Na Happynes Mayebele – Dar es salaam.
Timu ya Soka ya Chuo cha Uandishi wa Habari wa habari na Utawala, Dar es Salaam City College(DACICO TANZANIA), Juzi imefanikiwa kuichakaza timu ya soka ya Chuo cha Mlimani professional school of studis (mlimani fc) katika Mechi ya kirafiki iliyochezwa katika uwanja wa Bwaroni jirani na shule ya sekondari ya brilliant Mbezi kwa Msuguri jijinin Dar es Salaam.
Katika Mchezo huo ambao ulikuwa wa marudiano baina ya timu hizo mbili ,mchezo ulianza saa 10:40 kwa saa za afrika Mashariki kutokana na Hali ya Hewa kuwa na mvua, ilisababisha mchezo kuwa wa patashika kutokana na timu ya Dacico kushinda katika uwana wake wa nyumbani ambapo timu ya Dacico iliibuka na ushindi wa kishindo pia wa 1-0 dhidi ya Mlimani Professional School of Studies kwa bao 1-0 kwenye mchezo huo uliokuwa wa Marudio. .
Washindi walijipatia bao katika kipindi cha pili dakika ya 82 ambapo mchezaji , Japhet George wa Dacico f.c, akitokea benchi baada ya kuingia kipindi cha pili alifanikiwa kufunga kwa penalty kufuatia mlinda mlango wa timu ya Mlimani F.c kumchezea madhambi mshambuliaji nyota wa Dacico(Super Sub), Ramadhani Dulla, wakati akielekea kufunga.
Akizungumzia mpambano huo, kocha wa Timu ya Dacico f.c Bwana, Chambuya Maurice "sisi huku tumefuata ushindi pamoja na vikwazo vya uwanja kuwa mbovu na wachezaji kukosa nafasi ya ushindi katika kipindi cha kwanza lakini bado tumekuwa vinara kwa kuubeba ushindi kwa kishindo’’ alisema Chambuya
Hata hivyo, mmoja wa wachezaji kutoka timu ya Mlimani professional studis Bw. Elly Omary alisema “mechi ilikuwa nzuri japo tumekubali kufungwa lakini hawakutuzidi kimchezo maana hata gori hilo moja wamepewa na mwamuzi, wangekuwa wametufunga hata mabao mawili hapo ndiyo tungesema wametuzidi kimchezo pia katika mchezo uwanjani kufungwa au kufunga ni jambo la kawaida lakini endapo tutapatav mchezo mwingine na Dacico hakika tutashinda maana tutajiandaa kwani tumegundua pia kuwa Dacico inao wachezaji wakali" alisema Elly.
Aidha, kocha wa Timu ya Mlimani professional school of studies(mlimani FC) Bw Fredrik Emmanuel alisema "nawashukuru sana wachezaji wote pande mbili kwa kuonesha bidii katika mchezo huu kwani mchezo ulikuwa mzuri na wachezaji wote wamecheza vizuri kwa kuonesha kila timu umahili wake pamoja na uwanja kuwa na matope yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyotangulia kunyesha, lakini wamejitahidi kwa kuonesha kile wanachojifunza” alisema Fredrik. Pia kuhusu kufungwa kwa timu yake alisema”kufungwa ni changamoto ya kuongeza bidii hivyo kipindi kijacho tutajitahidi kwa kuubeba ushindi”.alisema Fredrik.
Sambamba na hayo, mchezo huo ulifikia tamati kwa dacico fc kuibuka na ushindi huo wa bao 1-0. Kwa Upande wa Timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala Dacico kikosi kilikuwa kama ifuatavyo:- Gifti Habibu, Alexandre Ngelezi, Raphael Magitta, abudallah dulla, razack mushi,Baraka,frank.
Na katika kikosi cha mlimani fc ni pamoja na Braiy,Frank,paschal,alpha ,Baraka, afidhi, kefhan, flaivn,jumanne, haruna, mrisho,Fredrik Emmanuel pamoja na morgan britorn.
Mwisho