Mwamuzi wa Mchezo huo Shaaban Mpalule, akionekana kuwaita baadhi ya wachezaji wa Timu zote kutokana na kuonyesha mchezo mbaya.(Picha na Mathias Haule).
Baadhi ya Wanafunzi na Mashabiki wa Certificate, wakifuatilia kwa makini Mpambano huo
Wachezaji wa Timu ya Certificate, wakielekeza mashambulizi katika lango la timu ya Diploma.
Mashabiki wa timu hizo wakimzonga Mwamuzi baada ya kutaka kumlazimisha baadhi ya maamuzi wakati wa kupuliza filimbi, kitendoo kilichosababisha mpira kusimama kwa muda.
Mchezaji Nyota wa Timu ya Certificate, Deogratius, akiambaa na mpira kuelekea katika lango la timu ya Diploma
Mwamuzi wa Mpambano huo Shaaban Mpalule, akionyesha kati baada ya timu ya Certificate kusawazisha bao, ambalo hata hivyo lilitaka kuleta mzozo kutokana na wachezaji wa timu ya Diploma kugomea bao hilo ambalo liliunganishwa kwa mkwaju mkali baada ya kumshinda mlinda mlango wa timu ya Diploma.
Baadhi ya Matukio ya picha wakati wa mchezo huo(Picha zote na Mathias Haule).
======================================================
DIPLOMA Vs CERTIFICATE ZASHINDWA KUTAMBIANA.
Na: Mariam Mwakatumbula
Timu ya Soka ya DACICO Diploma dhidi ya timu ya Certificate jana zimeshindwa kufungana baada yab kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 katika mchezo wa marudiano uliofanyika katika Uwanja wa Kibwegele nje kidogo ya mji wa Kibamba Chama.
Wakicheza mbele ya Mkurugenzi mkuu wa Chuo bwana Idrisa Mziray, wachezaji wa timu zote walionekana kucheza kwa kukamiana kutokana na kila mmoja kutaka kuchaguliwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ambayo inatarajia kumenyana na timu za vyombo vya habari zikiwemo timu za Taswa F.c.
aidha katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa chuo cha DACICO uliopo kibamba CCM timu hizo zilishindwa kutambiana baada kumaliza dakika 90 kwa kufungana 2-2 na hivyo kuomba mchezo wa marudiano ambao pia timu hizo zimeshindwa kupata mbabe na kulazimisha kutafutwa mchezo mwingine ili iweze kujulikana ni timu ipi yenye ubavu itakayowezakuibuka na ushindi.
wakizungumza baada ya mpambano huo makocha wa timu zote mbili, Mwalimu Kashilima wa Diploma na Mwalimu wa Michezo wa Timu ya Certificate Ombeni wamesema kuwa kushindwa kupata timu iliyoibuka na ushindi kumetokana na wachezaji kucheza kwa kukamiana na hivyo kusababisha mchezo huo kutawaliwa na vurugu zilizosababisha mwamuzi kushindwa kuumudu vyema mchezo huo kutokana na kila mara wachezaji kwenda kwa mwamuzi na kumzongazonga.
"Wachezaji wangu wamecheza mpira mgumu sana leo na hiyo imetokana na kukamia mpambano, unajua timu hizi ni pinzani pamoja na kwamba wanasoma katika chuo kimoja, kikubwa hapa ni kwamba wachezaji wa Diploma wanawaona hawa wa Certificate kama watoto wadogo, lakini kumbe mpira ama mchezo wowote hauna kuzarau, kwani hawa vijana wangu wa Certificate wanacheza mchezo mzuri na wa hali ya juu ila kwa leo naweza kusema wamecheza mchezo wan kuwaiga hawa wachezaji wa timu ya Diploma, ila tunaomba mchezo wa tatu ambao bila shaka utamaliza ubishi wote na hapo tutapata kufahamu ni timu ipi bora ukilinganisha na ingine" alisema mwalimu wa michezo katika chuo cha Uandishi wa habari na Utawala DACICO.
wakati huo huo kocha wa Diploma mwalimu kasilima amewalaumu wachezaji wa timu yake kwa kushindwa kulinda goli ambalo lilifungwa mapema kwenye dakika za mwanzo kabla ya kwenda mapumziko baada ya mchezaji nyota wa timu hiyo Hilary Mgenzi kuwalamba chenga walinzi wa timu ya Certificate na kisha kufunga kwa Shutin kali lililokwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha mlinda mlango wa Certificate othman juma akiutazama kwa macho.
"sikutarajia kama mchezo huu ungekuwa mgumu kiasi hiki, maana hii ni mara ya pili tunashindwa kuibuka na ushindi pamoja na kwamba sisi ndiyo tunaanza kuwafunga hawa wenzetu wa Certificate, nilijaribu kuwapa maelekezo kuhusu kucheza kwa makini lakini kutokana na kukamia mchezo wachezaji wangu wameshindwa kufuata maelekezo yangu na hivyo kupelekea kusawazisha kwa hawa wachezaji wa Certificate, lakini tunazungumza na Mkurugenzi wetu ili aweze kudhamini mpambano mwingine utakaotoa matokeo ya timu ipi ni bora zaidi ya mwingine, mchezo ambao utakuwa ni wa mwisho kwa ajili ya kupata kikosi cha timu ya DACICO F.C. alisema Kasilima.
kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa chuo bwana Idrisa Mziray, mchezo wa marudiano umepangwa kufanyika mapema baada ya wanafunzi kumaliza mitihani ambayo inatarajia kuanza jumatatu ya kwanza ya mwezi huu.