona misaada pekee wanayotoa haiwezi kuongeza
 kasi ya maendeleo.
Alisema kupitia uwekezaji huo, utasaidia kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kiuchumi pamoja na kubadilishana uzoefu.
“Kupitia uwekezaji huu, pia utasaidia kubadilishana bidhaa kwa kununua zilizopo Tanzania kwani nchi nyingi za Afrika zinategemea sana kuuza mafuta, madini na mazao ya chakula nje,” alisema.
Posted: 14 May 2013 09:42 PM PDT
David John na Neema Malley
 CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeitaka Serikali itoe tamko la kuiomba radhi Serikali ya Saudi Arabia kutokana na raia wake wanne kuhusishwa na tukio la ulipuaji bomu mkoani Arusha na baadaye kuachiwa baada ya uchunguzi kubaini hawakuhusika.
Tukio hilo lililotokea Mei 5 mwaka huu, katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, mkoani humo ambapo watu watatu walifariki dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.
Mwenyekiti wa chama hicho Taifa,
Prodesa Ibrahim Lipumba, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akifungua Kikao cha Baraza Kuu la chama hicho na kuongeza kuwa, kwa muda mrefu Saudi Arabia na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri hivyo ni wajibu wa Serikali kuomba radhi ili kuendeleza uhusiano huo.
Alisema wageni hao waliingia nchini kihalali hivyo kitendo cha kuhusishwa na tukio hilo ambalo limetangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari kimechafua jina la nchi yao.
“Serikali inapaswa kuwa makini na inachokifanya, kitendo cha kuwakamata wageni hawa ambao wanatoka kwenye nchi ya Kiislamu, kinaweza kuwagawa Waislamu na Wakristo kitu ambacho ni hatari kwa Taifa,” alisema.
Aliongeza kuwa, Serikali inatakiwa kuchukua hatua stahiki yanapotokea matukio makubwa kama hilo la uvunjifu wa amani ili kuwajengea imani Watanzania kuwa Serikali yao ipo makini.
Katika hatua nyingine, Prof. Lipumba alizungumzia uamuzi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, kumuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda.
Alisema kilichofanywa kwa kiongozi huyo si cha kiungwana kwani kesi iliyokuwa ikimkabili ilikuwa ikihusu kiwanja hivyo ingehamishiwa kwenye Mahakama ya Ardhi.
“Serikali imekuwa ikikuza mambo na kusababisha mifarakano katika jamii...inapaswa kufanya uchunguzi wa kina kwanza kwani mwisho wa siku nchi itaingia katika matatizo,” alisema.
Pia Prof. Lipumba alidai kuhofia deni kubwa la Taifa na kudai kuwa ili kuondokana na madeni ya aina hiyo, Serikali inapaswa kuacha tabia ya kukopa bila utaratibu kwani mwisho wa siku tutashuhudia Taifa likipata mzigo wa kurejesha madeni hayo.
Aliongeza kuwa, kipindi cha utawala wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa, wakati akiingia madarakani alikuta Taifa likiwa na deni kubwa hivyo alitumia kipindi cha miaka mitano kulipunguza sana.
Alisema pamoja na nchi kuwa na rasilimali za kutosha katika Taifa, bado utegemezi umekuwa mkubwa na Serikali imekuwa bingwa wa kutoa ahadi zakutekeleza miradi mbalimbali.
Posted: 14 May 2013 09:38 PM PDT
Na Derick Milton, Simiyu
 MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti amewataka wanasiasa mkoani humo kuacha mara moja tabia za kuwadanganya au kuwapotosha wananchi kuhusu kilimo cha mkataba hususani zao la pamba.
Alisema, yeyote ambaye ataenda kinyume na agizo hilo atakamatwa ili kufikishwa
mahakamani, sheria ichukue mkondo wake.
Hayo aliyasema jana ofisini kwake mjini Bariadi wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alikuwa anazungumzia juu ya zao la pamba msimu huu.
Alisema kuwa, katika msimu uliopita wa zao hilo baadhi ya wanasiasa walipita kwa wakulima kuhamasisha wakatae kilimo cha mkataba kwa madai wakijiunga watanyang'anywa mashamba yao na wafanyabiashara.
Mkuu huyo alisema, baada ya wakulima kuambiwa hivyo na wanasiasa hao waliokuwa wame j i u n g a wa l i a n z i s h a mgogoro mkubwa kati yao na wafanyabiashara hadi kusitishwa kwa kilimo hicho.
Kutokana na hali hiyo, Mabiti aliamua kupiga marufuku kwa mwanasiasa yeyote atakayebainika anapinga kilimo cha mkataba kwa msimu ujao kuwa atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Alibainisha kuwa, hali ya zao la pamba kwa msimu huu ni mbaya katika uzalishaji wake kuwa mdogo, na kutaja sababu kuwa ni kusitishwa kwa kilimo cha mkataba baada ya kuwepo mgongano baina ya wahusika katika kilimo hicho.
Pia alisema, kwa sasa serikali pamoja na wadau wengine wa zao la pamba wakiwemo wafanyabiashara wanafanya utaratibu wa haraka na ambao utakuwa ni mzuri kuhakikisha kilimo hicho kinarudi ili kumkomboa mkulima.
“Katika utaratibu utakaowekwa hivi karibuni, mtu yeyeyote ambaye ni mwanasiasa atakayeonekana na kubainika anapinga kilimo hicho sitamuonea huruma, nitamkamata na kumchukulia hatua za kisheria labda aongelee nje ya mkoa wangu,”alisema Mabiti.
Alibainisha kuwa, wanasiasa hao wamekuwa wakifanya hivyo kwa maslahi yao binafsi na kusababisha wananchi wengi hasa wakulima kubaki maskini na hata bila kutoa msaada wowote kwa watu hao.

Posted: 14 May 2013 09:25 PM PDT

Na Ester Maongezi
Wanafunzi wa kike 32 wanaosoma katika Shule ya Sekondari Manzese, iliyopo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, jana walianguka wakiwa darasani na kupoteza fahamu.
Tukio hilo ambalo limetokea saa tatu asubuhi, limehusishwa na imani za kishirikina ambapo uongozi wa shule ulilazimika kuwaruhusu wanafunzi wengine
kurudi majumbani kwao.
Akizungumza na gazeti hili, Mkuu wa shule hiyo, Bw. Linus Mwakasege, alisema tukio hilo limekuwa likijirudia mara kwa mara kwa siku za Jumatano na Ijumaa.
“Idadi ya wanafunzi waliokuwa wa k i a n g u k a k a t i k a s i k u hizi ni ndogo ambayo huwezi kuilinganisha na tukio la leo (jana) ambalo limetushtua sana,” alisema Bw. Mwakasege.
Akielezea mazingira ya tukio hilo, Bw. Mwakasege alisema alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele akiwa darasani, kuanguka chini na kupoteza fahamu.
Alisema hali hiyo iliendelea kwa wanafunzi wengine hadi ilipofikia idadi hiyo na wengine kukimbia ovyo ambapo walimu walifanya kazi kubwa ya kuwatuliza.
Bw. Mwakasege alisema baada ya tukio hilo, alifanya jitihada za kuita viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu ambao walifika shuleni hapo na kuwaombea wanafunzi waliopatwa na tatizo ambapo hali hiyo iliwasaidia kurudi katika hali ya kawaida.
Mwanafunzi mmoja wa shule hiyo ambaye naye alipatwa na tatizo hilo, Hellen Said alisema hakuwa akifahamu lolote bali alijikuta mapigo ya moyo yakimuenda mbio, kuanguka na kupoteza fahamu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Manzese, Bw. Salehe Rashidi, alisema tukio hilo limekuwa likijirudia shuleni hapo hivyo atashirikiana na uongozi wa shule kuhakikisha kila mwanafunzi kwa imani yake wanafanya maombi kila wiki.
“Maombi haya yatasaidia kukabiliana na mapepo mabaya yanayowaandama wanafunzi ambao wanakosa uhuru wa kusoma ili kujiwekea msingi mzuri.wa ,aisha alisema.