Jumapili, 28 Julai 2013

HARAKATI NA UANAHARAKATI WA MAANDALIZI YA MAHAFALI YA 12 YA CHUO CHA DAR ES SALAAM CITY COLLEGE(DACICO) 2013.

Zote katika Zote picha Unazoziona ni Harakati ya Siku ya Mahafali, Ambayo kwa Hakika Yamefana kwa asilimia Mia moja  100%, maana kila jambo limetekelezwa na kuungwa kwa juhudi zote kama ilivyo sera ya Chuo na Utawala wa Chuo. Endelea kubofya kila wakati hapa, Tukio bado linaendelea hadi uone Mwisho wake, Mungu ibariki Dar es Salaam City College, Kiwe Chuo Bora zaidi cha Taaluma ya Uandishi wa Habari na Utawala ifikapo mwaka 2015 kiwe ni moja ya miimili ya Taaluma hii. 

 Baadhi ya Wanafunzi wakiwa katika Kuandaa Hafla hiyo ya Mahafali ya 12 ya Chuo cha Dar es Salaam City College 2013
 Wahitimu wakisubiri muda wa kwenda Ukumbini
 Kwa ajili ya kupata Chakula ilitumika nguvu ya Ziada, Babu Mkomavu kama anavyojulikana, akiendelea na matayarisho
 mmoja wa wahitimu wa Mahafali hayo, akiwasili katika eneo la Tukio baada ya kukamilisha maandalizi yake
 Wadau wa Vyombo vya habari kutoka sehemu mbalimbali wakiwa katika Mitego kupata Vipande vya habari wakati wa maandalizi ya mahafali hayo
 Mmoja wa wahitimu akijaribu kuwasiliana na wenzake kufika ili aweze kuvalishwa maua.
 Mmoja wawahitimu akiwasiliana na ndugu, rafiki na jamaa "shoga usisahau kuniletea zawadi" mapema kabla ya mahafali kuanza katika ukumbi wa Temboni Kibamba CCM.
 Mmoja wa Wahitimu akitafuta bila mafanikio kupata mawasiliano "ivi hawa wenye mtandao huu leo vip mbona siwaelewi" ni wakati wa maandalizi ya mahafali hayo.
 aikujulikana kama huyu pia ni Mwanafunzi au mmoja wa ndugu wa wanafunzi waliofika kutuza ndugu zao, isipokuwa alioekana muda mwingi akikatiza maeneo ya mahafali
 Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo cha DACICO, ambaye yupo mwaka wa kwanza, Tegemeo la Chuo kutokana na Umaili wake katika Miondoko ya Urembo na pia ni mwenye kipaji cha Utangazaji na M.C.
 Mmoja wa wahitimu akiwa katika harakati, pembeni yake ni ndugu wadodgo zake waliofika kwa lengo la kumtuza.
 Mmoja wa walimu Tegemeo wa Chuo, Maadam Rehema, ambaye kwa namna kubwa alikuwa ni mmoja wa wafanikishaji wakuu wa maandalizi ya Mahafali ya 12 ya Chuo cha DACICO 2013.
 Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo cha DACICO,  Tegemeo la Chuo kutokana na Umaili wake katika Miondoko ya Urembo na pia ni mwenye kipaji cha Utangazaji na M.C.
Walimu wa Chuo wakiwa katika harakati za Maandalizi ya Mahafali ya 12 ya chuo cha DACICO-TANZANIA, Endelea kufuatilia tukio la Mahafali ya 12 ya DACICO.
(Picha Zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni