Jumapili, 4 Mei 2014

DACICO F.C YAIGARAGAZA MLIMANI PROFESIONAL

Na: Recho George/Edger Kaizer,  Mbezi kwa Msuguri Dar es Salaam..

 Timu ya Mpira wa Miguu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala, Dar es Salaam City College,(DACICOFC),hatimaye  imefanikiwa kuifunga Timu ya Mlimani Profesional F.c kwa  1-0  katika mchezo wa kirafiki uliofanyika majira ya jioni katika uwanja wa Bwaloni uliopo mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Salaam Jana.
Mmoja wa Walimu katika Chuo cha DACICO TANZANIA.

Katika mchezo huo ambao mashabiki wa timu ya Dacico F.c walionekana kutoa shutuma nyingi kwa Mwamuzi kutokana na kitendo chake cha kutowasikiliza mashabiki wakati mchezo ukiendelea kwa kile walichodai kuwa alikuwa akionyesha upendeleo kwa wapinzani wao timu ya Mlimani F.c.
Akizungumzia mchezo huo kocha wa timu ya Dacico fc Moris Chambua alisema kuwa “Kiwango cha Mpira kilichoonyeshwa na Kikosi cha wachezaji wangu ndiyo silaha iliyowafanya wakaibuka na ushindi huo”alisema kocha huyo.
Na  Kwa upande wa kocha wa timu ya Mlimani Professional yeye alisema kuwa” timu yake ilicheza vizuri lakini walizidiwa mbinu chache za kiufundi hali iliyopelekea timu yake kupoteza mchezo huo”alisema Fredrick Emanuel.
Wakati mashabiki wa timu hizo walisema kuwa  “timu ya dacico ilikuwa na uwezo wa kushinda zaidi ya goli moja walilolipata lakini washambuliaji wa timu hiyo hawakuwa makini kwenye suala zima la umaliziaji” alisema Fack A. Fack shabiki wa Dacico F.c,  na kwa upande wa shabiki wa mlimani professional Mohamed hawadh  yeye alisema kuwa “uwanja umechangia wao kutofanya vizui kutokana na uwanja huo kujaa tope” alisema mohamed

Mchezo huo ambao ulianza saa kumi na dakika arobaini jioni kutokana na hali ya hewa ambayo kwa wakati mwingi Mvua za hapa na pale( Rasharasha) zilisababisha kucheleweshwa kwa Mtanange huo ambao hata hivyo pamoja na Mvua Mashabiki waliendelea na shamrashamra zao hadi mwisho wa mchezo.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika katika mpambano huo, timu zote zilikwenda mapumziko mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu kwa kutofungana kutokana na wachezaji wa pande zote mbili kucheza kwa kukamiana wakati wote pamoja na washambuliaji wa pande zote kutokuwa makini wakati wa umaliziaji.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo kwa upande wa timu ya Dacico, kocha wa timu hiyo Moris Chambua aliwatoa Mohamed Abdalah na nafasi yake ikachukuliwa na mchezaji Razack Mushi, alitoka Alafa Julius(a.k.a Mbaba) na nafasi yake kuchukuliwa na Jafet Mantari, alitoka Moody Mohamed na nafasi yake kuchuliwa na Sixmond wakati Mlimani wao waliwaingiza Mrisho Mrisho na Baraka S. Baraka mabadiliko ambayo yalionekana kuipa nguvu timu hiyo. 

Baada ya Makocha wa timu zote mbili kufanya mabadiliko hali ya mchezo ilibadilikia pia kutokana na kuingia wachezaji wenye nguvu ambapo kwenye dakika ya 58, 66, 70 mwamuzi wa mpambano huo, Shaaban Mpalule  ambaye ni Mwalimu katika chuo cha Dar es Salaam City College, alipuliza filimbi mara kwa mara wakati wachezaji wa Timu ya DACICO walipokuwa wakielekea kufunga kuwa Wameotea.

Kipindi cha pili katika dakika 64 hadi 72 timu ya Mlimani Profesional ilionekana kuelemewa zaidi na Wenzao wa DACICO F.c kabla ya dakika 73 hadi 81 ambapo Mlimani baada ya kufanya mabadiliko, ilionekana kupata nguvu na kuanza kulishambulia lango la timu ya Dacico lakini bahati haikuwa upande wao kutokana na Dacico kupata Penalti katika dakika ya 82 ya mchezo na iliweza kuwekwa kimiani na kiungo mchezeshaji Jafeti George, ambaye alifunga kwa Shuti kali lililokwenda moja kwa moja kimiani na kumshinda mlinda mlango wa Mliman Briy B. Briy.

Baada ya mchezo kumalizika mwandaaji wa mpambano  Alexander Ngerezi  alisema kuwa maandalizi ya mchezo yalikwenda vizuri isipokuwa kulikuwa na mapungufu madogo madogo ambayo yalihitaji msaada wa wadhamini ikiwamo masuala ya mipira, jezi, Filimbi, pamoja na Viatu kwa Wachezaji ambao muda mwingi wanatumia kuwa masomoni hivyo kukosa muda wa kufuatilia vifaa vya michezo, katika mpambano wa kwanza pia timu ya Dacico iliibuka na ushindi wa bao 1-0 

katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala cha Dar es Salaam City College(DACICO TANZANIA) uliopo Kibamba Chama jijini Dar es Salaam.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni