Jumapili, 29 Juni 2014

SHEREHE ZA MAHAFALI YA 13 YA CHUO CHA DACICO NI JUMAMOSI YA TAREHE 5/7/2014

Dar es Salaam City College - dacico Tanzania 
Na: Happiness Mayebele (DACICO-DAR ES SALAAM) 

Chuo cha uandishi wa habari na Utawala. dar es salaam city College, siku ya jumamosi tarehe 5 ya mwezi wa saba mwaka huu wa 2014, kinatarajia kufanya Mahafali ya 13 ya Wahitimu katika Vyuo vya Mbeya, Dar es Salaam na Sumbawanga, Jumla ya Wahitimu 282 wanatazamia kuwa miongoni mwa wanafunzi watakaokuwa wanamaliza katika vyuo hivi bora kutoka hapa TANZANIA.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Mtendaji wa Dar es Salaam City College, Bwana Idrisa Mziray, Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo ni Naibu Waziri wa Michezo na Habari, Juma Nkamia,ambaye atawatunuku wahitimu vyeti pamoja na kutoa Risala kwa wahitimu ambao wengi wao wanalenga kuwa waajiriwa muda mfupi baada ya kuwa wamemaliza masomon yao kwenye vyuo hivi vya DACICO. 
Aidha kwa Upande wake mkurugenzi wa Chuo kwa Upande wa Dar es Salaam, Mr. Vedasto Malima,  Mahafali hayo yamepangwa kufanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Dar es Salaam City College(DACICO TANZANIA) ambapo ni makao makuu ya Vyuo vya DACICO TANZANIA yaliyopo jijini Dar es Salaam na   yanatazamia kuanza majira ya saa nne asubuhi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni