Jumamosi, 13 Septemba 2014

DACICO FC , FDC NGUVU SAWA KIBAHA

NACTE INTER COLLEGE TANZANIA-2014/2015- DAR ES SALAAM- YAPAMBA MOTO 

DACICO Qween kushusha kikosi cha Maangamizi

Na: Violet John (Kihaba).

Timu ya chuo cha Uandishi wa habari wa habari na utawala Dar es salaam city college (DACICO mwishoni mwa juma ili siku ya ijumaa Septemba 12, ilishindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya FDC ya Tumbi Kibaha Pwani , baada ya kumaliza muda wa dakika 90 kwa mabao 2-2 mchezo uliochezwa katika viwanja vya Hospitali ya Tumbi wilayani Kihaba mkoa Pwani.
Mchezo huo kwa upande wa kikosi cha DACICO ni maandalizi ya kushiriki kwenye Bonanza la Vyuo vya Elimu ya kati kwa Kanda Dar es Salaam na Pwani, NACTE INTER COLLEGE BONANZA 2014/2015, Bonanza ambalo linashirikisha vyuo mbali mbali ambavyo vimepata usajili wa serikali na kuwa chini ya NACTE TANZANIA linalotarajia kufanyika kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Viwanja vya Shule ya Kibaha Pwani.
FDC iliutumia mchezo huo kama mandalizi ya ligi ya Diwani inayotarajia kutimua vumbi ivi karibuni katika viwanja vya shule ya Sekondari Kibaha, ambapo iliwachukua dakika tano tu ya kipindi cha kwanza kujihakikishia bao mla kuongoza kupitia kwa kiungo mchezeshaji Deus Denes, aliyekuwa amevalia jezi namba saba mgongoni kuweza kuwainua mashabiki wao waliokuwa wamefurika katika uwanja wao wa nyumbani.
Hali ilizidi kuwa mbaya kwa upande wa timu ya Chuo cha DACICO pale ilipojikuta ikipigwa Sindano mbili za haraka haraka, Moja ikiwa ya kutuliza na kuweka Misuli joto na Ingine ya kupunguza Uchovu kwa timu ya DACICO iliyokuwa imewasili muda mfupi ikitokea Makao Makuu ya Chuo yaliyopo Kibamba CCM jijini Dar Es Salaam, kutoka kwa washika Sindano hao wa HOSPITALI ya Tumbi, baada ya Timoth matshala mchezaji wa FDC aliyekuwa amevalia jezi namba kumi mgongoni kupachika bao kunako dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza.
Dacico Fc ambao kwa hakika imepania kufanya vizuri katika Bonanza la Vyuo shiriki la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015, ilikuja juu baada ya kutandikwa dripu hizo mbili, na kuanza kufanya mashambulizi ya nguvu kwenye lango la FDC iliyokuwa imebweteka baada ya kupata mabao hayo mawili, hivyo Dacico iliutumia nafasi hiyo kunako dakika ya 30 mchezaji wa kutumainiwa wa Dacico mshambuliaji nyota ambaye anamudu pia katika nafasi ya kiungo, Moody Mapanki AKA Ronaldo, aliweza kuwainua juu mashabiki wa DACICO baada ya kufunga bao kwa ufundi wa hali ya juu pale mpira ulipompita mlinda mlango wa FDC Henry John dakika ya 30 baada ya kufunga bao linguine kwa dacico katika dakika ya 10 likiwa ni bao la kusawazisha na kuamusha vifijo na nderemo za mashabiki wa Dacico waliokuwa kwa muda wote kimya kutokana na kichapo cha mabao mawili ya haraka haraka katika kipindi hicho cha kwanza.
Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko zilitoshana nguvu ya mabao 2-2, ambapo kipindi cha pili pamoja na timu zote kufanya mabadiliko, hali hiyo haikuleta matunda kwa timu zote mbili hadi mwisho wa mchezo timu hizo ziligawana pointi moja moja.
Akizungumza baada ya mchezo kumalizika, mlinda mlango wa timu ya FDC Henry John, alisema kuwa awali walibweteka kutokana na kuusoma mchezo huo vibaya “ Matokeo ya mchezo huu kweli umekuwa ni tofauti kabisa na matarajio yetu, mchezo umekuwa mgumu sana, maana tulivyotarajia sivyo walivyokuja hawa wenzetu wa dacico, mwanzo tulidhani kuwa tumeshawamudu na tulikuwa tunacheza vizuri tu lakini kama unavyofahamu mpira ni mchezo wa makosa, kwa hiyo unapoteleza kidogo ndipo mpinzani anapochukua hatua kwa haraka na ndivyo ilivyotokea kwa hawa DACICO, mwanzo tulidhani hawatakuwa na mazoezi kinyume na matarajio yetu, lakini kwa kuwa wapo katika maandalizi ya Bonanza la vyuo vya Elimu ya Kati NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, basi wajiibidishe tu mazoezi lakini timu yao ni nzuri na wanaweza kufanya vizuri katika bonanza hilo” alisema mlinda mlango huyo wa FDC Henry John.
Mpambano mwingine baina ya timu hizo unatarajiwa kufanyika baada ya mwezi mmoja kabla ya tarehe ya mashindano ya vyuo vya elimu ya kati ambapo wachezaji na makocha wa timu zote mbili wametambiana kuibuka na ushindi kila mmoja, katika mchezo wa mwisho uliofanyika ivi karibuni kabla ya mchezo wa juzi timu ya Dacico ilikuwa ikishikilia rekodi ya kuifunga timu hiyo katika uwanja wao kwa jumla ya bao 1-0.Dacico iliwatumia zaidi wachezaji wapya ambao ndiyo kwanza wameingia kuanza masomo lakini hata hivyo Bado kocha mkuu wa Dacico anayo kazi ya kupata kikosi cha kwanza kutokana na wachezaji wote kuwa katika hali nzuri ya mchezo.
Naye kocha wa timu ya Dacico Mwalimu Kelvin alisema maandalizi ya kushiriki Bonanza la NACTE kwa upande wao wanaendelea vizuri na ndiyo wapo kwenye ratiba ya kucheza michezo mingi ya kirafiki “Sisi tupo kwenye maandalizi ya kushiriki Tamasha la Michezo la Vyuo vya Elimu ya Kati, linalotarajiwa Mungu akipenda kufanya mwezi wa kumi na moja tarehe za 21 huko, wachezaji wangu wengi wazoefu kwa muda huu wapo likizo, hapa wamekuja wengi wapya, na safari hii wamejitokeza wanafunzi wengi DACICO wanamichezo hata mimi mwenyewe nashindwa nitaipanga vipi hii timu, na ndiyo maana tumeanza kufungwa dakika za mwanzo kutokana na kutojuana kwa wachezaji wangu, hawaja kaa na kucheza pamoja, ndiyo kwanza wanaanza kuzoeana, lakini hata hivyo kutokana na uzoefu nilionao, nimeweza kubaini makosa kwa haraka na kufanya marekebisho na ndiyo maana tukasawazisha magoli hayo kwenye hicho hicho kipindi walichotufunga hawa wenzetu wa EDC, maana hata hii timu siyo ya kubeza, ni timu imara imeonyesha uwezo mkubwa sana, wachezaji wangu ni vijana nilitegemea wangewatoa udenda hawa vibabu wa fdc lamkini kumbe nao wamekamilika, wameutumia vizuri uwanja wao na sisi mwishoni mwa mwezi au kabla ya Bonanza la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015, tutapanga mchezo mwingine wa mwisho na hawa hawa maana wamenipa changamoto nzuri,wiki hii jumamosi tunatarajia kucheza na timu ya majirani zetu Timu ya Veterani ya Kibamba Hospitali kwenye Uwanja wa Kibamba Hospitali siku ya ijumaa, michezo hii kwetu ni maandalizi tunahitaji kuwa fiti kwa timu zote za wanawake na wanaume, isipokuwa nichukue fulsa hii kuvihamasisha vyuo vingine pia kufanya maandalizi Mapema” alisema Kelvin
Mwisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni