Alhamisi, 12 Desemba 2013

Baadhi ya Wanafunzi wa Dacico wakiwa kwenye Mafunzo ya Kazi ya Upigaji Picha za Television

Wanafunzi wa Dar es Salaam City College, wanaosoma kozi za Uandishi wa Habari na Utangazaji wakiwa kwenye Moja ya Mafunzo ya Kurekodi Matukio ya Television makao makuu ya Chuo Kibamba Jijini Dar es Salaam.(Picha Zote na Aurea Simtoe & Dina Chuwa).

KONGAMANO LA VIJANA LA KUJITAMBUA KUHUSU BILA KUFANYA DHAMBI ST. ANNE MARIE JIJINI DAR ES SALAAM

 Kikundi cha Obrigado wanafunzi wa St. Joseph wakitumbuiza katika kongamano hilo.
 Mmoja wa waumini wa Dhehebu la Kikiristo akitoa neno la Mungu.
Waumini wakipata Mkate kama ishara ya kumkumbuka bwana Yesu
Baadhi ya Wanafunzi wa vyuo  wakitumbuiza
 Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa katika kongamano hilo.
 Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa katika kongamano hilo.
Rais wa Serikali ya wanafunzi katika chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala, DAR ES SALAAM CITY COLLEGE, Mathias Canall wa pili kushoto, akiwa na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Mlimani Profesional.(Picha Zote na Aurea Simtowe).

Jumanne, 26 Novemba 2013

SERIKALI YA WANAFUNZI WA DACICOSTUA 2013 WAKIAPISHWA

WAZIRI WA ELIMU JACKSON  YOHANA MOLELI
KATIBU MKUU-ROZINA MCHOMVU
NAIBU WAZIRI WA KATIBA, SHERIA, ULINZI NA USALAMA-SAULO SANASIO
WAZIRI MKUU-GOODLUCK MOSES KAJUNA
WAZIRI WA AFYA NA MAZINGIRA-RAZACK MUSHI
WAZIRI WA HABARI, MAMBO YA NDANI NA NJE-DIGNER CHUWA
WAZIRI WA KATIBA, SHERIA, ULINZI  NA USALAMA- CHRISTOPHER LYOGELO
WAZIRI WA MICHEZO, STAREHE NA MAAFA-ALEXZANDER NGELEZI

Jumatatu, 25 Novemba 2013

DACICO VS GLOBAL- ZATAMBIANA TEGETA

 Baadhi ya Wachezaji wa DACICO FC, wakiwa kwenye maandalizi ya mchezo huo
  Baadhi ya Wachezaji wa GLOBAL  FC, wakiwa kwenye maandalizi ya mchezo huo
 KIKOSI CHA GLOBAL FC
 KIKOSI CHA DACICO FC
 Wachezaji wa Timu wa DACICO  Vs GLOBAL, wakichuana Vikali katika mpambano huo.
 Baadhi ya Mashabiki wa DACICO wakifuatilia kwa makini mpambano
 Nyota wa DACICO, Said(mbele) akimtoka kiungo mchezeshaji wa GLOBAL, Moland, wakati wa mpambano
 Beki nyota wa timu ya DACICO FC, Mathias Canal, akijaribu kuondoa hatari zote kwenye lango la DACICO.
 Baadhi ya Mashabiki wa Timu ya Global Publishers, wakifuatilia kwa makini mpambano huo.
==================================================
Na: Wanafunzi DACICO.

imu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala, Dar es Salaam City College(DACICO TANZANIA, mwishoni mwa juma ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Global Publishers, katika Uwana wa Shule ya Sekondari Tegeta.
Katika Mchezo huo ambao Global ilionekana kuzidiwa kwa kiwango kikubwa, hadi timu zote zinakwenda mapumziko matokeo ilikuwa 0-0 kabla ya timu Zote kufanya mabadiliko ya Hapa na pale, ambapo Global ilibidi kuwatumia wachezaji wa kukodi(Mamruki) na kuweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Akizungumzia mchezo huo, kocha wa timu ya DACICO FC, Ombeni, alisema kuwa kikosi chake pamoja na kupoteza mchezo huo ilitokana na wachezaji wengi kucheza bila mazoezi kutokana na kwamba muda mwingi waliutumia katika masomo kwani walikuwa katika maandalizi ya mitihani.
"tumefungwa na Global kwa mengi moja ni pamoja na kukosa mazoezi wachezaji wangu kutokana na kuwa kwenye maandalizi ya mitihani, pia wenzetu wa Global wametumia wachezaji Mamruki ambao siyo waajiliwa wao kama tulivyotarajia wangecheza wenyewe, wametuchezeshea wachezaji wa ligi sijui wamewachukua timu gani hawa maana wana kasi na mbio sana, lakini goli hilo moja tutarejesha wakati wa mchezo wa marudiano"alisema ombeni
mchezo mwingine wa marudiano unatarajia kuchezwa mwishoni mwa mwezi wa kumi na mbili.

Jumamosi, 16 Novemba 2013

BENDERA YA DACICO YAPANDISHWA RASMI MAKAO MAKUU YA CHUO DAR ES SALAAM.

Hii ndiyo Bendera ya Dar es Salaam City College  DACICO TANZANIA.
 Mkurugenzi Mkuu wa DACICO, Idrisa Mziray, Baada ya kukabidhi majukumu ya Bendera ya Chuo na ya Tanzania, ambazo zimepandishwa Rasmi Makao Makuu ya DACICO jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa Wafanyakazi wa DACICO-TANZANIA. Mpalule Shaaban, akipandisha Bendera ya Chuo Rasmi.
 Bendera ya DACICO ikiwa imepandishwa Tayari.

 Mkurugenzi Mkuu wa DACICO-TANZANIA, Bwana, Idrisa Mziray, muda mfupi baada ya Bendera ya DACICO Kupandishwa.
Majengo ya Chuo yakiwa katika Mwonekano wa Pekee baada ya Kupandishwa Bendera ya Chuo.(Picha Zote kwa Hissan ya Miss Demokrasia Tanzania).

Jumatano, 6 Novemba 2013

WANAFUNZI DACICO WAENDELEA NA MITIHANI KATIKA CUMPUS YA DAR, MBEYA NA SUMBAWANGA.

Baadhi ya Wanafunzi wa DACICO, Wakiwa katika Vyumba vya Mitihani Leo tarehe 6/11/2013, Cumpus ya Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanafunzi wa DACICO, Cumpus ya Dar es Salaam, Muda mfupi kabla ya kuanza mitihani, wakisimama kwa ajili ya kupata Maombi.(Picha Zote kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).