Alhamisi, 4 Septemba 2014

WASAFIRI WA BASI LA AMANI EXPRESS WALALAMIKA BAADA YA KUSOTA NJIANI

Na: Violet John (DACICO)

Abiria waliokuwa wakisafiri jana na basi la Amani Express aina ya Scania lenye usajili namba T-846 BGU, lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Kahama, lilishindwa kuendelea na safari hiyo muda mfupi baada ya kuondoka katika Stand kuu za Ubungo jijini Dar ers Salaam kutokana na itilafu ya injini ya gari hiyo.
Wakizungumzia hali hiyo ya kuondoka tu stand kisha kushindwa kuendelea na safari kwa mwendo wa muda mfupi, abiria waliokuwa katika basi hilo walisema kuwa inashangaza kwa kuwa dereva na kondakta walitakiwa kufanya ukaguzi mapema ili kubaini tatizo kabla ya kuanza safari hiyo ambayo hata hivyo walisema ni ubabaishaji wa wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao wanapenda kupokea fedha bila kuwa na uhakika wa safari zao.
“naitwa juma Mussa mfanyabiasha katika Mkoa wa Kahama, na hapa nimebeba baadhi ya vifaa ambavyo ni kwa ajili ya wateja ambao waliniagiza na wanatakiwa kupata mizigo yao jioni na kama unavyoona sasa hali hii sidha ni tena kama safari hii itafanyika kama ilivyopangwa, maana kinachonishangaza hapa ni vipi hawa wahusika wameshindwa kutengeneza gari yao kabla ya kuchukua pesa zetu, magari yalikuwapo mengi ningeweza kupanda basi ingine, angalia ivi sasa wanasema kuwa watafute gari (basi) lingine ambalo linaelekea huko watupakize, huu unakuwa ni usumbufu kwa kweli” alisema Mussa Juma
Naye Kondakta wa basi hilo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa basi hilo lilishindwa kuendelea na safari yake kutokana na itilafu ya injini tatizo ambalo limeibuka baada ya kuwa wameanza safari hiyo ya kuelekea Kahama na iliwachukua muda mfupi katika safari hiyo kasha wakabaini kwamba tatizo lililopo ni kubwa ambalo ni la injini.
“Ni kweli kwamba tupo hapa gari imepata tatizo lakini hata hivyo tunajaribu kufanya utaratibu wa kuhakikisha kwamba abiria ambao ni wateja wetu wanapata usafiri mwingine wa kuwafikisha katika safari zao endapo tukibaini kwamba tatizo hili limeshindikana kutatuliwa kwa muda huu, maana tunalazimika kutafuta njia mbadala lakini pia abiria wanatakiwa kuwa na subira ili ni gari, alisemi wala hakuna aliyeweza kutambua wapi lilitakiwa marekebisho na ili utambue ubovu wa gari ni mpaka liharibike kwa hiyo wao wasubiri kwanza ikishindikana watapatiwa usafiri mwingine kwani tunajaribu kuomba msaada zaidi kutoka katika ofisi zetu za jijini Dar es Salaam”alisema kondakta wa basi hilo
Basi hilo lilishindwa kuendelea na safari hiyo majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi tu toka kuondoka katika stand kuu za Ubungo na ilipo fika maeneo ya Daraja la Kibamba kuelekea chama ndipo liliposhindwa kupanda kilima na kuwekwa pembeni kwa ajili ya utaratibu mwingine.
Aidha wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri wametakiwa kuwa waangalifu na wafuatiliaji wa karibu kwa watendaji wao kutatua matatizo yanayoweza kusababisha usumbufu kwa abiria na hata wakati mwingine ubovu wa basi unaweza kupelekea kusababisha ajali na kuleta maafa, hivyo wametakiwa kuchukua taadhali mapema kwa ajili ya kuboresha huduma zao.
Hata hivyo Abiria zaidi ya 40 waliokuwa katika basi hilo hatimaye waliweza kupandishwa kwenye mabasi mengine kwa awamu kwa ajili ya kuendelea na safari hiyo ambayo basi hilo lilishindwa kuendelea na safari na hivyo kulazimika kutafuta wataalamu kwa ajili ya kufika kulifanyia matengenezo.
Mwisho. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni