Jumatatu, 1 Septemba 2014

NAWINA RESORT YATIKISIKA NA ASIYEKUJUA AKUTHAMINI WA MASHAUZI CLASSIC.

Na: Blanca Albert (DACICO)

Kundi Maarufu la Muziki wa Taarabu jijin I Dar es Salaam lijulikanalo kwa jina la Mashauzi Classic, mwishoni mwa juma siku ya jumamosi,  liliweza kuitikisa mbagala katika Ukumbi wa Kisasa Nawina Resort uliopo mbagala kuu na kukonga nyoyo za Mashabiki.
Safu yetu iliweza kuongea na meneja wa Bendi hiyo bwana Ismail Rashid “Suma Rager”kwa niaba ya Mkurugenzi wake Aisha Ramadhani maarufu kwa jina la Aisha Mashauzi, ambaye pia alisema kuwa aisha hakuwa katika hali nzuri Kiafya hivyo hakuweza kupatikana baada ya kumaliza onyesho hilo .

Suma Rager ambaye alizungumza kwa kirufu alisema kuwa malengo ya Bendi hiyo ni kuwapa ajira watu mbali mbali katika bendi hiyo kwa kuzingatia uwezo na ufanisi wa kazi ya kila mmoja.
Pia alisemam kuwa lengo linguine ni kuhakikisha kwamba bendi hiyo inafikia hatua ya kuwa na vitendea kazi vyake ambavyo vitasaidia kuifanya bendi hiyo kujiendeleza zaidi katika suala zima la muziki wa hapa nyumbani.

Akizungumzia historia yak undo hilo kwa ufupi alisema kuwa, ni hatua za kujivunia mpaka sasa kwa hatua waliofikia, kwani pamoja na kuwa na ushindani wa Miziki hiyo ya Mwambao, lakini wameshafanikiwa kuwateka baadhi ya mashabiki wa miziki hiyo kutokana na vibao vyao kuwa vya kuwaridhisha mashabiki wake.
Jumla ya wanamuziki 32 wanajumuhisha kundi hilo akiwamo kiongozi wa kundi ambaye pia ndiye mkurugenzi mkuu na mwimbaji nyota anayetikisa katika vibao mbali mbali ukiwemo wimbo mpya wa asiyekujua akuthamini ulioitikisa mbagala kuu Aisha Ramadhani maarufu kama aisha Mashauzi.
Akizungumzia nyimbo mpya zinazotarajiwa kutoka hivi karibuni suma rager alisema kuwa “Sura siyo Roho” wimbo huo unaimbwa na mwimbaji nyota Aisha Ramadhani, na kwamba wanatarajia kuzindua wimbo wa “Wema hauuzwi na Ubaya Haulipizwi” wimbo ambao unaimbwa na mwanamuziki Asia Khamis Mzinga.
Kuhusu changamoto wanazokutana nazo ni kubwa, lakini kwao hakuna changamoto hizo kutokana na hapo awali muziki wa taarabu ulikuwa kama starehe tofauti na miaka hii ya sasa ambapo muziki huo umekuwa ni biashara inayoingiza pato kubwa na kukidhi mahitaji ya wanamuziki ndani ya kundi hilo.
Kuhusu ratiba ya maonyesho ya burudani wana mashauzi, Suma rager alisema kuwa  siku za kupata burudani zao ni Jumanne, alhamisi na ijumaa ambapo siku ya alhamisi inakuwa ni siku mama ya kuwapa burudani mashabiki wa kinondoni katika ukumbi wa Mango Gardeni.
Aliitimisha kwa kusema kuwa, kabla ya uzinduzi wa nyimbo hizo Mashauzi Classic wameandaa shoo kubwa mashabiki wasubiri siku watakayotangaziwa na wameahidi kufanya onyesho kabambe kabla ya uzinduzi huo wa nyimbo zao mpya.

Safu hii pia ilipata fulsa ya kuzungumza na Mkurugenzi wa Nawina Resort, Bi, Mery Komba, ambaye alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa hatua aliyoweza kufikia katika kuandaa Burudani katika Ukumbi wa Nawina Resort “ Namshuru Mungu kwa kuwa ameweza kunisimamia katika kuandaa tamasha hili, kwa si kitu rahisi na wateja wangu waendelee kutegemea vitu vizuri zaidi kwani nawapenda wote, na napenda kuchukua fulsa hii kuwakaribisha wakazi wa mbagala na vitongoji vyake katika ukumbi wa Nawina Resort mbagala kuu, kwani tunaendelea kuwaandaliwa vitu vingi vizuri vitakavyozidi kuwapa raha”alisema mary Komba.

Aidha ukumbi huo ambao unapatikana katika Eneo la mbagala kwa sasa umeendelea kuwa gumzo kutokana na maboresho yaliyofanyika baada ya kupata ajali ya moto hivi karibuni.
Kutokana na hivyo umeweza kuboreshwa na kuwa na eneo pana kwa ajili ya usalama, eneo la maegesho Parking za magari, pikipiki na baiskeli.

Kuhusu suala la usumbufu kwa wateja kwa sasa katika ukumbi huo hakuna kwani wateja wanaendelea kupata huduma inayostahili ikiwa ni pamoja na vinywaji na Chakula.

“Natarajia kuendelea kuukarabati ukumbi huu wa Nawina Resort, na matarajio makubwa ni kuwawekea wakazi wa mbagala Ukumbi wa kisasa wenye hadhi ya kimataifa itakayowatikisha watu mbali mbali ususani vijana wa hiki yaani wapenda burudani, (NIGHT CLUB) itakayo kuwa pamoja na ukumbi”aliongeza Mary Komba.

 Hata hivyo aliowataka wapenzi wote wa Nawina kukaribia kila siku kupata vinywaji na chakula vinavyoandaliwa kwa kiwango cha hali ya juu ukilinganisha na maeneo mengine .

Vibao vingine vinavyoendelea kutikisa ndani ya Mashauzi ni pamoja na kibao cha ropokeni yanayowahusu kilichoimbwa na Saida Ramadhani, Haya ni Mapenzi tu kibao kilichoimbwa na Zubeida Malicky, Bonge la Bwana kibao kilichoimbwa na Hashim Saidi.
Burudani hiyo ilianza mapema saa 2:00 usiku na kuendelea.

Mwisho.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni