Jumatatu, 25 Novemba 2013

DACICO VS GLOBAL- ZATAMBIANA TEGETA

 Baadhi ya Wachezaji wa DACICO FC, wakiwa kwenye maandalizi ya mchezo huo
  Baadhi ya Wachezaji wa GLOBAL  FC, wakiwa kwenye maandalizi ya mchezo huo
 KIKOSI CHA GLOBAL FC
 KIKOSI CHA DACICO FC
 Wachezaji wa Timu wa DACICO  Vs GLOBAL, wakichuana Vikali katika mpambano huo.
 Baadhi ya Mashabiki wa DACICO wakifuatilia kwa makini mpambano
 Nyota wa DACICO, Said(mbele) akimtoka kiungo mchezeshaji wa GLOBAL, Moland, wakati wa mpambano
 Beki nyota wa timu ya DACICO FC, Mathias Canal, akijaribu kuondoa hatari zote kwenye lango la DACICO.
 Baadhi ya Mashabiki wa Timu ya Global Publishers, wakifuatilia kwa makini mpambano huo.
==================================================
Na: Wanafunzi DACICO.

imu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala, Dar es Salaam City College(DACICO TANZANIA, mwishoni mwa juma ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Global Publishers, katika Uwana wa Shule ya Sekondari Tegeta.
Katika Mchezo huo ambao Global ilionekana kuzidiwa kwa kiwango kikubwa, hadi timu zote zinakwenda mapumziko matokeo ilikuwa 0-0 kabla ya timu Zote kufanya mabadiliko ya Hapa na pale, ambapo Global ilibidi kuwatumia wachezaji wa kukodi(Mamruki) na kuweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Akizungumzia mchezo huo, kocha wa timu ya DACICO FC, Ombeni, alisema kuwa kikosi chake pamoja na kupoteza mchezo huo ilitokana na wachezaji wengi kucheza bila mazoezi kutokana na kwamba muda mwingi waliutumia katika masomo kwani walikuwa katika maandalizi ya mitihani.
"tumefungwa na Global kwa mengi moja ni pamoja na kukosa mazoezi wachezaji wangu kutokana na kuwa kwenye maandalizi ya mitihani, pia wenzetu wa Global wametumia wachezaji Mamruki ambao siyo waajiliwa wao kama tulivyotarajia wangecheza wenyewe, wametuchezeshea wachezaji wa ligi sijui wamewachukua timu gani hawa maana wana kasi na mbio sana, lakini goli hilo moja tutarejesha wakati wa mchezo wa marudiano"alisema ombeni
mchezo mwingine wa marudiano unatarajia kuchezwa mwishoni mwa mwezi wa kumi na mbili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni