Alhamisi, 27 Novemba 2014

DACICO KUUNGURUMA NA KUTOA KIPIGO BONANZA LA USITAWI WA JAMII SEASO TWO

NACTE INTER COLLEGE TANZANIA  2014/2015 - SEASON  TWO
VYUO NANE UWANJA WA USTAWI WA JAMII KIJITONYAMA .
Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Entertainment C.o Ltd kwa kushirikiana na kituo bora cha Matangazo TIMES FM 100.5 kwa pamoja wanakuletea bonanza la vyuo SEASON TWO itakayofantika katika viwanja vya ustawi wa jamii kijitonyama siku ya jumamosi wiki hii tarehe 29/11/2014.
Vyuo mbalimbali vya NACTE mkoa wa dar es salaam, vinatarajia kuchuana katika bonanza la hilo litakalokuwa na michezo ya soka, Basketball, Voleyball na netball, ikiwa ni sehemu ya pili ya mchujo wa kutafuta timu zitakazoshiriki ligi ya NACTE Tanzania katika msimu wa 2014/2015,baada ya sehemu ya kwanza kumalizika kwenye chuo cha DIT Mwishoni mwa juma na kuhusisha vyuo mbali mbali vya Dar es salaam.
Sehemu ya pili ambayo imepangwa kufanyika katika uwanja wa ustawi wa jamii kijitonyama jumamosi ya tarehe 29 mwezi huu inatarajia kuwa ya kusisimua kutokana na Michuano hii ya Mtoano kuwa kivutio kwa Wachezaji na Mashabiki ambao wengi wao ni wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali wanaofika kushuhudia michuano hiyo inayoendeshwa kwa ubunifu wa hali ya juu.
 Timu zinazochuana juma hili ni pamoja na Institute of Adult Education, Institute of Social Work (ISW) - DSM, Lugalo Military Medical School - Dsm, St. Joseph  College (University),  Dar es salaam City College (DACICO, Dar-es-Salaam School of Journalism (DSJ) - DSM, National Institute of Transport (NIT) - DSM, Bandari College - DSM,huku timu mwalikwa ikiwa ni Timu ya wafanyakazi wa PPF Dsm.

Timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya pili wiki iliyopita kwa upande wa soka ni Chuo cha IFM waliofanikiwa kuwafunga DIT katika fainali kwa njia ya penalt baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 bika kufungana, kabla ya kutinga hatua hiyo ya fainali kikosi cha IFM kilifanikiwa kuwafunga CBE katika mchezo wa kwanza kwa 2-1 wafungaji wa magoli wakiwa ni Godlisten Kessy aliyepachika mabao yote mawili dakika ya 15 kipindi cha kwanza na dakika 51 kipindi cha pili huku bao la CBE likiwekwa wavuni na Mwendo Sitena mchezo uliochezeshwa na mwamuzi Mussa Charles.
Wakati DIT wakafanikwa kutinga fainali baada ya kuwafunga Muhimbili kwa bao 1-0, TRA ikaambulia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Times, wakati Voleyball  wanaume CBE  waliibuka kidedea dhidi ya wenyeji DIT, huku David Davic akiibuka (Best Spiker), Dickison Benjamini wa DTI, aliibuka (Best Broker), Gideon Joseph wa IFM aliibuka (Best Recever), Joseph Mafuru wa CBE aliibuka (Best Seter), Daniel Msambusi wa DIT aliibuka (Best Rebelo), na MVP katika ufunguzi huo akiwa ni nyota wa CBE Samweli Kitime.
Kwa upande wa mpira wa mikono netball pia IFM ilijidhiilisha kuwa kijoo cha mjini baada ya kufuata nyayo za kaka zao kwa kuwafunga chuo cha DIT kwa 19 dhidi ya 14 huku wafungaji katika mchezo huo wakiwa ni Sarah Shaaban aliyefunga magoli 12(GS) na Teckila teas akifunga 7 (GA) katika mchezo wa Fainali pia uliofanyika kwenye viwanja vya DIT.
CBE  pia ilimg’ara katika mchezo wa Kikapu (Basketball) kwa upande wa wanaume baada ya kuwafunga DIT katika mchezo wa Fainali kwa vikapu 51-37 ambapo wahezaji waliong’ara ni Sarehe Ramadhani, Evance David, Edger Mwakase  huku kwa DIT waking’ara wachezaji Evance Kamola na Charles Poul.
Michuano hiyo ya  NACTE INTER COLLEGE TANZANIA imeanza siku ya jumamosi tarehe 22/11/2014 ikiwa  ni  ufunguzi  ambapo vyuo vilivyohusika katika ufunguzi huo ni pamoja na IFM, DIT, TRA, MUHIMBILI, CBE, ROYAL, MLIMANI Profesianal na timu Mwalikwa Times Fm 100.5.
Aidha vyuo vyote vinavyohusika na michezo ya wiki hii zimetakiwa kuwahi Viwanjani ili kukamilisha taratibu za ukaguzi kabla ya michuano hiyo ya mtoano kuanza na ikumbukwe kwamba michuano hiyo inaendeshwa kwa mfumo wa Bonanza na inafanyika kila siku za jumamosi kutokana na wanafunzi kuwa masomoni katika siku za kawaida.
kila mwaka michuano hii itakuwa ikifanyika kwa kushirikisha vyuo mbali mbali  vya elimu ya kati  hapa nchini Tanzania na vilivyopata usajili wa kudumu wa NACTE ambapo Kanda mbali mbali za Tanzania kupitia vyuo vyao vitashindana katika michezo mbali mbali kwa wavulana na wasichana
ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA ndizo zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER COLLEGE DAR ES SALAAM.
Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji  kwa viongozi wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa Michezo,Fedha,  na Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.

Wadhamini aliojitokeza mpaka sasa na kuonyesha nia ya kusaidia mashindano hayo ni pamoja na Coca Cola, Vodacom, MLONGE BY MAKAI, CXC –Tours, na 100.5 Times Fm.  lakini hata hivyo dirisha la wadhamini bado liko wazi kwa maana bado gharama ni kubwa za uendeshaji ambapo wajitokeze waweze kusaidia michezo hii iliyoanza kwa shamrashamra nyingi na kuwa na mvuto kwa watazamaji ususani wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliojitokeza.

Season TWO -ISW -ground Kijitonyama 29/11/2014
Institute of Adult Education



St. Joseph  College (University).

Dar es salaam City College (DACICO




Season THREE -Njuweni ground Kibaha 6/12/2014









Season FOUR – UDSM - ground –UBUNGO 13/12/2014









NSSF
wana DACICO NJOONI KUSHANGILIA USHINDI SIKU YA KESHO KUTWA USTAWI WA JAMII HAPO NI KIPIGO TU KWA HAO WATAKAOJITOKEZA.

Jumamosi, 13 Septemba 2014

DACICO FC , FDC NGUVU SAWA KIBAHA

NACTE INTER COLLEGE TANZANIA-2014/2015- DAR ES SALAAM- YAPAMBA MOTO 

DACICO Qween kushusha kikosi cha Maangamizi

Na: Violet John (Kihaba).

Timu ya chuo cha Uandishi wa habari wa habari na utawala Dar es salaam city college (DACICO mwishoni mwa juma ili siku ya ijumaa Septemba 12, ilishindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya FDC ya Tumbi Kibaha Pwani , baada ya kumaliza muda wa dakika 90 kwa mabao 2-2 mchezo uliochezwa katika viwanja vya Hospitali ya Tumbi wilayani Kihaba mkoa Pwani.
Mchezo huo kwa upande wa kikosi cha DACICO ni maandalizi ya kushiriki kwenye Bonanza la Vyuo vya Elimu ya kati kwa Kanda Dar es Salaam na Pwani, NACTE INTER COLLEGE BONANZA 2014/2015, Bonanza ambalo linashirikisha vyuo mbali mbali ambavyo vimepata usajili wa serikali na kuwa chini ya NACTE TANZANIA linalotarajia kufanyika kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Viwanja vya Shule ya Kibaha Pwani.
FDC iliutumia mchezo huo kama mandalizi ya ligi ya Diwani inayotarajia kutimua vumbi ivi karibuni katika viwanja vya shule ya Sekondari Kibaha, ambapo iliwachukua dakika tano tu ya kipindi cha kwanza kujihakikishia bao mla kuongoza kupitia kwa kiungo mchezeshaji Deus Denes, aliyekuwa amevalia jezi namba saba mgongoni kuweza kuwainua mashabiki wao waliokuwa wamefurika katika uwanja wao wa nyumbani.
Hali ilizidi kuwa mbaya kwa upande wa timu ya Chuo cha DACICO pale ilipojikuta ikipigwa Sindano mbili za haraka haraka, Moja ikiwa ya kutuliza na kuweka Misuli joto na Ingine ya kupunguza Uchovu kwa timu ya DACICO iliyokuwa imewasili muda mfupi ikitokea Makao Makuu ya Chuo yaliyopo Kibamba CCM jijini Dar Es Salaam, kutoka kwa washika Sindano hao wa HOSPITALI ya Tumbi, baada ya Timoth matshala mchezaji wa FDC aliyekuwa amevalia jezi namba kumi mgongoni kupachika bao kunako dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza.
Dacico Fc ambao kwa hakika imepania kufanya vizuri katika Bonanza la Vyuo shiriki la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015, ilikuja juu baada ya kutandikwa dripu hizo mbili, na kuanza kufanya mashambulizi ya nguvu kwenye lango la FDC iliyokuwa imebweteka baada ya kupata mabao hayo mawili, hivyo Dacico iliutumia nafasi hiyo kunako dakika ya 30 mchezaji wa kutumainiwa wa Dacico mshambuliaji nyota ambaye anamudu pia katika nafasi ya kiungo, Moody Mapanki AKA Ronaldo, aliweza kuwainua juu mashabiki wa DACICO baada ya kufunga bao kwa ufundi wa hali ya juu pale mpira ulipompita mlinda mlango wa FDC Henry John dakika ya 30 baada ya kufunga bao linguine kwa dacico katika dakika ya 10 likiwa ni bao la kusawazisha na kuamusha vifijo na nderemo za mashabiki wa Dacico waliokuwa kwa muda wote kimya kutokana na kichapo cha mabao mawili ya haraka haraka katika kipindi hicho cha kwanza.
Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko zilitoshana nguvu ya mabao 2-2, ambapo kipindi cha pili pamoja na timu zote kufanya mabadiliko, hali hiyo haikuleta matunda kwa timu zote mbili hadi mwisho wa mchezo timu hizo ziligawana pointi moja moja.
Akizungumza baada ya mchezo kumalizika, mlinda mlango wa timu ya FDC Henry John, alisema kuwa awali walibweteka kutokana na kuusoma mchezo huo vibaya “ Matokeo ya mchezo huu kweli umekuwa ni tofauti kabisa na matarajio yetu, mchezo umekuwa mgumu sana, maana tulivyotarajia sivyo walivyokuja hawa wenzetu wa dacico, mwanzo tulidhani kuwa tumeshawamudu na tulikuwa tunacheza vizuri tu lakini kama unavyofahamu mpira ni mchezo wa makosa, kwa hiyo unapoteleza kidogo ndipo mpinzani anapochukua hatua kwa haraka na ndivyo ilivyotokea kwa hawa DACICO, mwanzo tulidhani hawatakuwa na mazoezi kinyume na matarajio yetu, lakini kwa kuwa wapo katika maandalizi ya Bonanza la vyuo vya Elimu ya Kati NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, basi wajiibidishe tu mazoezi lakini timu yao ni nzuri na wanaweza kufanya vizuri katika bonanza hilo” alisema mlinda mlango huyo wa FDC Henry John.
Mpambano mwingine baina ya timu hizo unatarajiwa kufanyika baada ya mwezi mmoja kabla ya tarehe ya mashindano ya vyuo vya elimu ya kati ambapo wachezaji na makocha wa timu zote mbili wametambiana kuibuka na ushindi kila mmoja, katika mchezo wa mwisho uliofanyika ivi karibuni kabla ya mchezo wa juzi timu ya Dacico ilikuwa ikishikilia rekodi ya kuifunga timu hiyo katika uwanja wao kwa jumla ya bao 1-0.Dacico iliwatumia zaidi wachezaji wapya ambao ndiyo kwanza wameingia kuanza masomo lakini hata hivyo Bado kocha mkuu wa Dacico anayo kazi ya kupata kikosi cha kwanza kutokana na wachezaji wote kuwa katika hali nzuri ya mchezo.
Naye kocha wa timu ya Dacico Mwalimu Kelvin alisema maandalizi ya kushiriki Bonanza la NACTE kwa upande wao wanaendelea vizuri na ndiyo wapo kwenye ratiba ya kucheza michezo mingi ya kirafiki “Sisi tupo kwenye maandalizi ya kushiriki Tamasha la Michezo la Vyuo vya Elimu ya Kati, linalotarajiwa Mungu akipenda kufanya mwezi wa kumi na moja tarehe za 21 huko, wachezaji wangu wengi wazoefu kwa muda huu wapo likizo, hapa wamekuja wengi wapya, na safari hii wamejitokeza wanafunzi wengi DACICO wanamichezo hata mimi mwenyewe nashindwa nitaipanga vipi hii timu, na ndiyo maana tumeanza kufungwa dakika za mwanzo kutokana na kutojuana kwa wachezaji wangu, hawaja kaa na kucheza pamoja, ndiyo kwanza wanaanza kuzoeana, lakini hata hivyo kutokana na uzoefu nilionao, nimeweza kubaini makosa kwa haraka na kufanya marekebisho na ndiyo maana tukasawazisha magoli hayo kwenye hicho hicho kipindi walichotufunga hawa wenzetu wa EDC, maana hata hii timu siyo ya kubeza, ni timu imara imeonyesha uwezo mkubwa sana, wachezaji wangu ni vijana nilitegemea wangewatoa udenda hawa vibabu wa fdc lamkini kumbe nao wamekamilika, wameutumia vizuri uwanja wao na sisi mwishoni mwa mwezi au kabla ya Bonanza la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015, tutapanga mchezo mwingine wa mwisho na hawa hawa maana wamenipa changamoto nzuri,wiki hii jumamosi tunatarajia kucheza na timu ya majirani zetu Timu ya Veterani ya Kibamba Hospitali kwenye Uwanja wa Kibamba Hospitali siku ya ijumaa, michezo hii kwetu ni maandalizi tunahitaji kuwa fiti kwa timu zote za wanawake na wanaume, isipokuwa nichukue fulsa hii kuvihamasisha vyuo vingine pia kufanya maandalizi Mapema” alisema Kelvin
Mwisho.

Alhamisi, 4 Septemba 2014

Msongamano wa Magari Daraja la Kibamba Chama siku Zinahesabika

Na:Violet John (DACICO)

Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro katika eneo la Daraja lililopo kati kati ya  Kibamba Chama na Kibamba Hospitali unaonekana kutia matumaini kwa sasa kutokana na ujenzi huo kufikia hatu nzuri inayokuja kuondokana na tatizo la vyombo vingi vya usafiri kukwama kwa masaa mengi pale inapotokea mojawapo ya gari kushindwa kupanda kilima hicho ambacho kimesumbua sana Madereva wa malori na Mabasi yanayokuwa hayana nguvu za kuweza kuimili urefu wa kilima hivyo kusababisha msongamano wa magari kitendo ambacho imekuwa ni kero ya muda mrefu kwa Magari yaendayo mikoani na yanayoingia jijini Dar es Salaam.

Barabara hiyo ambayo kwa sasa inaonekana kuwekwa matoleo ya njia mbadala wakati inapotokea uharibifu wa gari,ujenzi unaendelea kwa hatua ya kurizisha pamoja na kwamba imewachukua muda mrefu kukamilisha kipande cha njia hizo toka kwa Mangi hadi kibamba chama.
Aidha eneo hilo ambalo kwa mujibu wa wakazi wa maeneo hayo kabla ya kuanza kuwekwa matoleo hayo, ilikuwa ikitishiwa amani kwa madereva na wakazi wa maeneo hayo kutokana na wimbi kubwa la vijana wa kiuni waliokuwa wakivizia wakati magari yanaposhindwa kuimili urefu wa kilima ama kwenda mwndo mdogomdogo, wao walikuwa na tabia za kuiba mali na hata kuwatishia wenye vyombo hivyo vya usafiri ususani masaa ya usiku.
“tunamshuku sana mheshimiwa wetu Magufuli, maana nahisi ndiye aliyewatuma hawa kufanya huu ujenzi wa hii barabara, kweli kabisa tunampongeza sana, ameweza kutuondolea hadha kubwa ya vitisho vya hawa vijana waliokuwa wakivizia tu magari yakshindwe kupanda vilima ili wao waweze kuwaibia mali zao, na wakati wakifanya hivyo njia walizokuwa wakizitumia kukimbia ni maeneo ya nyumba zetu, nap engine Serikali ingeweza siku moja kutuhusisha katika haya matatizo, mimi nikiwa ni mmoja wa wakazi wa Kibamba hapa niseme tu kuwa hili sasa linakaribia kumalizika, maana hatua waliyofikia siyo mbaya na hata unaona sasa pamoja nakwamba upanuzi tayari kilichobaki ni kuweka tu lami, lakini muda huu hata kama gari ikikwamba katikati ya barabara bado njia hizo za fumbi zitawawezesha wengine kuendelea na safari” alisema Ombeni Msangi
Ujenzi huo unaendelea kila siku ambapo kampuni inayofanya ujenzi wa Barabara za Jiji la dare s salaam  ndiyo wanaoendelea kukamilisha eneo hilo ambalo hapo nyuma limesababisha uharibifu wa mali na vyombo vingi vya usafiri , isipokuwa Serikali inatakiwa kuongeza jitiada za makusudi kuhakikisha eneo hilo linamalizika mara moja ili kutoa unafuu wa madereva kuvuka na kuendelea na safari zao.
Mwisho
================================================================

KIBAMBA CHAMA WAKAZI WAMEIOMBA SERIKALI KUTENGE MAENEO MAALUMU KWA AJILI YA MINADA

Na: Violet John (DACICO)

Wakazi wa Kibamba na Wafanyabiashara wa Mnada wa kila jumatano katika eneo la barabara ya vumbi(Service road) eneo ambalo serikali imetenga kwa ajili ya kufanyika kwa mnada huo wa kila siku ya jumatano, imelalamikiwa na wakazi wengi wa maeneo hayo na kuitaka Serikali kutafuta sehemu ambayo itakidhi usalama wao kwa ujumla.
Wakizungumzia hali ambayo ujitokeza mara kwa mara wakati wa biashara hapo Kibamba chama wakazi na waf
anyabiashara wa minada walisema kuwa  “Suala la mnada ni zuri sana kwa sababu linaturahisishia sana sisi watoto wa masikini kupata mahitaji mengi kwa gharama kidogo, na kama unavyoona kwamba hapa nimenunua bidhaa nyingi lakini kwa bei nafuu zasa ukilinganisha ningekwenda kunununu bidhaa hizi sehemu zingine kama Kariakoo, Manzese, na posta, nimenunu fungu la viatu furushi kwa shilingi elfu moja tu, tatizo hapa ni eneo ambalo serikali imetenga maana kama unavyoona hapa bidhaa zimewekwa hata karibu na barabara hii kubwa tena yenye mabasi yanayokwenda mwendo wa hatari, malori ndiyo njia yake kuu hii ya Morogoro, kwa hiyo ni harai sana kwa upande mwingi, itakapotokea gari likiacha njia basi wafanyabiashara na watu wengi sana watapoteza maisha hapa, Serikali itazame hili, siyo kwamba hatutaki huu Mnada ila eneo hili walilopewa kufanya biasha hapa ndiyo sehemu hatari” alisema kijana ambaye ni mkazi wa kibamba Ramadhani Kavel
“Naitwa Blanca Arbert mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari hapa jirani Dar es Salaam City College, ila kwa sasa ni mkazi wa eneo hili la kibamba chama, kwa ujumla kuhusu mnada ni suala zuri na naona kuna vitu vingi tofauti tofauti, ni eneo safi na zuri kutokana na sisi kupata bidhaa nyingi kwa bei nafuu, lakini kubwa niseme tu ni kuhusu hii njia ya barabara kwani siyo sehemu official kwa ajili ya biashara pamoja na kwamba sisi tunafurahi kwa ukaribu tulionao nyumba moja tu tumefika, ila tujaribu kuzungumza na serikali ya kijiji ili itazame kwa undani sana kupata eneo la biashara hii ambayo kwa kweli inasaidia wakazi wa Kibamba kupata mahitaji yao muhimu” alisema Blanca
Naye juma ambaye ni mfanya biashara za nguo alisema kuwa kwa upande wao wanamshukuru mungu kwa serikali kutenga eneo hilo, japo ni eneo dogo kwao lakini linaendelea kukidhi haja ya mahitaji ya biashara zao, akizungumzia unafuu wa mnada huo ukiachilia mbali nguzo alisema kuwa Chungwa linauzwa 100 siku za mnada, siku za kawaida linauzwa zaidi ya 30 hadi 500, na hata ukiangalia bidhaa zinazouzwa wakati wa mnada  bei yake ni tofauti kabisa na siku zingine ama ukienda kwenye maduka baada ya mnada utakuta bei inawatatiza wakazi wa maeneo hayo kutokana na kipato wanachopata kwa ajili ya kuendesha familia zao,
“Hapo awali huu mnada haukuwa hapa kama unakumbuka ilikuwa kule njia panda, lakini tuliamka siku moja serikali ikasema imeamisha eneo hilo la mnada na kupeleka nyuma ya stand ya kuelekea maili moja kwa hapa kibamba chama, eneo hilo pia alikuwa salama na tulijaribu kuiomba serikali ili itafute njia ya kupata eneo litakalotuwezesha kwa umoja kuwa na amani nikimaanisha wafanyabiashara na wateja wote kwa pamoja tuwe na amani, maana kama unavyoona mwenyewe kaeneo haka ni kadogo sana, msongamano unakuwa mkubwa, utadhani tupo mtaa wa Kongo, nah ii ni hatari sana sit u kwa wakazi ama wafanyabiashara, ila siku ikitokea majanga, kutokana na vyombo vyetu vya usafiri basi siku hiyo litazungumzwa lingine, na si hivyo tu lakini pia purukushani zinazoendelea na kukanyagana pia inasababishwa na ufinyu wa eneo, kweli tunahitaji sana huu mnada kwa kuwa ndiyo pekee unaotupatia bidhaa nyingi kwa bei nafuu, n animalize kwa kusema kwamba, wakati serikali inatafuta ardhi kwa ajili ya mambo yake mara moja upatikana lakini inapotafuta kama ivi wanasema hakuna maeneo kitu ambacho si kweli, Serikali ibadilike na iweze kutambua mahitaji ya sisi wananchi wake au wanadhani kua wananchi wao wengine zaidi yetu Watanzania”? Alioji mama huyo ambaye alisema anaitwa mama boya
Naye mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kibamba chama Bwana  Kayombo Kayombo alipoulizwa kuhusiana na mpango mkakati kuhusiana na upatikanaji wa eneo kubwa litakalokidhi hitaji hilo alisema kuwa kwa sasa hawezi kusema chochote kutokana na kwamba Serikali ipo kwenye mikakati hiyo na ndiyo maana baada ya kuondolewa kwenye maeneo ya mwanzo waliweza kuwekwa hapo kwa muda wakisubiri kuwatangazia eneo ambalo litakuwa la kudumu kwa ajili yam nada wa Kibamba Chama ambao unakidhi mahitaji ya wakzi wa maeneo hayo na vitongoji vya jirani.
Mnada huo wa kibamba chama ni mnada ambao unafanyika kila siku ya jumatano ambapo wafanyabiashara mbalimbali kutoka maeneo mengi kwa bidhaa zao tofauti tofauti wanafika na kupanga biashara chini kwa ajili ya kuwauzia wakazi wa Kibamba chama na vitongoji vyake, na mara nyingi mnada huo uanza majira ya saa kamili asubuhi mpaka saa moja kamili usiku,
Mwisho

WASAFIRI WA BASI LA AMANI EXPRESS WALALAMIKA BAADA YA KUSOTA NJIANI

Na: Violet John (DACICO)

Abiria waliokuwa wakisafiri jana na basi la Amani Express aina ya Scania lenye usajili namba T-846 BGU, lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Kahama, lilishindwa kuendelea na safari hiyo muda mfupi baada ya kuondoka katika Stand kuu za Ubungo jijini Dar ers Salaam kutokana na itilafu ya injini ya gari hiyo.
Wakizungumzia hali hiyo ya kuondoka tu stand kisha kushindwa kuendelea na safari kwa mwendo wa muda mfupi, abiria waliokuwa katika basi hilo walisema kuwa inashangaza kwa kuwa dereva na kondakta walitakiwa kufanya ukaguzi mapema ili kubaini tatizo kabla ya kuanza safari hiyo ambayo hata hivyo walisema ni ubabaishaji wa wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao wanapenda kupokea fedha bila kuwa na uhakika wa safari zao.
“naitwa juma Mussa mfanyabiasha katika Mkoa wa Kahama, na hapa nimebeba baadhi ya vifaa ambavyo ni kwa ajili ya wateja ambao waliniagiza na wanatakiwa kupata mizigo yao jioni na kama unavyoona sasa hali hii sidha ni tena kama safari hii itafanyika kama ilivyopangwa, maana kinachonishangaza hapa ni vipi hawa wahusika wameshindwa kutengeneza gari yao kabla ya kuchukua pesa zetu, magari yalikuwapo mengi ningeweza kupanda basi ingine, angalia ivi sasa wanasema kuwa watafute gari (basi) lingine ambalo linaelekea huko watupakize, huu unakuwa ni usumbufu kwa kweli” alisema Mussa Juma
Naye Kondakta wa basi hilo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa basi hilo lilishindwa kuendelea na safari yake kutokana na itilafu ya injini tatizo ambalo limeibuka baada ya kuwa wameanza safari hiyo ya kuelekea Kahama na iliwachukua muda mfupi katika safari hiyo kasha wakabaini kwamba tatizo lililopo ni kubwa ambalo ni la injini.
“Ni kweli kwamba tupo hapa gari imepata tatizo lakini hata hivyo tunajaribu kufanya utaratibu wa kuhakikisha kwamba abiria ambao ni wateja wetu wanapata usafiri mwingine wa kuwafikisha katika safari zao endapo tukibaini kwamba tatizo hili limeshindikana kutatuliwa kwa muda huu, maana tunalazimika kutafuta njia mbadala lakini pia abiria wanatakiwa kuwa na subira ili ni gari, alisemi wala hakuna aliyeweza kutambua wapi lilitakiwa marekebisho na ili utambue ubovu wa gari ni mpaka liharibike kwa hiyo wao wasubiri kwanza ikishindikana watapatiwa usafiri mwingine kwani tunajaribu kuomba msaada zaidi kutoka katika ofisi zetu za jijini Dar es Salaam”alisema kondakta wa basi hilo
Basi hilo lilishindwa kuendelea na safari hiyo majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi tu toka kuondoka katika stand kuu za Ubungo na ilipo fika maeneo ya Daraja la Kibamba kuelekea chama ndipo liliposhindwa kupanda kilima na kuwekwa pembeni kwa ajili ya utaratibu mwingine.
Aidha wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri wametakiwa kuwa waangalifu na wafuatiliaji wa karibu kwa watendaji wao kutatua matatizo yanayoweza kusababisha usumbufu kwa abiria na hata wakati mwingine ubovu wa basi unaweza kupelekea kusababisha ajali na kuleta maafa, hivyo wametakiwa kuchukua taadhali mapema kwa ajili ya kuboresha huduma zao.
Hata hivyo Abiria zaidi ya 40 waliokuwa katika basi hilo hatimaye waliweza kupandishwa kwenye mabasi mengine kwa awamu kwa ajili ya kuendelea na safari hiyo ambayo basi hilo lilishindwa kuendelea na safari na hivyo kulazimika kutafuta wataalamu kwa ajili ya kufika kulifanyia matengenezo.
Mwisho.