Alhamisi, 4 Septemba 2014

WASAFIRI WA BASI LA AMANI EXPRESS WALALAMIKA BAADA YA KUSOTA NJIANI

Na: Violet John (DACICO)

Abiria waliokuwa wakisafiri jana na basi la Amani Express aina ya Scania lenye usajili namba T-846 BGU, lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Kahama, lilishindwa kuendelea na safari hiyo muda mfupi baada ya kuondoka katika Stand kuu za Ubungo jijini Dar ers Salaam kutokana na itilafu ya injini ya gari hiyo.
Wakizungumzia hali hiyo ya kuondoka tu stand kisha kushindwa kuendelea na safari kwa mwendo wa muda mfupi, abiria waliokuwa katika basi hilo walisema kuwa inashangaza kwa kuwa dereva na kondakta walitakiwa kufanya ukaguzi mapema ili kubaini tatizo kabla ya kuanza safari hiyo ambayo hata hivyo walisema ni ubabaishaji wa wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao wanapenda kupokea fedha bila kuwa na uhakika wa safari zao.
“naitwa juma Mussa mfanyabiasha katika Mkoa wa Kahama, na hapa nimebeba baadhi ya vifaa ambavyo ni kwa ajili ya wateja ambao waliniagiza na wanatakiwa kupata mizigo yao jioni na kama unavyoona sasa hali hii sidha ni tena kama safari hii itafanyika kama ilivyopangwa, maana kinachonishangaza hapa ni vipi hawa wahusika wameshindwa kutengeneza gari yao kabla ya kuchukua pesa zetu, magari yalikuwapo mengi ningeweza kupanda basi ingine, angalia ivi sasa wanasema kuwa watafute gari (basi) lingine ambalo linaelekea huko watupakize, huu unakuwa ni usumbufu kwa kweli” alisema Mussa Juma
Naye Kondakta wa basi hilo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa basi hilo lilishindwa kuendelea na safari yake kutokana na itilafu ya injini tatizo ambalo limeibuka baada ya kuwa wameanza safari hiyo ya kuelekea Kahama na iliwachukua muda mfupi katika safari hiyo kasha wakabaini kwamba tatizo lililopo ni kubwa ambalo ni la injini.
“Ni kweli kwamba tupo hapa gari imepata tatizo lakini hata hivyo tunajaribu kufanya utaratibu wa kuhakikisha kwamba abiria ambao ni wateja wetu wanapata usafiri mwingine wa kuwafikisha katika safari zao endapo tukibaini kwamba tatizo hili limeshindikana kutatuliwa kwa muda huu, maana tunalazimika kutafuta njia mbadala lakini pia abiria wanatakiwa kuwa na subira ili ni gari, alisemi wala hakuna aliyeweza kutambua wapi lilitakiwa marekebisho na ili utambue ubovu wa gari ni mpaka liharibike kwa hiyo wao wasubiri kwanza ikishindikana watapatiwa usafiri mwingine kwani tunajaribu kuomba msaada zaidi kutoka katika ofisi zetu za jijini Dar es Salaam”alisema kondakta wa basi hilo
Basi hilo lilishindwa kuendelea na safari hiyo majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi tu toka kuondoka katika stand kuu za Ubungo na ilipo fika maeneo ya Daraja la Kibamba kuelekea chama ndipo liliposhindwa kupanda kilima na kuwekwa pembeni kwa ajili ya utaratibu mwingine.
Aidha wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri wametakiwa kuwa waangalifu na wafuatiliaji wa karibu kwa watendaji wao kutatua matatizo yanayoweza kusababisha usumbufu kwa abiria na hata wakati mwingine ubovu wa basi unaweza kupelekea kusababisha ajali na kuleta maafa, hivyo wametakiwa kuchukua taadhali mapema kwa ajili ya kuboresha huduma zao.
Hata hivyo Abiria zaidi ya 40 waliokuwa katika basi hilo hatimaye waliweza kupandishwa kwenye mabasi mengine kwa awamu kwa ajili ya kuendelea na safari hiyo ambayo basi hilo lilishindwa kuendelea na safari na hivyo kulazimika kutafuta wataalamu kwa ajili ya kufika kulifanyia matengenezo.
Mwisho. 

Jumatatu, 1 Septemba 2014

NAWINA RESORT YATIKISIKA NA ASIYEKUJUA AKUTHAMINI WA MASHAUZI CLASSIC.

Na: Blanca Albert (DACICO)

Kundi Maarufu la Muziki wa Taarabu jijin I Dar es Salaam lijulikanalo kwa jina la Mashauzi Classic, mwishoni mwa juma siku ya jumamosi,  liliweza kuitikisa mbagala katika Ukumbi wa Kisasa Nawina Resort uliopo mbagala kuu na kukonga nyoyo za Mashabiki.
Safu yetu iliweza kuongea na meneja wa Bendi hiyo bwana Ismail Rashid “Suma Rager”kwa niaba ya Mkurugenzi wake Aisha Ramadhani maarufu kwa jina la Aisha Mashauzi, ambaye pia alisema kuwa aisha hakuwa katika hali nzuri Kiafya hivyo hakuweza kupatikana baada ya kumaliza onyesho hilo .

Suma Rager ambaye alizungumza kwa kirufu alisema kuwa malengo ya Bendi hiyo ni kuwapa ajira watu mbali mbali katika bendi hiyo kwa kuzingatia uwezo na ufanisi wa kazi ya kila mmoja.
Pia alisemam kuwa lengo linguine ni kuhakikisha kwamba bendi hiyo inafikia hatua ya kuwa na vitendea kazi vyake ambavyo vitasaidia kuifanya bendi hiyo kujiendeleza zaidi katika suala zima la muziki wa hapa nyumbani.

Akizungumzia historia yak undo hilo kwa ufupi alisema kuwa, ni hatua za kujivunia mpaka sasa kwa hatua waliofikia, kwani pamoja na kuwa na ushindani wa Miziki hiyo ya Mwambao, lakini wameshafanikiwa kuwateka baadhi ya mashabiki wa miziki hiyo kutokana na vibao vyao kuwa vya kuwaridhisha mashabiki wake.
Jumla ya wanamuziki 32 wanajumuhisha kundi hilo akiwamo kiongozi wa kundi ambaye pia ndiye mkurugenzi mkuu na mwimbaji nyota anayetikisa katika vibao mbali mbali ukiwemo wimbo mpya wa asiyekujua akuthamini ulioitikisa mbagala kuu Aisha Ramadhani maarufu kama aisha Mashauzi.
Akizungumzia nyimbo mpya zinazotarajiwa kutoka hivi karibuni suma rager alisema kuwa “Sura siyo Roho” wimbo huo unaimbwa na mwimbaji nyota Aisha Ramadhani, na kwamba wanatarajia kuzindua wimbo wa “Wema hauuzwi na Ubaya Haulipizwi” wimbo ambao unaimbwa na mwanamuziki Asia Khamis Mzinga.
Kuhusu changamoto wanazokutana nazo ni kubwa, lakini kwao hakuna changamoto hizo kutokana na hapo awali muziki wa taarabu ulikuwa kama starehe tofauti na miaka hii ya sasa ambapo muziki huo umekuwa ni biashara inayoingiza pato kubwa na kukidhi mahitaji ya wanamuziki ndani ya kundi hilo.
Kuhusu ratiba ya maonyesho ya burudani wana mashauzi, Suma rager alisema kuwa  siku za kupata burudani zao ni Jumanne, alhamisi na ijumaa ambapo siku ya alhamisi inakuwa ni siku mama ya kuwapa burudani mashabiki wa kinondoni katika ukumbi wa Mango Gardeni.
Aliitimisha kwa kusema kuwa, kabla ya uzinduzi wa nyimbo hizo Mashauzi Classic wameandaa shoo kubwa mashabiki wasubiri siku watakayotangaziwa na wameahidi kufanya onyesho kabambe kabla ya uzinduzi huo wa nyimbo zao mpya.

Safu hii pia ilipata fulsa ya kuzungumza na Mkurugenzi wa Nawina Resort, Bi, Mery Komba, ambaye alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa hatua aliyoweza kufikia katika kuandaa Burudani katika Ukumbi wa Nawina Resort “ Namshuru Mungu kwa kuwa ameweza kunisimamia katika kuandaa tamasha hili, kwa si kitu rahisi na wateja wangu waendelee kutegemea vitu vizuri zaidi kwani nawapenda wote, na napenda kuchukua fulsa hii kuwakaribisha wakazi wa mbagala na vitongoji vyake katika ukumbi wa Nawina Resort mbagala kuu, kwani tunaendelea kuwaandaliwa vitu vingi vizuri vitakavyozidi kuwapa raha”alisema mary Komba.

Aidha ukumbi huo ambao unapatikana katika Eneo la mbagala kwa sasa umeendelea kuwa gumzo kutokana na maboresho yaliyofanyika baada ya kupata ajali ya moto hivi karibuni.
Kutokana na hivyo umeweza kuboreshwa na kuwa na eneo pana kwa ajili ya usalama, eneo la maegesho Parking za magari, pikipiki na baiskeli.

Kuhusu suala la usumbufu kwa wateja kwa sasa katika ukumbi huo hakuna kwani wateja wanaendelea kupata huduma inayostahili ikiwa ni pamoja na vinywaji na Chakula.

“Natarajia kuendelea kuukarabati ukumbi huu wa Nawina Resort, na matarajio makubwa ni kuwawekea wakazi wa mbagala Ukumbi wa kisasa wenye hadhi ya kimataifa itakayowatikisha watu mbali mbali ususani vijana wa hiki yaani wapenda burudani, (NIGHT CLUB) itakayo kuwa pamoja na ukumbi”aliongeza Mary Komba.

 Hata hivyo aliowataka wapenzi wote wa Nawina kukaribia kila siku kupata vinywaji na chakula vinavyoandaliwa kwa kiwango cha hali ya juu ukilinganisha na maeneo mengine .

Vibao vingine vinavyoendelea kutikisa ndani ya Mashauzi ni pamoja na kibao cha ropokeni yanayowahusu kilichoimbwa na Saida Ramadhani, Haya ni Mapenzi tu kibao kilichoimbwa na Zubeida Malicky, Bonge la Bwana kibao kilichoimbwa na Hashim Saidi.
Burudani hiyo ilianza mapema saa 2:00 usiku na kuendelea.

Mwisho.
 

MASHAUZI CLASIC YAITIKISA- NAWINA RESORT MBAGALA KUU.

Na: Violet John.
(DACICO TANZANIA).

Wakazi wa Mbagala Kuu na Maeneo ya jirani, mwishoni mwa juma na mwishoni mwa mwezi huu Bendi ya Muziki wa Taarabu ,Mashauzi classic, chini yake, Aisha Mashauzi, siku ya juzi jumamosi tarehe 30/8/2014 katika Ukumbi wa Kisasa wa Nawina Resort uliopo Mbagala kuu  ilipowapa raha Mashabiki kwa kibao kipya cha Asiyekujua Akuthamini.
Mwimbaji nyota wa muziki wa Mwambao, Bi, Aisha Mashauzi, akipagawisha katika Ukumbi wa Nawina Resort.

Safu yetu ilipata kuongea
 na Meneja wa Mashauzi Classic Bw. Ismail Rashid (Suma Ragar) baada ya kushindwa kuzungumza na Aisha Mashauzi kutokana na hali yake kutokuwa nzuri.

Ismail Rashid alisema kuwa malengo makubwa ya bendi hiyo ni kuwapa watu ajira, kumiliki vitendea kazi, na kujiendeleza kimuziki .
Aidha pia alisema kwamba kwa sasa tayari wamekamilisha nyimbo kadhaa zinazotarajiwa kuingizwa hivi karibuni kwenye soko la muziki.
Nyimbo zinazotarajiwa kuingizwa sokoni ni pamoja na Sura siyo Roho, ulioimbwa na Isha Ramadhani, Wema hauuzwi na Ubaya haulipizwi, ulioimbwa na Asia Hamisi Mzinga.
Vile vile alisema kuwa katika bendi ya Mashauzi kuna waimbaji thelathini na mbili(32), ambao ni Isha Ramadhani ambaye pia ndiye mkurugenzi katika bendi hiyo , Rukia Juma ambaye  ni mama mzazi wa Isha, Hashimu Saidi, Zubeida Malicky,Abdulmali Shakani Malicky pamoja na Wengineo.

Mwimbaji nyota wa muziki wa Mwambao, Bi, Aisha Mashauzi, akipagawisha katika Ukumbi wa Nawina Resort.

“Na vile vile napenda kuwakumbusha mashabiki wetu kuwa kila alhamisi tunakuwa pale Mango Gareden Kinondoni kwa ajili ya kuwaburudisha mashabiki wetu kwa kiingilio cha shilingi elfu tano tu” alisema Suma.
Safu hii pia ilipata fulsa ya kuzungumza na Mkurugenzi wa Nawina Resort, Bi, Mery Komba, ambaye alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa hatua aliyoweza kufikia katika kuandaa Burudani katika Ukumbi wa Nawina Resort “ Namshuru Mungu kwa kuwa ameweza kunisimamia katika kuandaa tamasha hili, kwani si kitu rahisi na wateja wangu waendelee kutegemea vitu vizuri zaidi kwani nawapenda wote, na napenda kuchukua fulsa hii kuwakaribisha wakazi wa mbagala na vitongoji vyake katika ukumbi wa Nawina Resort mbagala kuu, kwani tunaendelea kuwaandaliwa vitu vingi vizuri vitakavyozidi kuwapa raha”alisema mary Komba.
Aidha ukumbi huo ambao unapatikana katika Eneo la mbagala kwa sasa umeendelea kuwa gumzo kutokana na maboresho yaliyofanyika baada ya kupata ajali ya moto hivi karibuni.
Kutokana na hivyo umeweza kuboreshwa na kuwa na eneo pana kwa ajili ya usalama, eneo la maegesho Parking za magari, pikipiki na baiskeli.
Kuhusu suala la usumbufu kwa wateja kwa sasa katika ukumbi huo hakuna kwani wateja wanaendelea kupata huduma inayostahili ikiwa ni pamoja na vinywaji na Chakula.
“Natarajia kuendelea kuukarabati ukumbi huu wa Nawina Resort, na matarajio makubwa ni kuwawekea wakazi wa mbagala Ukumbi wa kisasa wenye hadhi ya kimataifa itakayowatikisha watu mbali mbali ususani vijana wa hiki yaani wapenda burudani, (NIGHT CLUB) itakayo kuwa pamoja na ukumbi”aliongeza Mary Komba.
 Hata hivyo aliwataka wapenzi wote wa Nawina kukaribia kila siku kupata vinywaji na chakula vinavyoandaliwa kwa kiwango cha hali ya juu ukilinganisha na maeneo mengine .
Vibao vingine vinavyoendelea kutikisa ndani ya Mashauzi ni pamoja na kibao cha ropokeni yanayowahusu kilichoimbwa na Saida Ramadhani, Haya ni Mapenzi tu kibao kilichoimbwa na Zubeida Malicky, Bonge la Bwana kibao kilichoimbwa na Hashim Saidi.
Burudani hiyo ilianza mapema saa 2:00 usiku na kuendelea.

Mwisho

Alhamisi, 14 Agosti 2014

BONANZA LA DACICO KUMEKUCHA HAPO KESHO

Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala (DACICO TANZANIA) siku ya kesho kutakuwa na Bonanza la Maandalizi ya Tamasha la Vyuo vya Elimu ya Kati Tanzania( NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015), kwa ajili ya Vyuo vilivyopata Usajili wa Serikali yaani NACTE TANZANIA, hivyo michezo hiyo kwa Chuo cha DACICO ni Maandalizi ya kuhakikisha Dacico inaibuka kidedea katika Tamasha hilo Kubwa na la aina yake.
Akizungumzia Maandalizi ya Bonanza hilo Mkurugenzi wa DACICO, Mr. Idrisa Mziray, amesema kuwa, lengo kubwa la DACICO kuweka Bonanza kwa ajili ya kushiriki Michezo katika ya Walimu na Wanafunzi, ni kutaka kupata kikosi cha Timu zitakazoshiriki wakati wa michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika 21-23/11/2014.
"sisi lengo kama unavyofahamu, ni kuhakikisha tutafanya Vizuri wakati wa michezo yetu, maana kumbuka kuwa katika Tamasha hilo la Vyuo vya Elimu ya Kati, ni kwa Mara ya Kwanza, hivyo kila Chuo kitataka kufanya vyema ili kujijengea heshima wakati wa Michuano katika Mwaka Mwingine, lakini Pia kupata zawadi, ikiwa ni pamoja na kujitangaza zaidi, maana sidhani kama Chuo kitakachofanya vibaya kwenye michuano hiyo, kupata sifa nzuri ama kujitangaza zaidi, maana kulingana na Waandaaji wa Tamasha hilo, Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, kwenye michezo hiyo mfumo uliotumika ni Mtowano, hivyo itakuwa ni jambo la kushangaza tutakapotupwa nje katika hatua za Mwanzo za Tamasha hilo, kwa niaba ya Chuo Changu cha DACICO, napenda kuwatangazia wachezaji wote wa DACICO kufika Mara Moja Chuoni kwa ajili ya kukamilisha Maandalizi haya na pia kuvitaka vyuo Vingine kuthibitisha Ushiriki wao Mapema, Wasiogope kuleta timu zao kwa kutuogopa sisi pamoja na kwamba Timu ya Dacico inasifika kwa kutoa Dozi kwa Timu za Vyuo Vingine lakini katika hilo Tamasha la NACTE, lolote laweza kutokea kutokana na Timu za Vyuo vyote hivi sasa kuwa kwenye Maandalizi Makali, kikubwa tu ni kuwasisitiza Wanamichezo wa Vyuo Vingine kuhakikisha kwamba wachezaji, Wanafunzi, na Mashabiki wao wanakuwa Watulivu wakati wote wa Mashindano" amesema Mziray
Bonanza hilo hapo kesho linatazamiwa kuanza mapema majira ya saa mbili asubuhi ambapo kocha wa timu ya Dacico Walimu Sir- Henry amejigamba kuibuka na ushindi mnono dhidi ya timu ya wanafunzi, lakini wakati huo huo akiwataka Wachezaji wa Timu ya Wanafunzi, kucheza Mchezo wa Utulivu ili kuhepuka kuwaumiza walimu ambao kwa Muda Mwingi wamefanya Maandalizi yao kwenye Vitabu kutokana na kuwa na Majukumu Mengi ya Ufundishaji wa Masomo kwa Wanafunzi.

MPAKA MUDA HUU KIKOSI CHA TIMU YA WANAFUNZI BADO KIMEFICHWA LAKIMNI KIKOSI CHA TIMU YA WALIMU TAYARI KIMEBAINISHWA, NA WALIMU WAMEJIGAMBA KUWAFUNGA TIMU INAYOUNDWA NA WANAFUNZI.

NA HIKI NDICHO KIKOSI KAMILI CHA TIMU YA WALIMU WA DACICO.
1, Idrisa Mziray
2, Sir- Masawe
3, Sir Malima
4, Sir Mpalule
5, Sir Mpoto
6, Mr. Ombeni
7, Sir Kelvini
8, Mr. Sam
9, Sir Michael Jackison
10, Sir Michael Jeremia
11, Sir Kasilima
Wachezaji wa Akiba ni
Mr. Cholo
Sir. Kisima
Sir. Kazimoto
Kocha Mkuu HENRY
Hawa ni Baadhi ya Washiriki wa Michezo mbali mbali kwa Upande wa Timu za Wanawake wa Chuo cha DACICO.

Na kwa Upande wa Timu ya Wanawake watakaoshiriki katika mchezo wa Netball ni Pamoja na Wachezaji
1. Doris Mchome,
2. Alice
3. Lucy
4. Veronica
5. Mwanahawa
6. Monica
  www.missdemocrasiatz.com
7.Violet
8. Laura Solima
9. Felister
10. Pepetua Luguga
11. Neema
12. Anthonia
13. Farida
14, Kalister
15, Victoria Godwin
======================================================
Baada ya michezo ya Timu za wenyewe kwa wenyewe DACICO Walimu na DACICO Wanafunzi, utafuata mpambano wa Timu ya K.E.C ya Shirika la Elimu Kibaha(Njuweni).
unaweza pia kufuatilia michezo ya Bonanza hilo la Maandalizi ya Tamasha la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015.
Wanafunzi Wote wa DACICO mnakaribishwa sana.
kwa habari zaidi bofya hapa. www.daressalaamcitycollege.blogspot.com
www.missdemokrasia.blogspot.com

Jumatatu, 4 Agosti 2014

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha DACICO TANZANIA, wakifuatilia Kozi work zao kwa Mwalimu Michael Jackison, wakati huu wa maandalizi ya Mitihani

 
Mwalimu Michael Jackison(kushoto) akifafanua jambo kwa wanafunzi wa masomo ya Uandishi wa Habari, Makao Makuu ya Chuo Jijini Dar es Salaam.(Picha Zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).

WANAFUNZI WA INTAKE JANUARY, APRIL, NA SEPTEMBER- DACICO WAANZA MITIHANI

 

























 
Kati ya wanafunzi hawa wengine wanamaliza masomo yao lakini pia wengine wanafanya  mitihani ya kufunga muhula wa kwanza, mitihani hii ni kwa ajili ya wanafunzi wa Vyuo vyote vya DACICO TANZANIA.