Mji wa Dodoma Umeanza kupendeza kutokana na Barabara Zinazoingia na kukatiza Mitaa yote kujengwa Kisasa kwa Rami tofauti na Miaka ya Nyuma Dodoma iliyokuwa Vumbi.
Barabara za Manspaa ya Mji wa Dodoma Zikionekana Kupendeza
Barabara za Manspaa ya Mji wa Dodoma Zikionekana Kupendeza
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Vyombo Mbalimbali vya Habari, wanaoripoti Matukio ya Ndani ya Bunge, wakiwa katika Ofisi za Habari ndani ya Bunge leo.
Mgeni Rasmi, akifunga Maonyesho ya Asasi za Kiraia kwenye Viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. leo
Waandishi wa Habari wakifutilia kwa Makini Hotuba ya Mgeni Rasmi wakati wa kufunga Maonyesho hayo.(Picha kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania)
Na:Mwandishi Wetu Dodoma.
Wakati wanafunzi wa Chuo cha Dar es Salaam City College kutoka Tawi la Dar es Salaam, wakiwasili Leo Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha Bunge hapo Kesho, Leo ndani ya Bunge kumeibuka Mzozo Mkubwa kati ya Wabunge na Wabunge kwa kile kilichodaiwa kuwapo kwa kuungwa Mkono Chama kinachosema Jinsia Moja kuoana cha nchini Marekani, ambapo inasemekana kuwa CHADEMA wamekiunga Mkono cha hicho ikiwa ni pamoja na kupokea ruzuku(Msaada )kutoka katika Makao Makuu ya Chama hicho.
Hata hivyo, jumla ya Wanafunzi 56 na Viongozi 6 wa Chuo cha DACICO wanatarajia kuingia Bungeni hapo Kesho, wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa DACICO, Mr. Idrisa Mziray, ambaye amefuatana na Walimu Kilangi Msiba, Vedasto Malima, Saasita, Seif Chomoka,
Katika Mwaliko huo wa DACICO kutembelea Kikao cha Bunge kwa wanafunzi na Walimu, ni moja ya mikakati ya Chuo kuwawezesha wanafunzi kujifunza masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi, na kitaifa ikiwa ni pamoja na kutembelea Vivutio vya Taifa vya Utalii hivi Karibuni.
Kwa Mujibu wa Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment Company Limited, ya jijini Dar es Salaam, ambao ndio waandaaji wakubwa wa safari hizi kwa Chuo hicho, Msemaji wa Miss Demokrasia Tanzania , Mr.Shaaban Mpalule, amesema kuwa baada ya Safari ya Bungeni Chuo hicho kinatarajia kwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Saadan iliyoko katikati ya Bagamoyo na Tanga, kwa lengo la kutembelea Kivutio hicho ikiwa ni pamoja na kuweza kutathmini Utendaji unaofanywa na Wahusika Wakuu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni