Jumatatu, 20 Januari 2014

SCHOOL BUSH DACICO & MLIMANI - DACICO YAITAMBIA MLIMANI KATIKA SOKA

Wachezaji wa Timu za Dacico Fc, kiungo Machejo Dula (nyekundu) na mlinzi wa timu ya Mlimani Profesional Fc. Masanga Mkama wakiwania mpira wakati wa mchezo wa kirafiki katika hafla ya Sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Dar es Salaam City College na Mlimani Profesional(School Bush) iliyofanyika kwenye Viwanja vya Kibamba Chama, jijini Dar es Salaam Jana. hadi mwisho wa mchezo Dacico iliibuka na ushindi wa bao  1-0 (Picha kwa Hissan ya Miss Demokrasia Tanzania).
Mchezaji wa Timu za Dacico Pooltable, Yohana Mathius, akijaribu kulenga shimo wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya  Mlimani Profesional Pooltable  katika hafla ya Sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Dar es Salaam City College na Mlimani Profesional(School Bush) iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Dar es Salaam City College Kibamba  jijini Dar es Salaam Jana.(Picha kwa Hissan ya Miss Demokrasia Tanzania).
Walimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala Dar es Salaam City College, Mwl. Kasilima Kasilima na Mwl. Grayson Mgoi wakishindana kucheza na kuimba wakati wa Hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Vyuo vya DACICO na Mlimani Profesional, iliyofanyika Makao makuu ya Chuo cha DACICO kibamba Chama jana na kushirikisha michezo mbali mbali ikiwamo Soka, Pooltable, kuimba, kucheza muziki, kuogelea, Urembo Mr. & Miss New Intake DACICO na mashindano ya kujibu Mada(Debate)(Picha kwa Hissan ya Miss Demokrasia Tanzania).
 Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala Dar es Salaam City College, wakati wa wakati wa kutafuta washindi wa Urembo Miss & Mr. Dacico kwenye  Hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Vyuo vya DACICO na Mlimani Profesional, iliyofanyika Makao makuu ya Chuo cha DACICO kibamba Chama jana na kushirikisha michezo mbali mbali ikiwamo Soka, Pooltable, kuimba, kucheza muziki, kuogelea, Urembo Mr. & Miss New Intake DACICO na mashindano ya kujibu Mada(Debate)(Picha kwa Hissan ya Miss Demokrasia Tanzania).
wanafunzi na Mashabiki na mashabiki wa Dacico f.c wakishangilia baada ya timu yao kuifunga timu ya Mlimani Profesional katika mchezo wa kirafiki uliyofanyika kwenye Viwanja vya kibamba chama dar es salaam jana.(Picha kwa hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).

Kikosi cha DACICO F.C.
Wanafunzi wapya wa Vyuo vya Uandishi wa Habari jana wamekaribishwa kwa sherehe na shamrashamrav mbalimbali kutoka Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala Dar es Salaam City Collge(DACICOSTUA) kwa kushirikiana na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mlimani Profesional vyote vya jijini Dar es Salaam, ambao waliandaa michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba, mashindano ya Urembo, kutunisha Misuli, kuimba, kucheza, kujibu mada, kuogelea, netball, volleyball katika hafla iliyofanyika makao makuu ya chuo cha Dacico kibamba chama.

Akizungumza katika hafla hiyo mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala, Dacico, Bw. Idrisa Mziray, alisema kuwa lengo la sherehe hizo ni kuwakaribisha wanafunzi wanaoanza mafunzo kwenye Vyuo hivyo new Intake, ambao baada ya kuwasili kila muhula ufanyiwa ukaribisho na serikali za vyuo hivyo kwa lengo la kutakiana baraka na pia kufanya utambulisho wa viongozi kwa wanafunzi wageni ili kuweza kuendana na utaratibu unaokuwa umewekwa na bodi ya chuo kwa kuwashirikisha wanafunzi ambao ni viongozi wa serikali yao.

Aidha katika Hafla hiyo mapema wanafunzi wa chuo cha Dacico kilichuana na Mlimani Profesional katika michezo mbalimbali lakini hata hivyo wachezaji wengi wa Mlimani Profesional walifanikiwa kuibuka washindi kwenye michezo ya Pooltabl, kuvuta Kamba kabla ya kubwagwa kwenye mchezo wa Soka kwa kukubali kufungwa bao 1-0  ambalo lilifungwa na mchezaji Mathias Haule kwa shti kali mchezo ambao ulifanyika kwenye uwanja wa Kibamba Chama.

baada ya mchezo huo hafla hiyo ilikwenda moja kwa moja ukumbini na kuwakutanisha tena katika  michezo ya pooltabe ambapo wachezaji wa Dacico walionekana kukabwa koo kutokana na wachezaji wa mlimani profesional kuonyesha kiwango kizuri katika kulenga na kutumbukiza mipira ukilinganisha na wenzao wa Dacico pooltable lakini hata hivyo hadi mwisho wa mchezo timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana michezo miwili miwili lakini Yohana Dula wa Dacico akiibuka nyota wa mchezo huo kutokana na kushangiliwa sana na mashabiki waliokuwa wamefurika kushuhudia michezo hiyo.

Kivutio kikubwa katika hafla hiyo ilikuwa ni mashindano ya Urembo ambayo yalishirikisha jinsia zote na hivyo kuonekana kuwa kivutio kikubwa kwa wote waliokuwa wakifuatilia shamrashamra hizo na hivyo kufanya vifijo na ndelemo kutawala muda wote ususani alipokuwa akikatiza mshindi  Ikumbo Gradman ambaye aliwabwaga wenzake kutokana na kuwa kivutio kikubwa kwenye mashindano hayo akifuatiwa na Fatuma Said, wakati kwa  upande wa wanaume kivutio kikubwa ilikuwa ni kwa haji juma maarufu kama kaseja kutokana na umahili wake wa kudaka mipira, wakati shindano la Miss Bantu lilikosa msisimuko kutokana na washiriki Cecilia Kimaro, Saumu Ramadhan, Rabia Salum, shamim Juma kushindwa kutokea Uwanjani.

Washindi wengine katika Michezo hiyo ilikuwa ni pamoja na Kasilima na Grayson Mgoi walitoshana nguvu baada ya wote kupata kura sawa kutoka kwa mashabiki waliokuwa wamejaa ukumbi wa Chuo cha Dar es Salaam City College, katika mchezo wa kuimba na kucheza, Happy Mayala kuogelea kwa upande wa Wanawake huku nafasi ya pili ikienda kwa Mariam Mwakatumbula na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Vanessa hata hivyo fainal hiyo ilishindwa kuwa na msisimko kutokana na kiza kuingia na hivyo washiriki wengine waliokuwa wamejiandikisha kushiriki kushindwa kutokana na muda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni