Alhamisi, 14 Agosti 2014

BONANZA LA DACICO KUMEKUCHA HAPO KESHO

Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala (DACICO TANZANIA) siku ya kesho kutakuwa na Bonanza la Maandalizi ya Tamasha la Vyuo vya Elimu ya Kati Tanzania( NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015), kwa ajili ya Vyuo vilivyopata Usajili wa Serikali yaani NACTE TANZANIA, hivyo michezo hiyo kwa Chuo cha DACICO ni Maandalizi ya kuhakikisha Dacico inaibuka kidedea katika Tamasha hilo Kubwa na la aina yake.
Akizungumzia Maandalizi ya Bonanza hilo Mkurugenzi wa DACICO, Mr. Idrisa Mziray, amesema kuwa, lengo kubwa la DACICO kuweka Bonanza kwa ajili ya kushiriki Michezo katika ya Walimu na Wanafunzi, ni kutaka kupata kikosi cha Timu zitakazoshiriki wakati wa michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika 21-23/11/2014.
"sisi lengo kama unavyofahamu, ni kuhakikisha tutafanya Vizuri wakati wa michezo yetu, maana kumbuka kuwa katika Tamasha hilo la Vyuo vya Elimu ya Kati, ni kwa Mara ya Kwanza, hivyo kila Chuo kitataka kufanya vyema ili kujijengea heshima wakati wa Michuano katika Mwaka Mwingine, lakini Pia kupata zawadi, ikiwa ni pamoja na kujitangaza zaidi, maana sidhani kama Chuo kitakachofanya vibaya kwenye michuano hiyo, kupata sifa nzuri ama kujitangaza zaidi, maana kulingana na Waandaaji wa Tamasha hilo, Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, kwenye michezo hiyo mfumo uliotumika ni Mtowano, hivyo itakuwa ni jambo la kushangaza tutakapotupwa nje katika hatua za Mwanzo za Tamasha hilo, kwa niaba ya Chuo Changu cha DACICO, napenda kuwatangazia wachezaji wote wa DACICO kufika Mara Moja Chuoni kwa ajili ya kukamilisha Maandalizi haya na pia kuvitaka vyuo Vingine kuthibitisha Ushiriki wao Mapema, Wasiogope kuleta timu zao kwa kutuogopa sisi pamoja na kwamba Timu ya Dacico inasifika kwa kutoa Dozi kwa Timu za Vyuo Vingine lakini katika hilo Tamasha la NACTE, lolote laweza kutokea kutokana na Timu za Vyuo vyote hivi sasa kuwa kwenye Maandalizi Makali, kikubwa tu ni kuwasisitiza Wanamichezo wa Vyuo Vingine kuhakikisha kwamba wachezaji, Wanafunzi, na Mashabiki wao wanakuwa Watulivu wakati wote wa Mashindano" amesema Mziray
Bonanza hilo hapo kesho linatazamiwa kuanza mapema majira ya saa mbili asubuhi ambapo kocha wa timu ya Dacico Walimu Sir- Henry amejigamba kuibuka na ushindi mnono dhidi ya timu ya wanafunzi, lakini wakati huo huo akiwataka Wachezaji wa Timu ya Wanafunzi, kucheza Mchezo wa Utulivu ili kuhepuka kuwaumiza walimu ambao kwa Muda Mwingi wamefanya Maandalizi yao kwenye Vitabu kutokana na kuwa na Majukumu Mengi ya Ufundishaji wa Masomo kwa Wanafunzi.

MPAKA MUDA HUU KIKOSI CHA TIMU YA WANAFUNZI BADO KIMEFICHWA LAKIMNI KIKOSI CHA TIMU YA WALIMU TAYARI KIMEBAINISHWA, NA WALIMU WAMEJIGAMBA KUWAFUNGA TIMU INAYOUNDWA NA WANAFUNZI.

NA HIKI NDICHO KIKOSI KAMILI CHA TIMU YA WALIMU WA DACICO.
1, Idrisa Mziray
2, Sir- Masawe
3, Sir Malima
4, Sir Mpalule
5, Sir Mpoto
6, Mr. Ombeni
7, Sir Kelvini
8, Mr. Sam
9, Sir Michael Jackison
10, Sir Michael Jeremia
11, Sir Kasilima
Wachezaji wa Akiba ni
Mr. Cholo
Sir. Kisima
Sir. Kazimoto
Kocha Mkuu HENRY
Hawa ni Baadhi ya Washiriki wa Michezo mbali mbali kwa Upande wa Timu za Wanawake wa Chuo cha DACICO.

Na kwa Upande wa Timu ya Wanawake watakaoshiriki katika mchezo wa Netball ni Pamoja na Wachezaji
1. Doris Mchome,
2. Alice
3. Lucy
4. Veronica
5. Mwanahawa
6. Monica
  www.missdemocrasiatz.com
7.Violet
8. Laura Solima
9. Felister
10. Pepetua Luguga
11. Neema
12. Anthonia
13. Farida
14, Kalister
15, Victoria Godwin
======================================================
Baada ya michezo ya Timu za wenyewe kwa wenyewe DACICO Walimu na DACICO Wanafunzi, utafuata mpambano wa Timu ya K.E.C ya Shirika la Elimu Kibaha(Njuweni).
unaweza pia kufuatilia michezo ya Bonanza hilo la Maandalizi ya Tamasha la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015.
Wanafunzi Wote wa DACICO mnakaribishwa sana.
kwa habari zaidi bofya hapa. www.daressalaamcitycollege.blogspot.com
www.missdemokrasia.blogspot.com

Jumatatu, 4 Agosti 2014

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha DACICO TANZANIA, wakifuatilia Kozi work zao kwa Mwalimu Michael Jackison, wakati huu wa maandalizi ya Mitihani

 
Mwalimu Michael Jackison(kushoto) akifafanua jambo kwa wanafunzi wa masomo ya Uandishi wa Habari, Makao Makuu ya Chuo Jijini Dar es Salaam.(Picha Zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).

WANAFUNZI WA INTAKE JANUARY, APRIL, NA SEPTEMBER- DACICO WAANZA MITIHANI

 

























 
Kati ya wanafunzi hawa wengine wanamaliza masomo yao lakini pia wengine wanafanya  mitihani ya kufunga muhula wa kwanza, mitihani hii ni kwa ajili ya wanafunzi wa Vyuo vyote vya DACICO TANZANIA.