Alhamisi, 4 Septemba 2014

Msongamano wa Magari Daraja la Kibamba Chama siku Zinahesabika

Na:Violet John (DACICO)

Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro katika eneo la Daraja lililopo kati kati ya  Kibamba Chama na Kibamba Hospitali unaonekana kutia matumaini kwa sasa kutokana na ujenzi huo kufikia hatu nzuri inayokuja kuondokana na tatizo la vyombo vingi vya usafiri kukwama kwa masaa mengi pale inapotokea mojawapo ya gari kushindwa kupanda kilima hicho ambacho kimesumbua sana Madereva wa malori na Mabasi yanayokuwa hayana nguvu za kuweza kuimili urefu wa kilima hivyo kusababisha msongamano wa magari kitendo ambacho imekuwa ni kero ya muda mrefu kwa Magari yaendayo mikoani na yanayoingia jijini Dar es Salaam.

Barabara hiyo ambayo kwa sasa inaonekana kuwekwa matoleo ya njia mbadala wakati inapotokea uharibifu wa gari,ujenzi unaendelea kwa hatua ya kurizisha pamoja na kwamba imewachukua muda mrefu kukamilisha kipande cha njia hizo toka kwa Mangi hadi kibamba chama.
Aidha eneo hilo ambalo kwa mujibu wa wakazi wa maeneo hayo kabla ya kuanza kuwekwa matoleo hayo, ilikuwa ikitishiwa amani kwa madereva na wakazi wa maeneo hayo kutokana na wimbi kubwa la vijana wa kiuni waliokuwa wakivizia wakati magari yanaposhindwa kuimili urefu wa kilima ama kwenda mwndo mdogomdogo, wao walikuwa na tabia za kuiba mali na hata kuwatishia wenye vyombo hivyo vya usafiri ususani masaa ya usiku.
“tunamshuku sana mheshimiwa wetu Magufuli, maana nahisi ndiye aliyewatuma hawa kufanya huu ujenzi wa hii barabara, kweli kabisa tunampongeza sana, ameweza kutuondolea hadha kubwa ya vitisho vya hawa vijana waliokuwa wakivizia tu magari yakshindwe kupanda vilima ili wao waweze kuwaibia mali zao, na wakati wakifanya hivyo njia walizokuwa wakizitumia kukimbia ni maeneo ya nyumba zetu, nap engine Serikali ingeweza siku moja kutuhusisha katika haya matatizo, mimi nikiwa ni mmoja wa wakazi wa Kibamba hapa niseme tu kuwa hili sasa linakaribia kumalizika, maana hatua waliyofikia siyo mbaya na hata unaona sasa pamoja nakwamba upanuzi tayari kilichobaki ni kuweka tu lami, lakini muda huu hata kama gari ikikwamba katikati ya barabara bado njia hizo za fumbi zitawawezesha wengine kuendelea na safari” alisema Ombeni Msangi
Ujenzi huo unaendelea kila siku ambapo kampuni inayofanya ujenzi wa Barabara za Jiji la dare s salaam  ndiyo wanaoendelea kukamilisha eneo hilo ambalo hapo nyuma limesababisha uharibifu wa mali na vyombo vingi vya usafiri , isipokuwa Serikali inatakiwa kuongeza jitiada za makusudi kuhakikisha eneo hilo linamalizika mara moja ili kutoa unafuu wa madereva kuvuka na kuendelea na safari zao.
Mwisho
================================================================

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni