Posted: 14 May 2013 10:39 PM PDT
Na Mwandishi Wetu, Moshi
MJUMBE
wa Kamati Kuu ya Halmashauri K u u y a Ta i f a , (NEC) wa Chama Cha
Mapinduzi, (CCM), Bw. Jerry Silaa, amesema kukosoana miongoni mwa
viongozi ndani ya CCM na Serikali ni njia mojawapo ya kukiimarisha chama
hicho na isitafsiriwe vingine.
Bw.
Silaa ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Jijini
Dar es Salaam, aliyasema hayo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, wakati wa
hafla ya kuwapokea wanachama wapya 155 wa CCM wa tawi la CCM la Chuo
Kikuu cha Ushirika na Biashara, cha mjini Moshi, (MUCCoBS).
"Ni vyema tukajenga tabia ya kukosoana pale tunapoona
mwenzetu au wenzetu wamepotoka katika kutekeleza ilani ya chama chetu
la sivyo ahadi zetu kwa wananchi na malengo ya ilani yetu ya miaka
mitano hayatatimia," alisema na kuongeza kuwa makosa anayoyafanya mtu
yawe ni ya kwake na kuwajibika nayona si chama wala serikali.
Bw.
S i l a a a l i s ema pia haitakuwa vyema k u w a c h u k u l i a w a l
e wanaojitolea kukikosoa chama au serikali kama wasaliti na kwamba kwa
kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kubariki mabaya ambayo yanakemewa.
"Wanaokosoa
mapungufu katika utekelezaji wa ilani yetu wasionekane kuwa ni wasaliti
kwa kuwa kwa kufanya hivyo tutakiangamiza chama chetu ambacho bado watu
wana imani nacho," alionya.
Alitoa
mwito kwa viongozi wa CCM MUCCoBS , kuungana na wale wa Umoja wa Vijana
wa CCM, (UVCCM), Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wenzao wa mikoa mingine
ili kuangalia uwezekano wa k uwa s i l i s h a k e r o zinazohusiana na
mapungufu yaliyoko katika bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa taasisi za
elimu ya juu na changamoto zake ili kuzitafutia ufumbuzi.
Awali katika risala yake, kaimu katibu wa CCM MUCCoBS, Bw. David Warioba, alisema kuwa moja
inayowakabili
wanafunzi ni mikopo kwa ajili ya wanafunzi hasa wale wa diploma ambao
wanataka kuendelea na mafunzo katika ngazi ya shahada.
"Kuna
wanafunzi zaidi ya 700 wa ngazi ya diploma hapa MUCCoBS ambao
wangependa kuendelea katika ngazi ya shahada, lakini wanashindwa
kutokana na serikali kupitia bodi ya mikopo kutoa kipaumbele kwa wale
waliotokea kidato cha sita," alisema.
Aidha
alitoa wito kwa CCM kupitia Serikali yake kuwachukulia hatua wale wote
wanaotumia dhamana waliyopewa kujinufaisha wenyewe jambo ambalo alisema
limechangia watu kuinyooshea serikali kidole pamoja na mambo mazuri
ambayo imeyafanya na inayoendelea kuyafanya.
Kwa
u p a n d e wa k e Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro, Bw.
Frederick Mushi, alitoa wito kwa CCM na serikali yake kuwatumia wasomi
katika kutekeleza ilani yake.
|
Posted: 14 May 2013 10:34 PM PDT
Na Rehema Mohamed
KIONGOZI
wa muda mr e f u s e r i k a l i n i n a m t a a l a m u a n a y e t a m
b u l i k a kitaifa na kimataifa katika masuala ya uwekezaji, Bw.
Emmanuel Ole Naiko, ameteuliwa kuwa balozi wa heshima wa Botswana nchini
Tanzania, ambapo makao yake yatakuwa jijini Dar es Salaam.
Akitangazwa
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard
Membe, jijini Dar es Salaam, juzi Bw. Naiko, aliishukuru serikali ya
Botswana chini ya uongozi wa Rais Ian Khama na Waziri wa Mambo ya Nje na
Mahusiano ya Kimataifa, Bw. Phandu T.C Skelemani, kwa kumteua kuwa
mwakilishi wao hapa Tanzania.
"Naamini ni Mwenyezi Mungu aliyewaongoza na
mimi
napenda kuwahakikishia kwamba sitawaangusha. Nitawawakilisha kwa
ukamilifu wote ulio ndani ya uwezo wangu," alisema Bw. Naiko.
Bw.
Naiko alimshukuru Waziri Membe kwa kukubali kumkabidhi dhamana hiyo
kubwa. "Wewe ni ndugu na rafiki yangu wa muda mrefu naamini uliona ni
vyema ukanipa heshima hii wewe mwenyewe," alisema.
Alisema
Botswana ina vivutio vingi vya uwekezaji kama Tanzania na kuwa
Watanzania na jumuiya y a Af r i k a Ma s h a r i k i wanakaribishwa
kuwekeza katika nchi hiyo.
"Nadhani wakati umefika Botswana nayo kupata wawekezaji kutoka Tanzania kama wao walivyowekeza Mlimani City," alisema.
Nc
h i y a B o t swa n a imepakana na nchi za Afrika ya Kusini, Zimbabwe,
Namibia na Zambia. Ina ukubwa wa sq km 58,2000, wakazi milioni 2.
Ni nchi iliyo na amani na utulivu toka uhuru na ina kiwango kidogo sana cha rushwa barani Afrika.
Nchi
hiyo imedhamiria kuongoza katika sekta za fedha, madini hasa uranium,
shaba na usafirishaji wa almasi na copper na pia kuendeleza uwekezaji
katika sekta ya utalii kwani Botswana ina mbuga nyingi za wanyama na
hasa Vistoria Falls ambayo iko mpakani na Zimbabwe na Zambia katika mji
wa Kasane.
"Watanzania walioko huko wameanzisha chama chao na mimi nilikutana nao nilipokuwa TIC," alisema.
Kodi
ya mapato katika nchi hiyo ni asilimia 22; VAT ni asilimia 12 na pia
kuna msamaha wa kodi kwa wawekezaji ni kati ya miaka mitano mpaka 10.
|
Posted: 14 May 2013 10:31 PM PDT
Na Reuben Kagaruki
BAADHI
ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamepinga vikali hoja iliyoanzia
bungeni wiki iliyopita kwamba kinywaji cha Konyagi aina ya Kiroba
kipigwe marufuku nchini na wameonya kuwa uamuzi huo ukifikiwa watahamia
kunywa gongo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wananchi hao, walisema endapo serikali itachukua
uamuzi wa kupiga marufuku kinywaji hicho, itakuwa haijawatendea haki
walalahoi, kwani ndiyo wanywaji wakubwa.
Mkazi wa Ukonga Mombasa, wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, alisema
Serikali isipige marufuku kinywaji hicho kwani ndiyo mkombozi wao.
"Tukikubali
hilo tutakuwa kama Zambia ambayo ilizuia viroba, lakini nchi nzima
imejaa viroba vya Malawi, Zaire na Burundi, lazima tuiadhibu serikali
ikose kodi kote kote, bia hatunywi, viroba vya nje tutakunywa, pamoja na
gongo,"alisema.
Alisema
haiingii akilini kukihusisha kinywaji hicho na ajali za magari.
Alifafanua kwamba hata kabla ya viroba kuingia sokoni ajali zilikuwepo
nyingi.
"Sisi
tuna imani na viroba kwa vile vina ubora wa uhakika tofauti na pombe ya
gongo ambayo inapikwa bila kupimwa ubora hivyo ni hatari kwa usalama wa
afya zetu," alisema Mwiruka.
Kwa
upande wake, Bw. John Kamugisha, mkazi wa Chanika, alisema, wanaotaka
viroba vipigwe marufuku hawawatendei haki wananchi wa kawaida ambao kwa
asilimia kubwa hawana uwezo wa kununua bia ambazo bei yake ni kubwa.
"Siku
hizi wananchi wengi wamehamia kwenye makambi ya jeshi ambapo bia
zinauzwa bei nafuu na wengine wanakunywa viroba kwa sababu vinauzwa bei
nzuri, wananchi hao wakibugudhiwa watahamia kwenye gongo," alisema.
Wakazi
wengi waliohojiwa walisema kuwa jambo hilo inawezekana ikawa njama za
wafanyabiashara kutoka nchi jirani ambao hawaitakii mema Tanzania kwa
kuwa pombe hiyo kuwepo kwake pia kunakuza pato la Taifa.
Naye,
Bw. Mwesigwa Joas alisema hapendi viroba ni pombe ya wanyonge hivyo
aliwataka wabunge kuthamini kinywaji hicho na bidhaa inayozalishwa na
wazawa.
"Huwezi
ukahusisha viroba na pikipiki, kwani nchi hii ina pikipiki nyingi na
watu milioni 43, uhusiano wake uko wapi, kwanza hata leseni hamuwapi?"
alisema.
Watu walitoa maoni hayo baada ya kuona kinywaji chao cha kiroba kinapigwa vita kupitia vyombo vya habari.
Inadaiwa
kuwa kampeni inayoendeshwa na kampuni zenye uhusiano na kampuni kubwa
ya pombe duniani yasiyopenda, nchi za Afrika zizalishe pombe zake, bali
ziendelee kununua kutoka Ireland, Kenya na Uingereza.
Akizungumza
na waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki hii, Mkurungenzi Mkuu wa
Konyagi, Bw. David Mgwassa, alisema kuwa kwa kipindi kirefu kumekuwa na
mchezo mchafu wa kuharibiana jina kampuni yake sokoni kwa kutumia baadhi
ya vyombo vya habari vya hapa nc
|
Posted: 14 May 2013 10:15 PM PDT
Na Goodluck Hongo
JUKWAA
la Katiba nchini, linakusudia kufungua kesi ili kuiomba mahakama
isitishe mchakato wa Katiba Mpya hadi Tume ya Mabadiliko ya Katiba na
wadau wakubaliane mambo ya msingi ndipo mchakato huo uendelee.
Lengo la jukwaa hilo ni kutafuta haki za Watanzania ili waweze kupata Katiba Mpya waitakayo si vinginevyo.
Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Bw. Deus Kibamba aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na
waandishi wa habari akidai mchakato huo una kasoro nyingi.
Alisema
hoja walizoamua kuziweka bayana ni mchakato huo ambao unaendelea
kushindwa kurekebisha makosa ya miaka iliyopita katika kuandika Katiba
ambayo ni uelewa, hamasa na ushiriki duni wa wananchi katika mchakato wa
Katiba yao.
Aliongeza
kuwa, jukwaa hilo limeunda timu ya mawakili 10 wakiongozwa na
Mwanasheria maarufu wa masuala ya Haki za Binadamu, Dkt. Rugemeleza
Nshala.
“Hivi
sasa tunaandaa hoja mu h imu z a k u z iwa k i l i s h a mahakamani
ndani ya siku saba zijazo, tunawaomba Watanzania watuelewe kuwa
tunakwenda mahakamani si kuvuruga mchakato huu bali kuurekebisha.
“Mchakato
huu umeshindwa kurekebisha makosa ya miaka ya nyuma hivyo Katiba
itakayopatikana inaweza kuwa mbaya zaidi kuliko hii tuliyonayo kwa
kuligawa Taifa,” alisema.
Alisema
sababu nyingine ya kwenda mahakamani ni juhudi walizozifanya kutaka
kuonana na Waziri wa Katiba na Sheria zaidi ya mara moja ili wazungumze
naye kuhusu suala hilo pamoja na kumuona Rais Jakaya Kikwete
kushindikana.
Bw.
Kibamba alisema ahadi alizotoa Rais Kikwete kuhusu mchakato huo
hazioneshi dalili ya kutekelezwa kutokana na tume kusuasua katika
utekelezwaji wake.
“Awali
tume ilipoteuliwa, wananchi walikuwa na imani nayo kutokana na watu
waliopewa dhamana hiyo...mwanzo walipewa sh. bilioni nane na mwaka 2012
walitengewa sh. bilioni 34, pesa hizi wanapewa wao lakini bado
wanachelewa kutoa rasimu yake.
“Tunaitaka
Serikali ifungue ma s i k i o kwa k u t e k e l e z a makubaliano
waliyoafikiana na vyama vya siasa...Uchaguzi wa Mabaraza ya Katiba
umevurugwa na tume kwa makusudi kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi
(CCM),” alisema.
Aliongeza
kuwa, chama hicho kilitoa fomu za kugombea nafasi hiyo wakati kazi hiyo
ni ya tume hivyo ni wazi kuwa mchakato huo ukiendelea, katiba ijayo
itakuwa ya CCM si ya Watanzania.
Alisema
kwa sasa mchakato huo hauna uongozi na mwelekeo madhubuti kutokana na
wananchi wengi walitoa malalamiko ya kuvurugwa kwa uchaguzi wa Wajumbe
wa Mabaraza ngazi ya Kata na Wilaya, kutosikilizwa.
Bw. Kibamba alisema baada ya kufungua kesi hiyo, jukwaa hilo halitazungumzia mchakato huo wakisubiri uamuzi wa mahakama
|
Posted: 14 May 2013 10:12 PM PDT
Na Esther Macha, Mbeya
VIBARUA
watatu wa kampuni inayojenga barabara ya China Communication and
Construction Company (CCCC), mkoani Mbeya, wamefariki dunia kwenye ajali
ya gari baada ya lori walilopanda likitoka kuchukua kifusi kupinduka.
Kamanda
wa Polisi mkoani humo, Diwani Athuman, alisema tukio hilo limetokea
jana saa sita mchana katika eneo la Iganzo, maarufu kama Mwisho wa Lami,
barabara ya Mbeya-Chunya.
Alisema gari hilo lenye namba T 405 BWA aina ya
Zhongji mali ya kampuni hiyo, lilikuwa likitoka kuchukua kifusi katika
eneo la Kawetele, ambapo dereva aliyesababisha vifo hivyo jina lake
halikufahamika mara moja baada ya kukimbia.
Aliongeza
kuwa, lori hilo lilipinduka baada ya dereva huyo kushindwa kulimudu
kutokana na mwendo kasi katika eneo lenye kona na mteremko mkali.
Hata
hivyo Kamanda Athuman alisema marehemu wote ambao miili yao
imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani humo, bado
hawajatambuliwa.
Alisema
katika ajali hiyo kulikuwa na majeruhi watano kati yao watatu
walitibiwa hospitali na kuruhusiwa, wawili wamelazwa katika hospitali
hiyo.
Aliwataja
majeruhi wanaoendelea na matibabu kuwa ni msimamizi wa vibarua hao raia
wa China, Don Fung Cheng (38), aliyejeruhiwa kichwani, pamoja na mtu
mwingine ambaye hajafahamika jina kutokana na hali yake kuwa mbaya.
Waliotibiwa na kuruhusiwa ni Ayoub Samson (25), Jelicko Apton(18) na Natifa Ngole (23), wote wakazi wa Mkoa huo.
|
Posted: 14 May 2013 10:11 PM PDT
Na Heri Shaaban
WATOTO
5,000 wenye umri wa miaka 10 kushuka chini, wanatumia dawa za kupunguza
makali ya virusi vya UKIMWI (ARVs), katika Hospitali ya Amana, Dar es
Salaam.
Mbali ya watoto hao, watu wazima 11,000 nao wameanza kutumia dawa hizo katika kliniki iliyopo hospitalini hapo.
Daktari
wa Kitengo cha Kuratibu Wagonjwa wa UKIMWI, Shani Mwaruka, aliyasema
hayo wakati kamati ya kudhibiti ugonjwa huo Manispaa ya Ilala,
ilipofanya ziara katika hospitali hiyo.
Alisema kwa siku kliniki hiyo uhudumia wagonjwa 250 hadi
300 ambao wanatoka kwenye maeneo mbalimbali na kudai kuwa, changamoto
waliyonayo ni baadhi ya wagonjwa kutokubaliana na hali waliyonayo pamoja
na uchache wa vitendea kazi.
“Watu
wengi hawakubaliani na hali waliyonayo, baba anapokuja kupima afya yake
anamficha mkewe na kuanza kutumia dawa peke yake na wanawake pia hivyo
hivyo,” alisema Dkt. Mwaruka.
Aliongeza kuwa, kitengo hicho kinafanya jitihada za kuhakikisha wazazi wanawaeleza watoto wanaotumia dawa hizo wanapokua.
Kwa
upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Said Kitambuliyo,
alisema lengo lao ni kutembelea mitandao yote na asasi za watu waishio
na ugonjwa huo, kusikiliza changamoto walizonazo na kuangalia kazi
wanazofanya.
|
Posted: 14 May 2013 10:08 PM PDT
Na Mwandishi Wetu
KAMATI
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua
Mattar Sarahan Said, kuwa mgombea wake wa chama hicho katika Jimbo la
Chambani, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba.
Uamuzi
huo umefikiwa kwenye kikao cha siku moja kilichofanyika mjini Dodoma
jana chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.
Pia
chama hicho kimewateua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Balozi Seif Idd na
Mwenyekiti mstaafu wa CCM ambaye pia ni Rais mstaafu wa awamu ya pili,
Mzee Ali Hassan Mwinyi, kufunga kampeni hizo.
|
Posted: 14 May 2013 10:00 PM PDT
Na Suleiman Abeid, Kahama
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mk o a n i S h i n y a n g a , Khamis
Mgeja amekataa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya
chama hicho iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya kwa
madai imeandikwa ovyo na kwa dharau.
Mbali
ya kukataa kupokea taarifa hiyo, Mgeja alilaani kitendo kilichooneshwa
na mkuu huyo wa wilaya baada ya kubainika kuwa taarifa aliyopelekewa
iliwahi kukataliwa pia hivi karibuni na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilayani Kahama.
Hata
hivyo, kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo, Mpesya alikanusha kufanya
dharau kwa chama chake na kwamba yeye anawajibika kwa Katibu wa CCM
wilayani Kahama na siyo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa na iwapo taarifa hiyo
ilikuwa na mapungufu basi ndivyo ilivyoandaliwa na watendaji wake wa
CCM.
“Nikiri
ni kweli taarifa hiyo mimi ndiye niliyeipeleka kwa katibu wa CCM wa
wilaya ambaye ndiye ninayewajibika kwake na siyo kwa mwenyekiti wa CCM
wa mkoa, aliyepaswa kuipeleka kwake ni katibu wake wa CCM siyo mimi
hivyo makombora niliyorushiwa yalistahili kuelekezwa kwa katibu huyo,”
alieleza Mpesya.
Akizungumza
na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Malunga wakiwemo wanachama
na viongozi wengine juzi, Mgeja alisema CCM haitokubali vitendo vya
kipuuzi vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wa serikali.
“Nimesikitishwa
sana na kitendo cha mkuu wa wilaya, niliomba nipatiwe taarifa ya
utekelezaji wa ilani yetu ya uchaguzi upande wa utoaji mikopo kwa
vikundi vya vijana na wanawake, lakini nilicholetewa kimenishangaza,
kinaonesha wazi mwenzetu huyu anatudharau viongozi wa chama,”
“Taarifa
aliyoandika haiwezi kuandikwa hata na DC (mkuu wa wilaya) anayejifunza
kazi, sijui mwenzetu huyu kiburi hiki anakipata wapi, nimeikataa na
ninaomba iandikwe nyingine ikiwa na uchambuzi kamili kuonesha jinsi gani
vijana na wanawake wamesaidiwa kupitia asilimia 10 ya mapato ya
halmashauri,” alisema Mgeja.
Mgeja
aliwataka watendaji wote wa serikali mkoani Shinyanga kuhakikisha
hawafanyi vitendo ambavyo vitasababisha wananchi wakichukie chama chao
hivyo kusababisha mpasuko wakati wa uchaguzi.
Kutokana
na hali hiyo Mgeja aliahidi kupeleka nakala ya taarifa hiyo makao makuu
ya chama na kwa Mwenyekiti wake wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete, Waziri
Mkuu Mizengo Pinda pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga ili
waweze kuona wenyewe madudu yanayofanywa na watendaji wa chini yao.
Hata
hivyo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Isaka aliyekaribishwa katika kikao
hicho, Gavana Ally alishauri vikundi vyote vya vijana na wanawake
wilayani humo kuandaa taarifa zao mapema zikionesha misaada au mikopo
yote waliyokwishapokea kutoka halmashauri ili ilinganishwe na ile
itakayoandikwa upya na mkuu huyo wa wilaya.
|
Posted: 14 May 2013 09:58 PM PDT
Na Rehema Mohamed
WALIOKUWA
wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ma z i n g i r a ( N EMC )
wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa
tuhuma za kushawishi rushwa ya sh.milioni 6.
Washtakiwa hao ni Jerome Kayombo (33) na Milton Mponda (32).
Mbele ya Hakimu Gane Dudu, wakili wa serikali kutoka Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kelvin Murusuri alidai kuwa
washtakiwa hao walitenda kosa hilo kati ya Mei 4 na 5, 2012 katika
Kiwanda cha Kamal Steels eneo la Chang'ombe.
Alidai
kuwa, washtakiwa hao wakiwa kama maofisa ma z i n g i r a wa NEMC
walishawishi wapewe rushwa ya sh. milioni 6 kutoka kwa Mkurugenzi wa
kiwanda hicho, Sammer Gupta ili iwe k ama k i s h awi s h i kwa
Mkurugenzi huyo asiadhibiwe kwa kukiuka sheria ya utunzaji mazingira.
Hata
hivyo washtakiwa hao walikana kutenda makosa hayo ambapo upande wa
mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.
A i d h a , k e s i h i y o imeahirishwa hadi Mei 23, mwaka huu itakaposikilizwa.
Washtakiwa
wote wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na
mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya sh. milioni 5 kila mmoja.
|
Posted: 14 May 2013 09:53 PM PDT
Na Darlin Said
kAMPUNI
za kufua umeme kutoka nchini Sweden, zipo katika mchakato wa kuzalisha
umeme kwenye vyanzo mbalimbali baada ya Shirika la Umeme nchini
(TANESCO), kutokidhi hitaji la kutoa huduma hiyo kwa wananchi wengi.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliyasema hayo Dar es
Salaam jana wakati akiwakaribisha wawekezaji hao na kuongeza kuwa, lengo
la Serikali ni
kuiboresha TANESCO ili iweze kutoa huduma bora.
Alisema
tangu kuanzishwa kwa shirika hilo mwaka 1961 ni asilimia 21 tu ya
Watanzania waliopo mijini na asilimia saba waliopo vijijini ambao ndiyo
wanaopata huduma ya umeme.
“Kimsingi
hali hii inasikitisha, tumegundua kuwa TANESCO peke yao hawawezi kutoa
huduma ya umeme kwa Watanzania wenye hitaji hilo hivyo wataendelea
kuumia,” alisema.
Prof.
Muhongo aliongeza kuwa, Serikali imewakaribisha wawekezaji hao kwa
sababu haina fedha za kuwekeza katika sekta ya nishati ili kusambaza
huduma ya umeme.
“Pato
la Taifa ni dola za Marekani bilioni 28 ambazo tukizigawa, kila
Mtanzania atapata sh. 6,000 hivyo lazima tutegemee wawekezaji ili tuweze
kujikomboa,” alisema.
Alisema
wawekezaji hao mbali ya kufua umeme nchini, pia watatekeleza miradi
mbalimbali, k u b o r e s h a mi u n d omb i n u , kusambaza umeme
vijijini na kupunguza upotevu wa umeme.
Aliongeza
kuwa, vyanzo vyote vya umeme nchini vingeweza kuzalisha umeme wa
megawati 1,438.24 lakini miundombinu iliyopo hata kama umeme huo
ungezalishwa, wangeshindwa kuusambaza kutokana na ubovu wa miundombinu
ambao hupoteza asilimia 23.4 ya umeme.
Alisema
kampuni hizo zitafua umeme kupitia upepo, miamba, kinyesi cha wanyama,
maji, jua na kusisitiza kuwa ni ndoto ya mchana kuitegemea TANESCO
izalishe umeme kupitia vyanzo hivyo.
Kwa
upande wake, Balozi wa Sweden nchini, Bw. Gunnar Oom, alisema wameamua
kuwekeza Tanzania baada ya kuona misaada pekee wanayotoa haiwezi
kuongeza
kasi ya maendeleo.
Alisema kupitia uwekezaji huo, utasaidia kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kiuchumi pamoja na kubadilishana uzoefu.
“Kupitia
uwekezaji huu, pia utasaidia kubadilishana bidhaa kwa kununua zilizopo
Tanzania kwani nchi nyingi za Afrika zinategemea sana kuuza mafuta,
madini na mazao ya chakula nje,” alisema.
|
Posted: 14 May 2013 09:42 PM PDT
David John na Neema Malley
CHAMA
cha Wananchi (CUF), kimeitaka Serikali itoe tamko la kuiomba radhi
Serikali ya Saudi Arabia kutokana na raia wake wanne kuhusishwa na tukio
la ulipuaji bomu mkoani Arusha na baadaye kuachiwa baada ya uchunguzi
kubaini hawakuhusika.
Tukio
hilo lililotokea Mei 5 mwaka huu, katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu
Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, mkoani humo ambapo watu watatu
walifariki dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.
Mwenyekiti wa chama hicho Taifa,
Prodesa Ibrahim Lipumba, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati
akifungua Kikao cha Baraza Kuu la chama hicho na kuongeza kuwa, kwa muda
mrefu Saudi Arabia na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri hivyo ni
wajibu wa Serikali kuomba radhi ili kuendeleza uhusiano huo.
Alisema
wageni hao waliingia nchini kihalali hivyo kitendo cha kuhusishwa na
tukio hilo ambalo limetangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari
kimechafua jina la nchi yao.
“Serikali
inapaswa kuwa makini na inachokifanya, kitendo cha kuwakamata wageni
hawa ambao wanatoka kwenye nchi ya Kiislamu, kinaweza kuwagawa Waislamu
na Wakristo kitu ambacho ni hatari kwa Taifa,” alisema.
Aliongeza
kuwa, Serikali inatakiwa kuchukua hatua stahiki yanapotokea matukio
makubwa kama hilo la uvunjifu wa amani ili kuwajengea imani Watanzania
kuwa Serikali yao ipo makini.
Katika
hatua nyingine, Prof. Lipumba alizungumzia uamuzi wa Mahakama ya
Kisutu, Dar es Salaam, kumuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda.
Alisema
kilichofanywa kwa kiongozi huyo si cha kiungwana kwani kesi iliyokuwa
ikimkabili ilikuwa ikihusu kiwanja hivyo ingehamishiwa kwenye Mahakama
ya Ardhi.
“Serikali
imekuwa ikikuza mambo na kusababisha mifarakano katika jamii...inapaswa
kufanya uchunguzi wa kina kwanza kwani mwisho wa siku nchi itaingia
katika matatizo,” alisema.
Pia
Prof. Lipumba alidai kuhofia deni kubwa la Taifa na kudai kuwa ili
kuondokana na madeni ya aina hiyo, Serikali inapaswa kuacha tabia ya
kukopa bila utaratibu kwani mwisho wa siku tutashuhudia Taifa likipata
mzigo wa kurejesha madeni hayo.
Aliongeza
kuwa, kipindi cha utawala wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw.
Benjamin Mkapa, wakati akiingia madarakani alikuta Taifa likiwa na deni
kubwa hivyo alitumia kipindi cha miaka mitano kulipunguza sana.
Alisema
pamoja na nchi kuwa na rasilimali za kutosha katika Taifa, bado
utegemezi umekuwa mkubwa na Serikali imekuwa bingwa wa kutoa ahadi zakutekeleza miradi mbalimbali.
|
Posted: 14 May 2013 09:38 PM PDT
Na Derick Milton, Simiyu
MKUU
wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti amewataka wanasiasa mkoani humo
kuacha mara moja tabia za kuwadanganya au kuwapotosha wananchi kuhusu
kilimo cha mkataba hususani zao la pamba.
Alisema, yeyote ambaye ataenda kinyume na agizo hilo atakamatwa ili kufikishwa
mahakamani, sheria ichukue mkondo wake.
Hayo
aliyasema jana ofisini kwake mjini Bariadi wakati akizungumza na
waandishi wa habari ambapo alikuwa anazungumzia juu ya zao la pamba
msimu huu.
Alisema
kuwa, katika msimu uliopita wa zao hilo baadhi ya wanasiasa walipita
kwa wakulima kuhamasisha wakatae kilimo cha mkataba kwa madai wakijiunga
watanyang'anywa mashamba yao na wafanyabiashara.
Mkuu
huyo alisema, baada ya wakulima kuambiwa hivyo na wanasiasa hao
waliokuwa wame j i u n g a wa l i a n z i s h a mgogoro mkubwa kati yao
na wafanyabiashara hadi kusitishwa kwa kilimo hicho.
Kutokana
na hali hiyo, Mabiti aliamua kupiga marufuku kwa mwanasiasa yeyote
atakayebainika anapinga kilimo cha mkataba kwa msimu ujao kuwa
atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na
kufikishwa mahakamani.
Alibainisha
kuwa, hali ya zao la pamba kwa msimu huu ni mbaya katika uzalishaji
wake kuwa mdogo, na kutaja sababu kuwa ni kusitishwa kwa kilimo cha
mkataba baada ya kuwepo mgongano baina ya wahusika katika kilimo hicho.
Pia
alisema, kwa sasa serikali pamoja na wadau wengine wa zao la pamba
wakiwemo wafanyabiashara wanafanya utaratibu wa haraka na ambao utakuwa
ni mzuri kuhakikisha kilimo hicho kinarudi ili kumkomboa mkulima.
“Katika
utaratibu utakaowekwa hivi karibuni, mtu yeyeyote ambaye ni mwanasiasa
atakayeonekana na kubainika anapinga kilimo hicho sitamuonea huruma,
nitamkamata na kumchukulia hatua za kisheria labda aongelee nje ya mkoa
wangu,”alisema Mabiti.
Alibainisha
kuwa, wanasiasa hao wamekuwa wakifanya hivyo kwa maslahi yao binafsi na
kusababisha wananchi wengi hasa wakulima kubaki maskini na hata bila
kutoa msaada wowote kwa watu hao.
|
Posted: 14 May 2013 09:25 PM PDT
Na Ester Maongezi Wanafunzi
wa kike 32 wanaosoma katika Shule ya Sekondari Manzese, iliyopo
Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, jana walianguka wakiwa darasani na
kupoteza fahamu.
Tukio
hilo ambalo limetokea saa tatu asubuhi, limehusishwa na imani za
kishirikina ambapo uongozi wa shule ulilazimika kuwaruhusu wanafunzi
wengine
kurudi majumbani kwao.
Akizungumza
na gazeti hili, Mkuu wa shule hiyo, Bw. Linus Mwakasege, alisema tukio
hilo limekuwa likijirudia mara kwa mara kwa siku za Jumatano na Ijumaa.
“Idadi
ya wanafunzi waliokuwa wa k i a n g u k a k a t i k a s i k u hizi ni
ndogo ambayo huwezi kuilinganisha na tukio la leo (jana) ambalo
limetushtua sana,” alisema Bw. Mwakasege.
Akielezea
mazingira ya tukio hilo, Bw. Mwakasege alisema alianza mwanafunzi mmoja
kupiga kelele akiwa darasani, kuanguka chini na kupoteza fahamu.
Alisema
hali hiyo iliendelea kwa wanafunzi wengine hadi ilipofikia idadi hiyo
na wengine kukimbia ovyo ambapo walimu walifanya kazi kubwa ya
kuwatuliza.
Bw.
Mwakasege alisema baada ya tukio hilo, alifanya jitihada za kuita
viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu ambao walifika shuleni hapo na
kuwaombea wanafunzi waliopatwa na tatizo ambapo hali hiyo iliwasaidia
kurudi katika hali ya kawaida.
Mwanafunzi
mmoja wa shule hiyo ambaye naye alipatwa na tatizo hilo, Hellen Said
alisema hakuwa akifahamu lolote bali alijikuta mapigo ya moyo yakimuenda
mbio, kuanguka na kupoteza fahamu.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Manzese, Bw. Salehe
Rashidi, alisema tukio hilo limekuwa likijirudia shuleni hapo hivyo
atashirikiana na uongozi wa shule kuhakikisha kila mwanafunzi kwa imani
yake wanafanya maombi kila wiki.
“Maombi
haya yatasaidia kukabiliana na mapepo mabaya yanayowaandama wanafunzi
ambao wanakosa uhuru wa kusoma ili kujiwekea msingi mzuri.wa ,aisha
alisema.
|