Ijumaa, 17 Mei 2013

HABARI ZILIZOANDIKWA NA GAZETI LA MAJIRA

MAJIRA - GAZETI HURU LA KILA SIKU:


Posted: 16 May 2013 01:06 AM PDT
Mratibu wa Chama cha Watabibu wa Tiba Asili Tanzania (ATME), Bw. Bonaventura Mwalongo (kushoto) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), Magomeni Kagera Dar es Salaam jana, dawa yaasili inayotibu ugonjwa wa ini kwa siku 21. Kulia ni mtaalam na mtengenezaji wa dawa asili nchini,Bw.Abba Ahmed Faqi. Picha na Charles Lucas
Posted: 16 May 2013 12:24 AM PDT
 Meneja wa Kampuni ya Simu za Samsung nchini, Bw. Kishor Kumar (wa pili kulia)akiwaonesha maofisa wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania simu aina ya SamsungGalax S4 yenye teknolojia ya kisasa,wakati wa uzinduzi wa simu hizo, Dar es Salaamjana. Wa pili kushoto ni Meneja Uendeshaji waMaduka ya Vodacom Tanzania, Bw.Elihuruma Ngowi, Meneja Mauzo na Usambazaji wa SamsungSylvester Manyar (kulia)na Meneja Masoko wa Vodacom Ibrahim Kingozi. Wateja watakaotumia simu hizowatapata huduma ya intaneti ya (5GB) bila malipo. Na Mpigapicha Wetu
Posted: 15 May 2013 11:01 PM PDT
Na Florah Temba, Moshi

 KAMATI ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi na Sekretarieti ya halmashauri kuu ya chama hicho Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, imesema haijaridhishwa na ujenzi wa daraja la Rau Mbokomu linalojengwa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, hivyo kuitaka manispaa hiyo kupitia upya ujenzi huo na kuhakikisha magari makubwa hayapiti, hadi pale litakapothibitishwa kuwa liko imara.
Daraja hilo ambalo litagharimu sh. milioni 102 bado halijakamilika lakini limeonekana kubomoka, hali ambayo imesababisha watu kuhofia kuwa
hata kama litakamilika na kukabidhiwa linaweza kuleta maafa kutokana na kujengwa chini ya kiwango.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi iliyotekelezwa na manispaa kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 Katibu wa CCM Manispaa ya Moshi, Aluu Segamba, alisema wao hawajaridhishwa na ujenzi wa daraja hilo ambalo lina umuhimu mkubwa kwa wananchi.
"Sisi si wataalamu lakini naomba niseme kuwa hatujaaridhishwa na ujenzi wa daraja hili,kwani haiwezekani daraja lijengwe halijakamilika lakini libomoke, kunahitajika uangalizi mkubwa hapa ili kuhakikisha daraja hili linakamilishwa kwa kiwango kinachostahili ili kuokoa maafa yatakayoweza kutokea kutokana na kukamilisha chini ya kiwango," alisema Segamba.
Aidha Segamba alisema kwa sasa wanaangalia uwezekano wa kutuma wataalamu ili kwenda kukagua daraja hilo na kujiridhisha kabla halijaanza kutumika.
Katibu huyo alishauri daraja hilo lisitumike kupitisha magari makubwa hata baada ya kukabidhiwa hadi pale watakapokwenda wataalamu kukagua na kujiridhisha hatua ambayo itasaidia kuepuka maafa.
Mjumbe wa NecManispaa ya Moshi, Agrey Marialle alisema licha ya taarifa kutolewa kuwa daraja hilo limeshakamilika kwa asilimia 80 bado kazi ni kubwa na inahitaji umakini wa hali ya juu.
Kwa upande wake mkadiriaji wa ujenzi manispaa hiyo, Charles Huka akizungumza kwa niaba ya mkandarasi wa manispaa hiyo alisema wao wanaridhishwa na ujenzi wa daraja hilo ambalo limekamilika kwa asilimia 80 na kwamba linatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu.
Kwa upande wake Eveta Lyimo msaidizi wa mchumi wa manispaa hiyo alisema mradi wa daraja hilo ambao uliibuliwa na wananchi kama mradi wa TASAF ulianza kujengwa mwaka 2009/2010 na kwamba ulihitajika uwe umekamilika lakini kutokana na mvua umeshindwa kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Posted: 15 May 2013 11:03 PM PDT
Na David John
 IMEELEZWA kuwa katika kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa (VISION 2025) Tanzania imejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo MKUKUTA yenye malengo ya kuhakikisha kiwango cha ukosefu wa ajira kinapungua.
Akizungumza katika mkutano uliwakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mkuu wa Ajira, Ally Msack alisema malengo hayo yanalenga kupunguza ajira isiyotimilifu, utumikishwaji wa watoto unapungua na uwepo wa hifadhi ya jamii kutokana na ajira.
Msack aliongeza kuwa kwa sasa imebakia miaka miwili kufikia malengo ya

maendeleo ya Millenia MDGS ambapo mwaka 2015, malengo ya Mkukuta11 2010/11 -2014/15 na malengo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2011/12-2015/16 ambapo nchi inapaswa kutoa taarifa ya viwango vya viashiria vya malengo hayo.
Alisema kwa Tanzania zaidi ya asilimia 75.1 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi wanajihusisha na shughuli zilizopo katika sekta zisizo rasmi kwa maana hiyo utafiti unagusa sehemu kubwa ya nguvu kazi na utaiwezesha Serikali kupata picha halisi ya hali ya ajira nchini.
"Unajua utafiti huu unawezesha kutoa taarifa juu ya hali ya ajira nchini katika sekta rasmi na isiyo rasmi, utumikishwaji wa watoto, hali ya hifadhi ya jamii, hali kipato nchini, matumizi ya muda na ajira mpya zilizozalishwa katika sekta zote kwa kipindi husika (2006-2013).
Alisema viashiria hivi vya soko la ajira ndiyo kigezo kikubwa kinachotokea picha halisi ya mafanikio ya kiuchumi na kuchochea maendeleo ya nchi.
Aliongeza kuwa kwa mara ya mwisho utafiti huo ulifanyika mwaka 2006 na kuwezesha nchi kupata viashiria vyote muhimu vya soko la ajira vikiwemo vya MkukutaMalengo ya Maendeleo ya Millenia MDGS mipango ya maendeleo ya Taifa na kazi yenye staha.
Hata hivyo ili kupanga matumizi sahihi nguvu kazi kwa maendeleo ya kiuchumi lazima nchi iwe na taarifa sahihi ya soko la ajira, hivyo mchakato huo wa masuala ya ajira na kazi ni masuala mtambuka ambayo juhudi za pamoja zinahitajika kati ya Serikali na taasisi za elimu na utafiti wawekezaji, mashirika yasiyo ya kiserikali, wabia wa maendeleo waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Posted: 15 May 2013 11:09 PM PDT

Na Pendo Mtibuche,
Dodoma

 MFUKO wa Pensheni ya Mashirika ya Umma ( P P F ) umesema kuwa kwa muda wa siku tatu za maonesho ya mifuko ya hifadhi ya jamii yanayofanyika mjini Dodoma chini ya usimamizi wa Mamlaka ya mifuko hiyo (SSRA) umefanikiwa kutembelewa na wananchi wapatao 572 na kupata elimu.
Akizungumza na gazeti hili katika viwanja vya maonesho hayo vya Mwalimu Nyerere Square, Meneja wa Kanda ya Mashariki na Kati, John Mwalisu alisema kuwa maonesho hayo ya mifuko ya hifadhi ya jamii yamekuwa na manufaa makubwa kwa jamii ya mkoa
huo.
Alisema kuwa kwa muda wa siku tatu za maonesho hayo mfuko wao wa PPF umefanikiwa kutembelewa na wananchi mbalimbali wapatao 572 lakini pia wamefanikiwa kutoa taarifa zaidi ya 217 za michango ya wanachama wao.
Mbali na hilo pia alisema kuwa walifanikiwa pia hata kuandikisha wanachama wapya wakiwemo wabunge ambaowameonesha kuufurahia mfuko wao na kuahidi kueneza ujumbe huo kwa wabunge wengine.
Akizungumzia hali halisi ya mfuko huo alisema upo katika hali nzuri kwani unaweza kulipa madeni yake na hata kubakiwa na ziada na kueleza kuwa thamani ya mfuko huo kwa sasa ni sh. trilioni 1.09 lakini lengo lao hadi kufikia 2015 mfuko huo uwe na thamani ya sh.trilioni 2.
Akizungumzia suala la wanachama wa mfuko huo kwa nchi nzima wanafika zaidi ya 218,000 ambapo kwa mwezi mfuko huo unatoa zaidi ya bilioni tatu kwa ajili ya pensheni za wastaafu.
Kwa upande wake naye Ofisa Mwandamizi wa uwekezaji katika mfuko huo, Anna Shayo akizungumzia hali halisi ya uwekezaji katika mfuko huo alisema kuwa mfuko huo umewekeza katika mali zinazohamishika na zisizohamishika.
Alisemakuwa wamefanikiwa kuwekeza katika majengo ya kuishi, majengo ya biashara, hisa za makampuni wamefanikiwa kuwekeza katik a vitegauchumi ambavyo riba zake zinajulikana kabla.
Kwa upande mwingine pia alisema kuwa wamefanikiwa kuwekeza katika mikopo amb a p o kwa s e h emu wamefanikiwa kujenga baadhi ya majengo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Ukumbi wa Bunge, majengo mengine Arusha na hata kuwa na saccosza wanachama wa PPF 42 ambazo wameshazikopesha bilioni 54 tangu mwaka 2004.
"Kwa upande wa saccosmwezi huu yaani Mei tunakusudia kutoa bilioni moja nyingine kwa ajili ya kufungua saccosnyingine mbili katika jiji la Dar es Salaam na hivyo tutakuwa na saccos44, hayo ni mafanikio ya mfuko," alisema.
Kwa upande wake Ofisa uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Megele akizungumzia suala zima la wao kushiriki maonesho hayo alisema kuwa mfuko wa pensheni wa PPF umeshiriki maonesho hayo lengo likiwa ni kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo.
Alisema kuwa umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko huo ni kutokana na kuwa na faida nyingi ambazo ni pamoja na kuwepo kwa fao la uzee, ugonjwa, kifo, wategeneziu, elimu, kiinua mgongo na fao la kujitoa.
Akizungumzia mafanikio ya mfuko huo alisema kuwa umewezesha kuwasomesha zaidi ya watoto 1,333 katika shule za msingi na sekondari katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Alisema kuwa mfuko huo ulifikia uamuzi wa kuwasomesha watoto hao kutokana na kuwepo kwa tatizo kwa wasimamizi wa mirathi pindi wazazi wa watoto hao wanapopoteza maisha.
Alisema kuwa hadi kufikia Desemba mwaka jana jumla ya sh. milioni 682.9 zililipwa kama mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi hao.

Posted: 15 May 2013 10:41 PM PDT
Na Steven William, Muheza

 WAUGUZI wa Afya katika Hospitali Teule wilayani Muheza wamedai kwamba wamekuwa wakicheleweshewa mishahara yao katika hospitali hiyo hali ambayo inasababisha wafanye kazi katika mazingira magumu.
Hayo yalisemwa katika risala ya wauguzi katika siku ya wauguzi duniani iliyoadhimishwa kiwilaya hivi karibuni katika Kijiji cha Magoda ambayo ilisomwa na Furaha Kiswaka.
Alisema kuwa wafanyakazi wa hospitali wamekuwa wakicheleweshewa mishahara hali ambayo inawafanya washindwe kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Kiswaka alisema pia wauguzi hao wanakabiliwa na tatizo la
nyumba kwa wanaoishi vijijini ambapo wanaishi katika makazi duni.
Alisema kuwa wauguzi wengine wanaishi mbali na vituo vya kufanyia kazi kitu ambacho wanahatarisha maisha yao hasa wakati wa usiku wanapokuwa na zamu huku wakishauri panapojengwa zahanati pajengwe na nyumba ya muuguzi.
Kiswaka alisema kuwa wauguzi wanakabiliwa na upungufu wa vifaa tiba, vifaa vya usafi na mahitaji muhimu kwa ajili ya usafi ambapo alisema mganga mkuu wa wilaya amekuwa akijitahidi kupatikana vifaa hivyo isipokuwa hospitali ya wilaya Teule bado kuna uhaba mkubwa wa dawa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Muheza, Ibrahim Matovu ambae aliwakilishwa na Kaimu wake, Maurd Mbugi aliwataka wauguzi kufanya kazi kwa moyo mmoja ili kuboresha afya za wananchi na hatimae kuongeza uchumi wa nchi.
Alisema kuwa matatizo yote waliyoyaeleza ameyasikia na atayafanyia kazi kwa kuyapeleka kunakohusika ili yafanyiwe kazi na kuwataka wasife moyo.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Zahanati ya Magoda, Leticia Ibrahim alisema kuwa zahanati hiyo wanatibu zaidi ya wagonjwa 20 kwa siku pamoja na kutoa huduma ya CHF.
Nae Muuguzi Mkuu, Victoria Wasapa aliongoza kuwaapisha wauguzi katika sherehe hiyo ili wawe na nidhamu katika kazi.

Posted: 15 May 2013 10:38 PM PDT
Na Steven William, Muheza
 ZAIDI ya miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.9 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Muheza mkoani Tanga
Miongoni mwa miradi hiyo itakaguliwa, kufunguliwa na kuweka mawe ya msingi pindi utakapowasili wilayani humo Mei 18, mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya Muheza, Subira Mgalu ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na ujio wa Mwenge huo wa Uhuru wilayani humo.
Alisema kuwa miradi ambayo itapitiwa na Mwenge huo ni
pamoja na kukagua mradi wa hifadhi ya bahari Kijiji cha Kigombe, kufungua ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Kijiji cha Mtiti.
Miradi mingine itakayotembelewa na Mwenge huo ni kukagua shamba la miti katika Kijiji cha Kigombe na kuweka jiwe la msingi Zahanati ya Kijiji cha Kilulu.
Mkuu huyo wa wilaya alitaja miradi mingine itakayopitiwa na kuweka jiwe la msingi kisima cha maji kilichopo Mang'enya Kata ya Genge na kukagua mabweni ya wanafunzi shule ya Livingstone.
Alisema kuwa baada ya Mwenge huo kukagua miradi hiyo utakagua mabanda ya maonyesho katika uwanja wa Jitegemee ambako mwenge huo utakesha mpaka asubuhi.
Kwa upande wake Mratibu wa Mwenge Wilaya ya Muheza, Athumani Komolanya aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuupokea mwenge huo katika barabara ambapo utapokelewa Kijiji cha Mjesani ukitokea wilayani Mkinga na asubuhi yake utakabidhiwa Kijiji cha Masaika ukielekea wilayani Pangani.
Posted: 15 May 2013 10:36 PM PDT
Na Yusuph Mussa, Lushoto

 BAADHI ya walimu wilayani Lushoto wameifananisha elimu ya Tanzania kama maghorofa mabovu yanayojengwa jijini Dar es Salaam, kwani inazidi kushuka kutokana na mfumo mbovu wa mitaala na uingizaji holela wa vitabu vya kufundishia na kujifunzia shuleni.
Wakizungumza juzi kwenye mkutano wa wakuu wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Bumbuli, ulioandaliwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba waliitaka Serikali ishirikishe wadau kwenye
mitaala.
"Kama mchakato wa Katiba Mpya unavyoshirikisha wadau, vivyo hivyo utungaji ama uanzishwaji wa mitaala mipya iwashirikishe wadau ili kupata mitaala itakayokubalika au sivyo elimu yetu itaendelea kuwa kama maghorofa ya Dar es Salaam.
"Itazidi kuporomoka kwa vile haina misingi mizuri. Hivi inakuwaje mtoto wa darasa la kwanza anakwenda shuleni na madaftari tisa, turudishe utaratibu wa K tatu yaani Kusoma, Kuandika na Kuhesabu" alisema Mratibu wa Elimu Kata ya Soni, Luth Msagati.
Mratibu wa Elimu Kata ya Milingano alisema mitaala iliyopo kwa sasa hata walimu hawaijui, hivyo ni vigumu mwalimu kumfundisha mwanafunzi akaelewa, huku akisema changamoto nyingine ni kuwaingiza sekondari wanafunzi waliopata alama 70.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kwamongo, Anthony Kihiyo alisema kwa Serikali kuruhusu wanafunzi wa shule za kata na zile za Mtakatifu kufanya mtihani mmoja ni sawa na kumpambanisha Francis Cheka na mgonjwa aliyelazwa Hospitali ya Muhimbili.
"Wanafunzi wa shule za kata kufanya mtihani mmoja na wale wa shule binafsi ni kuwaonea. Hata mabondia uzito wao unapimwa na unatakiwa ulingane ndipo wapigane," alisema Kihiyo.
Makamba alisema pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuunda tume ya kuchunguza kisa cha matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, bado walengwa ambao ni walimu hawajapewa nafasi ya kutoa maoni yao juu ya suala hilo.
"Sauti ya mwalimu haijasikika zaidi ya wanasiasa na makundi mengine, lakini walimu hasa ndiyo wanajua kitu gani kimefanya wanafunzi wamefanya vibaya, sababu ndiyo wanakaa na wanafunzi hawa kati ya saa nane hadi tisa," alisema Makamba.
Makamba aliungana na walimu kwa kusema mitaala isitegemee mapenzi ya waziri aliyepo madarakani ama Serikali inayoongoza dola, bali iwe ni suala la kitaifa ambapo kila Serikali ama waziri atakaekuja atafuata mitaala hiyo.
Posted: 15 May 2013 10:35 PM PDT
Na Yusuph Mussa, Lushoto

UMEME kupita juu ya Kijiji cha Wanga kilichopo Kata ya Mgwashi wilayani Lushoto na wao kushindwa kuwekewa trasfoma ili wapate huduma hiyo kumekigharimu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wananchi kuamua kumchagua Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho kupitia CHADEMA.
Wakizungumza juzi kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba wananchi walisema kupitisha nyaya za
umeme juu na kuwapelekea wanakijiji wenzao wa Mgwashi ni kuonesha Serikali ya CCM haiwajali.
"Umeme kupita juu kwa juu kwenda Kijiji cha Mgwashi na kutuacha sisi, tumeona Serikali haitujali. Lakini pia tunachangishwa michango mara mbili mbili, kwani tulikamilisha boma (darasa) la Shule ya Sekondari Handeni.
"Awali tulijenga likakamilika kwa kutoa kila mtu sh. 5,000, lakini kwa vile lilijengwa chini ya kiwango ikabidi tuchangishwe tena sh. 3,000. Wananchi wananyanyaswa kwa kuambulwa (kushikwa faini) kuku ili kujenga tena boma hilo," alisema Athuman Amir.
Makamba aliwataka wananchi wawe na subira kwani ipo mikakati ya kufikisha umeme kwenye kata kadhaa kwenye Halmashauri ya Bumbuli ikiwemo eneo hilo.
Pia alisema kwa kupata halmashauri wataweza kuipandisha barabara ya Mbelei- Mgwashi- Milingano- Mashewa kuwa chini ya Wakala wa Barabara (TANROADS).
Posted: 15 May 2013 10:26 PM PDT
Na Rehema Maigala

KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbaraka Abdul Wakili amesema kukua kwa teknolojia duniani kunasababisha kuenea kwa wingi uhalifu.
Hayo alisema jana wakati akifunga mkutano wa 18 wa Maofisa wa Jeshi la Polisi Katika Nchi za Kanda ya Kusini mwa Afrika (SARPCCO) ambao ulikuwa na lengo la kujadili jinsi ya kukabiliana ya uhalifu.
Alisema wakuu hao kutoka nchi 14 wamekutana kwa ajili ya
kukaa pamoja na kuweka mikakati ya ushirikiano ili kupambana ugaidi ulioenea katika nchi za Afrika.
"Hivi sasa uhalifu umevuka mipaka kwa sababu ya kukua kwa teknolojia hivyo inatakiwa kukaa pamoja na kujadili suala hili ili liweze kupungua,"alisema Wakili.
Aliongeza kusema kuwa nchi moja ikikaa peke yake ili iweze kutatua tatizo la ugaidi haiwezi kufanikiwa inatakiwa kukaa pamoja na nchi zingine ili kupanga nini cha kufanya.
Alisema kuwa kukaa kwa nchi zaidi ya tatu kutasaidia kuleta mafanikio makubwa kwani nchi nyingine inakuwa na uwezo mdogo na nyingine inakuwa na uwezo mkubwa wa kujua nini cha kufanya ili kumaliza tatizo la uhalifu.
Vilevile alisema hivi sasa wahalifu wengi hutumia teknolojia ya kisasa ili kufanikiwa na mambo yao wanayoyafanya.
Naye Mwenyekiti wa SARPCCO, Saidi Mwema ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania mkutano huo umesaidia kujua njia mbalimbali za kuweza kuwafichua wahalifu wanaozitesa nchi za Afrika.
Alisema kuwa, sasa hivi wanataka kufichua vyanzo vinne ambavyo ndivyo vya uhalifu ni wachocheaji, wawezeshaji na wanaojilipua wenyewe kwa ajili ya uhalifu.
Mwema alisema kuwa k a t i k a mk u t a n o h u o watapeana taarifa na kubadilishana taarifa hasa katika makosa ya uharamia baharini na kuzagaa kwa silaha katika nchi za Afrika.
Posted: 15 May 2013 10:24 PM PDT
Na Heri Shaaban
 WANACHAMA 331 wa Umoja wa Wauza Mitumba wa soko la Mchikichini (MIMCO)wameanza kupewa viwanja kwa kila mwanachama wa umoja huo ili wajenge nyumba za kuishi.
Viwanja hivyo walivyopewa wanachama wameuziwa na umoja wao wa MIMCO baada kununua shamba zaidi ya heka 20 eneo la Pemba Mnazi Wilayani Temeke,ambapo kila mwanachama hulipia sh.milioni 1.2 pamoja na kupatiwa leseni ya kiwanja kilichopimwa na Serikali.
Akisoma taarifa ya Bodi ya MIMCO Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bw.
Ajali Mohamed alisema kila mwanachama hai wa umoja huo ambaye hadaiwi ada atapatiwa eneo la kujenga.
Alisema kila mwanachama atagawiwa eneo la kujenga baada kukamilisha taratibu na fedha atalipa kwa awamu tofauti kwa kuanzia sh. 400,000.
"Madhumuni ya wanachama wangu kuwagawia kila mmoja kiwanja ni ili wajenge nyumba za kuishi watoke katika nyumba za kupanga halafu waweze kupata mikopo kwa urahisi kutokana dhamana ya leseni zao," alisema Bw. Mohamed.
Bw.Mohamed alisema umoja huo ulianzishwa mwaka 2005 mwezi Mei kikiwa na wanachama 331 kati yao wanawake 24 wanaume 307 na wajumbe wanane wa bodi hiyo.
Aliwataka wanachama wa umoja huo kulipa ada kila mwaka ili umoja huo uweze kukua sambamba na kukuza hisa zao.
Pia bodi hiyo imependekeza viwanja hivyo wauziwe wanachama walio hai ambao hawadaiwi hisa wala ada na mtu atakayepewa kiwanja alipe pesa ndani ya miezi mitatu ili waweze kupata fedha kwa maendeleo ya MIMCO na wanachama wake.
Kwa upande wake Mwenyekiti Mstaafu wa soko la Mchikichini Bw. Deo Mkali, aliwataka wanachama wa MIMCO wachague viongozi bora na si bora viongozi ili chama hicho kisipoteze mwelekeo katika uongozi wake.
Bw.Mkali alisema chama hicho kinapofanya chaguzi zake kichague viongozi bora na wenye upeo katika utendaji ambao watasaidia chama kupiga hatua zaidi katika elimu ya ujasiriamali.
Pia alikitaka chama hicho kiwape kipaumbele wanawake kuwa sehemu ya uongozi wa bodi na viwanja vigawiwe pasipo dhana ya ubaguzi.
"Nimestaafu kwa hiari yangu ila natoa wosia kwa chama tujiepushe na wanachama wanaojitokeza kuleta vurugu na uchochezi sokoni kwa ujumla pamoja na kujiepusha na masuala ya udini, siasa ukabila na ubaguzi vinavyoashiria kujitokeza sokoni kwa sasa,"alisema Bw.Mkali.
Posted: 15 May 2013 10:15 PM PDT
Na Queen lema, Arusha

 BARAZA la Madiwani Halmashauri ya ArushaVijijini,WilayayaArumeru limewa simamisha kazi watu mish iwatano wa halmashauri hiyo kwatuhuma za ubadhirifu.
Watumishi haowanakabiliwanatuhuma ya ubadhirifuwash.milio ni 56 6,654,173zilizoto lewa kwaajili yakujenga v yumbavyam ada rasaka tikabaadhi ya shule za sekondari zahalm ashaurih iyo.
Mwenyekiti wa HalmashauriyaArusha,Bw.SaimonSaning'oakitangaza uamuzi huo jana, a lisemamhusikamkuu katikakatikashauri hilo ni wasaid izi wake watatu .
Alisemawatumishi hao wamesimamishwa kupishauchunguzi.Aliongezakuwa wamebainikabaada yaMku rugenzi Mtendaji aliyehamishiwa katika Halmashauri hiyo kumuagiza Mkaguzi
wandanikatikahalmashauri hiyo, Bw. Jackson Laizer, kufanya ukaguzi.
Mwenyekiti huyo alisema wamebaini wizi wa fedha hizo Februari, mwaka huu na kuwa mchezo ulianza kufanyika Desemba mwaka uliopita.
Alisema kuwa, fedha hizo hazikupelekwa shuleni kama ilivyoelekezwa.
Mkaguzi huyo anadaiwa kubaini kuwa hati za malipo ziliandaliwa nje bila mfumo funganishi wa EPICOR na malipo kufanyika bila hidhini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, malipo kufanyika bila vifungu vya bajeti na hati za malipo zilizoandikwa kwa mkono.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha kwa sasa, Fedelist Lumato akizungumzia tukio la kusimamishwa kwa watumishi hao, alisema kuwa watumishi hao watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Posted: 15 May 2013 10:18 PM PDT
Na Queen lema, Arusha

BARAZA la Madiwani Halmashauriya ArushaVijijini,WilayayaArumeru limewasimamishakazi watumish iwatano wahalmashauri hiyokwatuhuma zaubadhirifu.
Watumishi hao wanakabiliwanatuhuma yaubadhirifuwash.milio ni 56 6,654,173zilizoto lewa kwaajili yakujenga vyumbavyamada rasaka tikabaadhi ya shule za sekondari zahalmashaurih iyo.
M wenye kitiwaHal mashauriyaArusha,Bw.Sai monSaning'o, akitangaza uamuzi huo
jana,a lisemamhusikamkuu katikakatikashauri hilo ni wasaidizi wake watatu .
Alisemawatumi shih a o wamesimam ishwaku pishauchunguzi.Alionge zakuwa wamebain ikabaada yaMku rugenzi Mtendajiali yehamish iwakatikaHalmashauri hiyo kumuagiza Mkaguzi wandanikatikahalmashauri hiyo, Bw. Jackson Laizer, kufanya ukaguzi.
Mwenyekiti huyo alisema wamebaini wizi wa fedha hizo Februari, mwaka huu na kuwa mchezo ulianza kufanyika Desemba mwaka uliopita.
Alisema kuwa, fedha hizo hazikupelekwa shuleni kama ilivyoelekezwa.
Mkaguzi huyo anadaiwa kubaini kuwa hati za malipo ziliandaliwa nje bila mfumo funganishi wa EPICOR na malipo kufanyika bila hidhini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, malipo kufanyika bila vifungu vya bajeti na hati za malipo zilizoandikwa kwa mkono.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha kwa sasa, Fedelist Lumato akizungumzia tukio la kusimamishwa kwa watumishi hao, alisema kuwa watumishi hao watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Posted: 15 May 2013 10:19 PM PDT


 WAANDISHI wahabarinchini wametakiwa kuhakikisha wanajilinda dhidiya maaduiwabayakwaki lekilichoda iwakuwahivisasausalama waonimdogo, anaripoti AnnethKagenda.
Wito huo umetolewaDaresSalaamjananaMwe nyekitiwaMakampuni ya IPPkwenyeMk utanowakenavyom bovya habari ulio lenga kuang alia nikwajinsi ganiusalam awawaand ishi utaboreshwa.
“Lakini ninachoweza kusema nikwamba maran yingiwapowa andishiambao wame kuwa wakihata risham aishay awaa ndishiwenzaokwa kutoa s irinje... jamani naombat abiahiitu iacheili
tusitoemwanya kwa ha owaba yakuhatarisham aisha yetu,” alisema.
Alisema wengine ambaowamekuwa wakisababisha waandishikupigwa,kuteswana kuuawaniviongoz iwasiokuwa waadilifua mbaowamekuwa wakishiriki ananawaandishi wasiokuwa waadilifu kufanyavitendo viovu.
Bw. Mengi alisema kwa muda mrefu sasa Tanzania imekuwa ikitajwa kuwa ni nchi ya amani, amani lakini kwa wakati huu mambo yanayojitokeza yamekuwa yakitisha wananchi.
Hata hivyo, alisema usalama unaotakiwa kwa waandishi ni kuanzia kwa mmiliki pamoja na mwandishi mwenyewe. Mratibu wa Kitaifa katika mtandao wa utetezi haki za Binadamu, Bw. Onesmo Olengurumwa, alisema usalama wa waandishi ni muhimu kwa taifa lolote linalotaka kusonga mbele.
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona kila siku waandishi 30 duniani wanauawa kuteswa na kupigwa.
“Taifa lolote linalotaka maendeleo haliwezi kukwepa waandishi wa habari, lakini pia usalama wa waandishi unatakiwa kwani bila wao hatuwezi kujua ni fedha shilingi ngapi zimeidhinishwa kwa ajili ya maendeleo."
Posted: 15 May 2013 09:38 PM PDT
Grace Ndossa na Mariam Mziwanda

 NAIBU Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kitaifa wa Serikali ya Denmark, Bw. Charlotte Slett, ameshauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ihakikishe malengo ya misamaha ya kodi yanapunguza umaskini na kuleta usawa katika jamii. Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Naibu waziri huyo, alipotembelea Mamlaka hiyo kujua mipango ya miaka mitano iliyowekwa kuhakikisha inapunguza umaskini Tanzania. Alisema Serikali ya Denmark inahakikisha misamaha ya kodi ni
asilimia hamsini kwa hamsini, ambayo haiwaumizi wananchi wake. Hata hivyo alisema Serikali ya Denmark inasaidia Tanzania kila mwaka kwa dola milioni 80 na kwamba watakutana na waziri wa fedha kuangalia ni namna gani wanaweza kusaidia bajeti ya wizara yake. Naye Kamishna Mkuu TRA, Bw. Harry Kitillya, alisema misamaha ya kodi inatolewa kama mtu akikosa sababu za msingi zinazofanya asamehewe au kupunguziwa kodi. Wakati huo huo TRA imezindua awamu ya pili utekelezaji wa mradi wa Mashine za kielektroniki ambayo imelenga kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani. Hayo yalibainishwa jana na Naibu Kamishna MKuu wa Mamlaka hiyo Bw. Rished Bade, alipokuwa anazindua mashine hiyo na kueleza kuwa awamu hiyo imelenga kuanza na kundi la wafanyabiashara 200,000. Alisema matumizi ya mfumo huo kwa miaka miwili ya utekelezaji yameonesha mafanikio katika ukuaji wa makusanyo yatokanayo kodi.

Posted: 15 May 2013 09:32 PM PDT

N a Yu s u p h Mu s s a ,
Lushoto

 BAADHI ya walimu wilayani Lushoto wamefananisha elimu nchini na maghorofa mabovu yanayojengwa jijini Dar es Salaam, kwani inazidi kushuka kutokana na mfumo mbovu wa mitaala na uingizaji holela wa vitabu vya kufundishia na kujifunzia shuleni. Wakizungumza juzi kwenye mkutano wa wakuu wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Bumbuli, uliondaliwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Bumbuli,Bw. January Makamba, walisema Serikali ishirikishe wadau kwenye
utungaji wa mitaala. "Kama mchakato wa Katiba Mpya unavyoshirikisha wadau, vivyo hivyo utungaji au uanzishwaji wa mitaala m i p y a i w a s h i r i k i s h e wadau ili kupata mitaala itakayokubalika vinginevyo elimu itaendelea kushuka. "Itazidi kuporomoka kwa vile haina misingi mizuri. Hivi inakuwaje mtoto wa darasa la kwanza anakwenda shuleni na madaftari tisa, turudishe utaratibu wa 'K' tatu yaani masomo ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu" alisema Mratibu wa Elimu Kata ya Soni, Bi. Luth Msagati. Mratibu wa Elimu Kata ya Milingano alisema mitaala iliyopo kwa sasa hata walimu hawaijui, hivyo ni vigumu mwalimu kumfundisha mwanafunzi akaelewa, huku akisema changamoto nyingine ni kuwaingiza sekondari wanafunzi waliopata alama 70.Mkuu wa Shule ya Sekondari Kwa Mongo,Bw. Anthony Kihiyo, alisema kwa Serikali kuruhusu  wanafunzi wa shule za kata na zile za Mtakatifu kufanya mtihani mmoja ni sawa na kumpambanisha Francis Cheka na mgonjwa aliyelazwa Hospitali ya Muhimbili. "Wanafunzi wa shule za kata kufanya mtihani mmoja na wale wa shule binafsi ni kuwaonea. Hata mabondia uzito wao unapimwa na unatakiwa ulingane ndipo wapigane," alisema,Bw. Kihiyo. Kwa upande wake Bw. Makamba alisema pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuunda tume ya kuchunguza kiini cha matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, bado walengwa ambao ni walimu hawajapewa nafasi ya kutoa maoni yao juu ya suala hilo .


Posted: 15 May 2013 09:27 PM PDT
Na Allan Ntana, Tabora

 SERIKALI mkoani Tabora, kupitia kwa Ofisa madini mkazi wa mkoa huo, BW. Elias Mutelani, imeagiza kufungwa kwa machimbo ya dhahabu yaliyopo katika kijiji cha Kapumpa, kata ya Kitunda, wilayani Sikonge, mkoani humo na wachimbaji wote wameamriwa kuondoka mara moja katika eneo hilo ili kuweka utaratibu na usimamizi mpya wa uchimbaji madini hayo. Ak i t o a t a a r i f a y a kufungwa kwa machimbo hayo, Bw. Mutelani alisema kuwa Serikali ya mkoa imeagiza kufungwa mara moja kwa shughuli zote za
uchimbaji katika eneo hilo ili kuweka utaratibu mpya utakaowezesha shughuli za uchimbaji zifanyike kwa utaratibu unaoeleweka vizuri zaidi. Akizungumzia agizo la kufungwa machimbo hayo afisa mtendaji wa kata ya Kitunda, Bw. Julius Ndege, alisema ni kweli machimbo yamefungwa rasmi, lengo likiwa ni kuweka utaratibu mzuri wa namna gani uchimbaji wa madini hayo uweze kufanyika na kubainisha kuwa agizo hilo limetolewa na uongozi wa Serikali ya mkoa. Kufungwa kwa machimbo hayo kumeleta kizaazaa na hali ya sintofahamu kwa wachimbaji zaidi ya 4,000 waliokuwepo katika eneo hilo, baada ya Mei 3, mwaka huu kukuta mabango la kuwataka waondoke. Wa k i z u n g u m z a n a waandishi wa habari mkoani hapa, Mwenyekiti wa wachimbaji hao, George Mtasha, alisema baada ya kupewa amri ya kuondoka, baadhi yao walipotea njia na wengine zaidi ya 2,000 walilazimika kutembea kwa miguu hadi Sikonge mjini umbali wa zaidi ya kilomita kutokana na kukosa nauli. Bw. Mtasha alibainisha kuwa askari walipofika katika machimbo hayo, walianza kuwafukuza huku wakichoma mahema ambayo walikuwa wakitumia kulala. Katibu wa kamati ya wachimbaji hao, Bw. Ibrahim Tundu, alisema kuwa katika eneo hilo dhahabu ipo ya kutosha sana na hadi sasa kuna askari polisi ambao wamebakisha wachimbaji wachache.

Posted: 15 May 2013 09:06 PM PDT
Na Salim Nyomolelo

 MBUNGE wa Fuoni kwa tiketi ya CCM, Bw.Said Mussa Zuberi, ameshangazwa na wabunge kupitisha bajeti za wizara mbalimbali, lakini fedha hizo hazipelekwi kama zinavyoidhinishwa.
Alitoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Alisema inashangaza wabunge kupitisha bajeti, lakini
fedha zinazotolewa ni kidogo na vilevile hazipelekwi zote kwenye wizara husika.
 Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya CCM,jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Bw. Nape Nnauye, alisema mkutano wa Kamati Kuu ya CCM uliofanyika hivi karibuni, umeitaka Serikali kuhakikisha mizizi inang’olewa ili kukomesha matukio ya aina hiyo.
Nape alisema kuwa CCM i m e r i d h i s h w a n a h a t u a zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi wakati wa tukio hilo. Alisema Kamati Kuu, ililaani matukio hayo kutokana na kuwa yanavuruga amani, upendo na umoja wa Watanzania.
“Kamati Kuu imeishauri Serikali kuongeza kasi kuwasaka na kung’oa mzizi huo ili kukomesha vitendo vya namna hiyo,” alisema, Bw. Nape
Hata hivyo, Bw. Nape alisema Mei 18 na 19 mwaka huu Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, atakutana na wabunge wa chama chake pamoja na sekretarieti ya chama ili kupata maoni ya wabunge pamoja na kushauriana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Bw. Nape alisema kuwa miongoni mwa ajenda zitakazozungumzwa ni pamoja na utekelezaji wa ilani ya chama na mwenendo wa maendeleo pamoja na kuweka mikakati thabiti ya maendeleo.
“Kikao kitakuwa kati ya mwe n y e k i t i , wa b u n g e n a sekretarieti ambayo ndiyo wamiliki wa ilani inayotekelezwa,” alisema.
Alisema kuwa baada ya kikao hicho na wabunge hao, Kamati Kuu ya CCM itakutana tena Mei 20 na 21 ili kujadili mambo yatakayoongelewa katika kikao cha wabunge.
Posted: 15 May 2013 09:06 PM PDT
Na Goodluck Hongo

 MBUNGE wa Fuoni kwa tiketi ya CCM, Bw.Said Mussa Zuberi, ameshangazwa na wabunge kupitisha bajeti za wizara mbalimbali, lakini fedha hizo hazipelekwi kama zinavyoidhinishwa.
Alitoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Alisema inashangaza wabunge kupitisha bajeti, lakini fedha zinazotolewa ni kidogo na vilevile hazipelekwi zote kwenye wizara husika.
 Alitolea mfano mradi wa Kurasini jijini Dar es Salaam, ambapo zilitakiwa zitolewe zaidi ya sh. bilioni
120 kwa ajili ya mradi huo, lakini ni kiasi cha sh.bilioni 10 ndizo zilizotolewa na Serikali.
“Kama kwe l i t u n a t a k a kutengeneza ajira kwa kusaidia vijana zaidi ya 100,000, kwa nini bunge likipitisha bajeti ya Wizara fedha hazipelekwi zote?”Alihoji Bw. Zuberi.
Alibainisha kuwa mradi huo wa Kurasini ambapo Wachina wangewekeza zaidi ya sh.bilioni 60 unashindikana hadi leo kutokana na Wizara kutopewa fedha zote kama ilivyoomba katika bajeti iliyopita, ambapo watu wengi wangepata ajira.
Alishangazwa na kitendo cha bunge hilo kutenga muda kidogo kuchangia bajeti ya wizara hiyo wakati hiyo ndiyo wizara muhimu kwani ndiyo inatoa ajira kupitia viwanda.
Naye Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Bw. Nimrod Mkono, alisema hawezi kuunga mkono hoja ya bajeti ya wizara hiyo hadi pale atakapopata majibu kutoka kwa Waziri, Dkt.Abdalaah Kigoda, kuhusiana na matatizo ya wizara hiyo.
Alisema ofisi ya Brela imeoza na haifai kuendelea kutoa huduma hizo, kwani hata ofisini haina viti wala meza, majalada yamejaa na yametunzwa holela hadi karibu na chooni.
Alisema mtu anachukua miaka kati ya miwili hadi mitatu ndipo apate usajili. “Ofisi ya Brela imeoza nakuomba waziri fumua hii na kuisuka upya kwa mazingira hayo hataweza kufanya biashara kwa hali hii, kwani wizara hii ina matatizo makubwa lakini hawa Brela wanafanya nini kwa kweli siungi mkono hoja hadi nipate majibu ndiyo nitaunga mkono hoja,” alisema Bw. Mkono
Naye Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa, alisema wamachinga nchini wamekuwa wakipigwa mabomu badala ya wahusika kukaa chini na kutafuta njia ya kutatua matatizo yao.
Akiwasilisha bajeti ya Wizara yake kwa mwaka 2013/2014 Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Kigoda aliliomba bunge kupitisha kiasi cha zaidi ya sh.bilioni 108 kwa mwaka wa fedha ujao ili Wizara iweze kutekeleza majukumu yake.
Alisema sh. bilioni 29 zitatumika katika matumizi ya kawaida, sh. bilioni 22 kulipa mishahara na sh. bilioni 78 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Posted: 15 May 2013 08:56 PM PDT
Na Esther Macha, Mbeya
 WANAFUNZI 15 wa Shule ya Sekondari ya Wazazi ya Lupata wilayani Rungwe, mkoani Mbeya wanashikiliwa na polisi kwa kosa la kuchoma moto bweni wakipinga hatua ya wanafunzi wenzao kusimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Diwani Athuman, alisema tukio hilo lilitokea Mei 14, mwaka huu saa 2.00 usiku.
Kamanda Athuman alisema kuwa wanafunzi hao baada ya
kuona wenzao watatu wamesimamishwa masomo walianza kufanya vurugu usiku na kuanza kuchoma moto bweni moja la wanafunzi wa kiume. Kamanda Athuman aliwataja wanafunzi waliosimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu shuleni hapo kuwa ni, Joseph Robert (18), Mwita Chacha na Daniel David (18).
“Hawa wanafunzi watatu waliosimamishwa masomo walihamasisha wenzao kuunga mkono kupinga adhabu hiyo kwa kufanya vurugu na kuchoma bweni hilo,”alisema Kamanda Athuman.
Alisema bweni lililochomwa moto walikuwa wanaishi wanafunzi ambao hawakuwa tayari kuunga mkono uvunjifu huo wa amani shuleni hapo. Aidha Kamanda Athuman alisema wanafunzi 15 wanashikiliwa na polisi wakiwemo vinara wa fujo hizo.
Kuhusu mali zilizoharibiwa, Kamanda huyo alisema thamani halisi ya uharibifu uliotokea bado haijajulikana. Kamanda Athuman ametoa wito kwa jamii hasa wanafunzi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake watatue matatizo kwa njia ya mazungumzo kwa kufuata mamlaka husika.
Posted: 15 May 2013 08:53 PM PDT
Na Sophia Fundi, Karatu

 HOS P ITALI Te u l e y a Karatu wilayani hapa nusura igeuke uwanja wa masumbwi baada ya kutokea mgogoro mkubwa baina ya pande mbili zilizokuwa zikigombea maiti kuhusu eneo atakalozikwa marehemu.
Tafrani hiyo ilidumu kwa saa kadhaa mjini hapa jirani na chumba cha kuhifadhia maiti. Hali hiyo ilitokea baada ya mume wa marehemu, Bw. Sauli Zakaria, kutaka kwenda kumzika mke wake, Eliza Mathayo, nyumbani kwao mkoani Mtwara.
Hata hivyo ndugu wa marehemu waligoma wakihoji iweje
azikwe mbali na nyumba yake waliyokuwa wakiishi. Wakizungumza na gazeti hili, ndugu wa marehemu walisema hawakubaliani na ndugu yao kuzikwa mbali (mkoani Mtwara) kwani ndugu zake wengine hawataweza kwenda kushiriki mazishi.
Akizungumza kwa njia ya simu baada ya ndugu hao kuzuia maiti hiyo, iliyokuwa isafirishwe jana saa nane mchana kwenda Mtwara, mume wa marehemu, Bw. Zakaria alisema yeye kama mume wa marehemu ndiye ana mamlaka ya kupanga ni wapi azikwe mke wake.
Alisema anashangazwa na ndugu hao kukataa asimzike mke wake ambaye walimpa akiwa hai na kufunga naye ndoa halali. “Leo hii wananikatalia nisimzike ninakotaka... mimi naamua kuwaachia maiti yao na mimi nitaondoka na watoto wangu,”alisema Bw. Zakaria na kuongeza;
“Nimeamua kuwaachia maiti yao hivyo naishia zangu na watoto wangu, wamzike mtu wao.” Baada ya malumbano hayo yaliyochukua muda mrefu, Bw. Zakaria aliwashukuru majirani waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwake na kuwataka kutawanyika kwani msiba hautakuwepo katika eneo hilo.
Baada ya kutoa kauli hiyo alifunga mlango wa nyumba yake na kwenda kusikojulikana huku akiacha maiti ya mke wake hospitali kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
Alipoulizwa kuhusiana na hali hiyo Katibu wa Hospitali hiyo, Bi. Joyce Kajivo, alisema kuwa wao kama viongozi wa hospitali wanasubiri maamuzi ya mume wa marehemu kwani yeye ndiye mwenye maamuzi ya wapi amzike mke wake na taratibu zote za hospitali zimekamilika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni