Jumamosi, 12 Aprili 2014

MJUMBE ATAJA ABABU ZA KUKATAA SERIKALI TATU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe dacicotanzania@gmail.com , au  namba +255713869133. 
Mbunge wa Kibaha Vijijini,Abuu Jumaa.
 
Mjumbe  wa Bunge Maalum la Katiba, Abuu Jumaa, amesema Tanzania haitakiwi kujiingiza katika masuala ya muundo wa Muungano wa serikali tatu kwa sababu bado ni nchi changa.
Akizungumza na NIPASHE jana, Jumaa ambaye pia ni Mbunge wa Kibaha Vijijini (CCM), alisema kwa sasa wanatakiwa kutatua changamoto zote zilizojitokeza kwenye serikali mbili ndiyo wafikirie muundo mwingine wa Muungano.

“Ni mapema sana kwa nchi yetu kujiingiiza katika masuala ya serikali tatu…sisi wenyewe tunaweza kujiona tumekuwa, lakini bado kabisa,” alisema.

Alisema utafiti uliofanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, umeonyesha kuwa changamoto zilizopo kwenye serikali mbili ni sita wakati za serikali tatu ni saba.

“Hatuwezi kwenda kwenye mfumo wa serikali tatu, maana muundo huo una changamoto nyingi na gharama zake ni kubwa ni bora twende kwanza na huu muundo wa serikali mbili,” alisema.

Aidha, alisema Watanzania wanatakiwa kuwa wavumilivu ikiwa ni pamoja na kufanyia marekebisho changamoto zilizojitokeza kwenye serikali mbili.

“Mimi sidhani kama wananchi wana uelewa kuhusu serikali tatu…wanatakiwa kwanza kupata elimu ya kutosha ili waweze kuelewa maana ya muundo wa serikali tatu na mbili,” alisema.

Alihoji: “Kama wasomi wamepata uelewa wa serikali mbili na serikali tatu… je wananchi wa kawaida ambao hawana uelewa huo itakuwaje?”

Aliwataka wananchi kusoma ili waelimishwe waelewe kuhusu muundo wa serikali tatu.

 “Hata siku katiba hii itakapokwenda kwa wananchi waende kupiga kura wakiwa na uelewa wa muundo wa serikali,” alisema.
SOURCE: NIPASHE

TAARIFA YA MUHIMU SANA: MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA YATOA TAHADHARI DHIDI YA UHALIFU UNAOFANYWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI ,SOMA HAPA KWA UMAKINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu dacicotanzania@gmail.com au namba ya mkononi+255713869133. 


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kuzingatia kifungu 5 (b) na (e) cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya 2003 inatoa tahadhari kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano, wananchi na umma kwa ujumla kujihadhari na utapeli unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi na mtandao wa intaneti kama ifuatavyo:

1. Usimpe mtu yeyote usiyemfahamu vizuri simu yako au kadi yako ya simu ili atumie.
2. Usitoe maelezo yoyote kuhusu namba yako ya simu au taarifa za binafsi kwa mtu yeyote anayekupigia simu kutaka taarifa hizo.
3. Usijibu ujumbe wa simu unaohusiana na fedha zako hata kama namba iliyotuma unaifahamu.
4. Usitekeleze maagizo yoyote yanayohusu fedha kwa ujumbe wa maandishi hata kama yanatoka kwenye namba ya mtu unayemfahamu. Mpigie aliyekutumia ujumbe uzungumze naye.
5. Usitekeleze maagizo yoyote kutokana na ujumbe wa simu za mkononi unaokutaka kutuma fedha kutoka namba ambayo mtumiaji wake unamfahamu na ambao unakueleza kwamba simu yake ina hitilafu hivyo hawezi kuongea, usitekeleze maagizo hayo.
6. Ukipata ujumbe kwamba umepokea fedha kwa njia ya simu, mpigie aliyekutumia na usitoe pesa hizo hadi uthibitishe kwamba zimetumwa kwa nia njema.
7. Weka njia za kuthibitisha taarifa kabla ya kufanya miamala ya kifedha kutumia simu ya mkononi.
8. Ukipigiwa simu na mtu yeyote kuhusu masuala ya fedha, hata kama unadhani unamfahamu mtu huyo; mpigie tena kwa namba yake unayoijua ili kuhakikisha kwamba ni yeye.
9. Iwapo unafanya biashara ya huduma za simu hakikisha kwamba simu unayoitumia kwa miamala ya kifedha ni tofauti na unayotumia kwa shughuli nyingine na hakikisha simu hiyo haitumiwi na mtu mwingine
10. Tumia namba ya siri ambayo sio rahisi mtu mwingine kukisia.
11. Usitoe namba zako za siri unazotumia kwa huduma
12. Thibitisha na hakiki namba ya mtu unayemtumia pesa au salio kabla ya kutuma
13. Ukipoteza simu au laini yako ya simu toa taarifa kwa mtoa huduma wako na Polisi mara moja.
14. Ukifanyiwa uhalifu ambapo simu au mtandao umetumika kufanyia uhalifu huo hilo nikosa la jinai. Toa taarifa Polisi ili wahalifu wasakwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
15. Usipopata ushirikiano wa kutosha kwa mtoa huduma wako katika kutatua tatizo lako wasilisha malalamiko yako Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. 

Unaweza kuwasilisha malalamiko kwa kutuandikia ( S.L.P 474 Dar es Salaam); kufika ofisini makao makuu namba 20 Sam Nujoma Dar es Salaam au kwenye ofisi za Kanda na Zanzibar; kupiga simu ( namba 0784 558270 au 0784 558271) na kwa barua pepe (malalamiko@tcra.go.tz au complaints@tcra.go.tz)
Imetolewa na:
 MKURUGENZI MKUU

 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

DACICO F.C KUNGURUMA IJUMAA DHIDI YA KIBAMBA HOSPITALI.

HII NDO DACICO FC VIJANA WAKALI KWELIIIIII HAWA
 
 
 
 
 

DACICO FM RADIO IMETOA POLE ROZINA MCHOMVU- KWA KUONDOKEWA NA BABA YAKE.

Kwa niaba ya serikali ya wanafunzi na uongozi wa chuo cha uandishi wa habari na utawala Dar es salaam city college nasikitika kutangaza kifo cha baba wa mwanafunzi Rozalina Mchomvu pamoja na dada yake Rozina Mchomvu ambaye ni katibu mkuu wa serikali ya wanafunzi Dacicostua tangu Novemba mwaka jana, kifo hicho cha baba yao kimetokea leo mchana baada ya kuugua muda mrefu, msiba upo nyumban kwao Mbagala...

Good dreams dudez! Saa mbaya.

Bado Nipoogo,Je Dacico mpoogo?

Like ·

Wadau wa DACICO wanena- wasema Waawataka Watu Kubadilika.

  • Mabadiliko hayawezi kuwa mabadiliko kama watu hawakubali kubadilika: uchu,uroho wa madaraka unaweza kusababisha ukashindwa kuwatetea hata wale waliokusapoti hii ni kutokana na kutotambua wapi ni mwanzo na wapi ni mwisho...

    MARTIN LUTHER KING aliwahi kusema kuwa sometimes we need to loose nothing to be honest ila usemi huu haumaanishi kwamba uruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa Kama vile ambavyo Serengeti shall never die vivyo hivyo DACICO SHALL NEVER DIE.

    Kuwa kiongozi ,haimanishi kupendwa. Bali inamanisha kufanya lililosahihi. Kunatofauti kubwa kufanya jambo zuri na jambo sahihi. Uongozi bora ni pale unapofanya yaliyosahihi hata Kama yanawaudhi wale unaowaongza ,badala ya kufanya mambo mazuri yanayowafurahisha.LEADESRSHIP IS NOT A POPULARITY CONTEST.

    Kumbuka kuwa Kila kiongozi mkubwa au maarufu (mwenye maono au fikra zenye busara) mwanzoni alichekwa au kudhihakiwa. Lakini sasa anaheshimika.

    Haijarishi WATU wengine wanafikiri nini juu yako. Kinachojalisha ni vile unavyofiri juu yako. Mara nyingi tunapoteza nguvu kuhusu mitazamo ya wengine tunatamani kukubalika na kupendwa, tunataka tufurahishe, uongozi uliotukuka ni pale unapokuwa uko juu zaidi ya mitazamo ya umma juu yako,yaani above social approval to self approval .kwa nini ujali vile Kila mtu anafikiri juu yako. Run your own race,your dream, Kumbuka success is not a popularity contest. Mwisho wa siku ni kuwa JE umekuwa mkweli juu yako mwenyewe?

    One of my best quote come from George Bernard Shaw , "The reasonable man adapts himself to the world,the unreasonable one persists in trying to adapt the world to himself " therefore all progress depends on the unreasonable man. Please think about that idea for a moment. I suggest it's a big one. ....have a great day

    Sayed mathias canal
    Like · · April 8 at 9:49am
  • HAKIKA NATOA PONGEZI ZA DHATI KWA UONGOZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTAWALA DAR ES SALAAM CITY COLLEGE KWA KUENDELEA KUWA CHUO BORA CHENYE MWANGAZA BORA WA ELIMU TANZANIA HUSUSANI KATIKA MAMBO YA HABARI NA UONGOZI YAANI UATAWALA, SHUKRANI ZA DHATI ZIENDE KWA MMILIKI WA CHUO HIKI MR MZIRAI HAKIKA ANAJITAHIDI KUFANYA MAMBO MAZURI JAPO KUNA CHANGAMOTO AMA MAZINGIRA MAGUMU YANAYOMZUNGUKA
    PILI NIWASHUKURU WANAFUNZI AMBAO WANAJIANDAA NA MITIHANI YA KUMALIZA MUHULA LAKINI PIA KUMALIZA CHUO KWA UJUMLA...KWA MASIKITIKO MAKUBWA NATOA POLE KWA WANAFUNZI WALIOIAMINI DACICOSTUA LAKINI LEO HII IMESHINDWA KUWATETEA NI KIPINDI KIFUPI SANA MTAKUWA KATIKA HATMA NZURI YA SERIKALI ILIYOTUKUKA,,.........NAWATAKIA MASOMO MEMA NA KWA WALE WANAOJIANDAA NA MITIHANI KILA LA KHERI
    Like · · April 8 at 9:15am
  • MAN MOE ndani ya DACICO FM ni shida.
    Like · · · April 7 at 4:56pm
  • Mambo mzima jamani
    Like · · March 15 at 11:20am via mobile
  • ndugu zangu wana DACICO ,nilijiaminisha kuwa sisi ni ndugu hata zaidi ya ndugu wa damu, nikiwa kama mmoja wa wanafamilia wa DAR ES SALAAM CITY COLLEGE habari hizi zimenishtua na kunihuzunisha sana kwa kuwa tuliamini kila tulichokiacha tukiwa kama viongozi wa awamu iliyopita kitazidi kuenziwa na kutunwa kwa manufaa ya wanadacico ,tulijipa moyo kuwa yote tuliyoyafanyia kazi yataendelezwa hata wakati tutakapokuwa mbali.
    Nikiwa kama mwanafamilia wa DACICO na mtu mwenye nia njema na DACICO sikuwahi kuwaza au kufikiria kama siku moja sisi kama wanafunzi tutakuja kufikia hatua ya kufarakana na kutengana hadi kufikia hatua ya kupingana wenyewe kwa wenyewe,.
    ninachokiamini ni kwamba wana DACICO tunahitaji maendeleo katika chuo na zaidi ya yote tunahitaji elimu iliyo bora na yenye kukidhi mahitaji ya soko la ajira hapa nchini na nje ya nchi pia.
    daima tumekuwa tukifanya maamuzi yaliyo sahihi katika kutafuta maendeleo ya chuo chetu, siwezi kuwapinga wanachuo wenzangu kwa hatua mliyoichukua ya kumuengua rais wa serikali ya wanafunzi, ila ninachowaomba tukae chini tufikirie kama watu wenye elimu na wenye hekima na wenye mapenzi mema na chuo., ndugu zangu demokrasia ya kweli inahitaji nguvu, uvumilivu, ukweli na zaidi ya yote uchapaji wa kazi pasipo kuyakimbia majukumu uliyopewa na watu wako.
    Sina mengi ya kuwaambia ndugu zangu ila ninachowasihi. TUWE NA UMOJA KATIKA KUJENGA CHUO NA KUPATA ELIMU ILIYO BORA, NA TUSIWE CHANZO CHA KUKIVURUGA CHUO AU KUPOTEZA AMANI YA CHUO. Naishia hapa kwa leo ila nitoe rai kwa wote ELIMU INAPASWA KUFURAHIWA NA SIYO KUWA KAMA NYAKATI ZA WAKOLONI, TUISHI KWA AMANI PASIPO MIKWARUZO NA MALUMBANO.

    Wapeni salamu zao wote,, Mwanaharakati wa kweli
    DISE PETER( Deogratuius A.Peter)
    Like · · March 6 at 1:43pm