Jumamosi, 12 Aprili 2014

MJUMBE ATAJA ABABU ZA KUKATAA SERIKALI TATU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe dacicotanzania@gmail.com , au  namba +255713869133. 
Mbunge wa Kibaha Vijijini,Abuu Jumaa.
 
Mjumbe  wa Bunge Maalum la Katiba, Abuu Jumaa, amesema Tanzania haitakiwi kujiingiza katika masuala ya muundo wa Muungano wa serikali tatu kwa sababu bado ni nchi changa.
Akizungumza na NIPASHE jana, Jumaa ambaye pia ni Mbunge wa Kibaha Vijijini (CCM), alisema kwa sasa wanatakiwa kutatua changamoto zote zilizojitokeza kwenye serikali mbili ndiyo wafikirie muundo mwingine wa Muungano.

“Ni mapema sana kwa nchi yetu kujiingiiza katika masuala ya serikali tatu…sisi wenyewe tunaweza kujiona tumekuwa, lakini bado kabisa,” alisema.

Alisema utafiti uliofanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, umeonyesha kuwa changamoto zilizopo kwenye serikali mbili ni sita wakati za serikali tatu ni saba.

“Hatuwezi kwenda kwenye mfumo wa serikali tatu, maana muundo huo una changamoto nyingi na gharama zake ni kubwa ni bora twende kwanza na huu muundo wa serikali mbili,” alisema.

Aidha, alisema Watanzania wanatakiwa kuwa wavumilivu ikiwa ni pamoja na kufanyia marekebisho changamoto zilizojitokeza kwenye serikali mbili.

“Mimi sidhani kama wananchi wana uelewa kuhusu serikali tatu…wanatakiwa kwanza kupata elimu ya kutosha ili waweze kuelewa maana ya muundo wa serikali tatu na mbili,” alisema.

Alihoji: “Kama wasomi wamepata uelewa wa serikali mbili na serikali tatu… je wananchi wa kawaida ambao hawana uelewa huo itakuwaje?”

Aliwataka wananchi kusoma ili waelimishwe waelewe kuhusu muundo wa serikali tatu.

 “Hata siku katiba hii itakapokwenda kwa wananchi waende kupiga kura wakiwa na uelewa wa muundo wa serikali,” alisema.
SOURCE: NIPASHE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni