Dar es Salaam City College - dacico Tanzania
Na: Happiness Mayebele (DACICO-DAR ES SALAAM)
Chuo
cha uandishi wa habari na Utawala. dar es salaam city College, siku ya
jumamosi tarehe 5 ya mwezi wa saba mwaka huu wa 2014, kinatarajia
kufanya Mahafali ya 13 ya Wahitimu katika Vyuo vya Mbeya, Dar es Salaam
na Sumbawanga, Jumla ya Wahitimu 282
wanatazamia kuwa miongoni mwa wanafunzi watakaokuwa wanamaliza katika
vyuo hivi bora kutoka hapa TANZANIA.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Mtendaji wa Dar es Salaam City College, Bwana Idrisa Mziray, Mgeni Rasmi katika Mahafali
hayo ni Naibu Waziri wa Michezo na Habari, Juma Nkamia,ambaye atawatunuku wahitimu vyeti pamoja na kutoa Risala kwa wahitimu ambao wengi wao wanalenga kuwa waajiriwa muda mfupi baada ya kuwa wamemaliza masomon yao kwenye vyuo hivi vya DACICO.
Aidha kwa Upande wake mkurugenzi wa Chuo kwa Upande wa Dar es Salaam, Mr. Vedasto Malima, Mahafali
hayo yamepangwa kufanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Dar es Salaam City
College(DACICO TANZANIA) ambapo ni makao makuu ya Vyuo vya DACICO TANZANIA yaliyopo jijini Dar es Salaam na yanatazamia kuanza majira
ya saa nne asubuhi.