Alhamisi, 4 Septemba 2014

KIBAMBA CHAMA WAKAZI WAMEIOMBA SERIKALI KUTENGE MAENEO MAALUMU KWA AJILI YA MINADA

Na: Violet John (DACICO)

Wakazi wa Kibamba na Wafanyabiashara wa Mnada wa kila jumatano katika eneo la barabara ya vumbi(Service road) eneo ambalo serikali imetenga kwa ajili ya kufanyika kwa mnada huo wa kila siku ya jumatano, imelalamikiwa na wakazi wengi wa maeneo hayo na kuitaka Serikali kutafuta sehemu ambayo itakidhi usalama wao kwa ujumla.
Wakizungumzia hali ambayo ujitokeza mara kwa mara wakati wa biashara hapo Kibamba chama wakazi na waf
anyabiashara wa minada walisema kuwa  “Suala la mnada ni zuri sana kwa sababu linaturahisishia sana sisi watoto wa masikini kupata mahitaji mengi kwa gharama kidogo, na kama unavyoona kwamba hapa nimenunua bidhaa nyingi lakini kwa bei nafuu zasa ukilinganisha ningekwenda kunununu bidhaa hizi sehemu zingine kama Kariakoo, Manzese, na posta, nimenunu fungu la viatu furushi kwa shilingi elfu moja tu, tatizo hapa ni eneo ambalo serikali imetenga maana kama unavyoona hapa bidhaa zimewekwa hata karibu na barabara hii kubwa tena yenye mabasi yanayokwenda mwendo wa hatari, malori ndiyo njia yake kuu hii ya Morogoro, kwa hiyo ni harai sana kwa upande mwingi, itakapotokea gari likiacha njia basi wafanyabiashara na watu wengi sana watapoteza maisha hapa, Serikali itazame hili, siyo kwamba hatutaki huu Mnada ila eneo hili walilopewa kufanya biasha hapa ndiyo sehemu hatari” alisema kijana ambaye ni mkazi wa kibamba Ramadhani Kavel
“Naitwa Blanca Arbert mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari hapa jirani Dar es Salaam City College, ila kwa sasa ni mkazi wa eneo hili la kibamba chama, kwa ujumla kuhusu mnada ni suala zuri na naona kuna vitu vingi tofauti tofauti, ni eneo safi na zuri kutokana na sisi kupata bidhaa nyingi kwa bei nafuu, lakini kubwa niseme tu ni kuhusu hii njia ya barabara kwani siyo sehemu official kwa ajili ya biashara pamoja na kwamba sisi tunafurahi kwa ukaribu tulionao nyumba moja tu tumefika, ila tujaribu kuzungumza na serikali ya kijiji ili itazame kwa undani sana kupata eneo la biashara hii ambayo kwa kweli inasaidia wakazi wa Kibamba kupata mahitaji yao muhimu” alisema Blanca
Naye juma ambaye ni mfanya biashara za nguo alisema kuwa kwa upande wao wanamshukuru mungu kwa serikali kutenga eneo hilo, japo ni eneo dogo kwao lakini linaendelea kukidhi haja ya mahitaji ya biashara zao, akizungumzia unafuu wa mnada huo ukiachilia mbali nguzo alisema kuwa Chungwa linauzwa 100 siku za mnada, siku za kawaida linauzwa zaidi ya 30 hadi 500, na hata ukiangalia bidhaa zinazouzwa wakati wa mnada  bei yake ni tofauti kabisa na siku zingine ama ukienda kwenye maduka baada ya mnada utakuta bei inawatatiza wakazi wa maeneo hayo kutokana na kipato wanachopata kwa ajili ya kuendesha familia zao,
“Hapo awali huu mnada haukuwa hapa kama unakumbuka ilikuwa kule njia panda, lakini tuliamka siku moja serikali ikasema imeamisha eneo hilo la mnada na kupeleka nyuma ya stand ya kuelekea maili moja kwa hapa kibamba chama, eneo hilo pia alikuwa salama na tulijaribu kuiomba serikali ili itafute njia ya kupata eneo litakalotuwezesha kwa umoja kuwa na amani nikimaanisha wafanyabiashara na wateja wote kwa pamoja tuwe na amani, maana kama unavyoona mwenyewe kaeneo haka ni kadogo sana, msongamano unakuwa mkubwa, utadhani tupo mtaa wa Kongo, nah ii ni hatari sana sit u kwa wakazi ama wafanyabiashara, ila siku ikitokea majanga, kutokana na vyombo vyetu vya usafiri basi siku hiyo litazungumzwa lingine, na si hivyo tu lakini pia purukushani zinazoendelea na kukanyagana pia inasababishwa na ufinyu wa eneo, kweli tunahitaji sana huu mnada kwa kuwa ndiyo pekee unaotupatia bidhaa nyingi kwa bei nafuu, n animalize kwa kusema kwamba, wakati serikali inatafuta ardhi kwa ajili ya mambo yake mara moja upatikana lakini inapotafuta kama ivi wanasema hakuna maeneo kitu ambacho si kweli, Serikali ibadilike na iweze kutambua mahitaji ya sisi wananchi wake au wanadhani kua wananchi wao wengine zaidi yetu Watanzania”? Alioji mama huyo ambaye alisema anaitwa mama boya
Naye mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kibamba chama Bwana  Kayombo Kayombo alipoulizwa kuhusiana na mpango mkakati kuhusiana na upatikanaji wa eneo kubwa litakalokidhi hitaji hilo alisema kuwa kwa sasa hawezi kusema chochote kutokana na kwamba Serikali ipo kwenye mikakati hiyo na ndiyo maana baada ya kuondolewa kwenye maeneo ya mwanzo waliweza kuwekwa hapo kwa muda wakisubiri kuwatangazia eneo ambalo litakuwa la kudumu kwa ajili yam nada wa Kibamba Chama ambao unakidhi mahitaji ya wakzi wa maeneo hayo na vitongoji vya jirani.
Mnada huo wa kibamba chama ni mnada ambao unafanyika kila siku ya jumatano ambapo wafanyabiashara mbalimbali kutoka maeneo mengi kwa bidhaa zao tofauti tofauti wanafika na kupanga biashara chini kwa ajili ya kuwauzia wakazi wa Kibamba chama na vitongoji vyake, na mara nyingi mnada huo uanza majira ya saa kamili asubuhi mpaka saa moja kamili usiku,
Mwisho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni