Na: Blanca Albert
(DACICO)
Kundi Maarufu la Muziki
wa Taarabu jijin I Dar es Salaam lijulikanalo kwa jina la Mashauzi Classic,
mwishoni mwa juma siku ya jumamosi,
liliweza kuitikisa mbagala katika Ukumbi wa Kisasa Nawina Resort uliopo
mbagala kuu na kukonga nyoyo za Mashabiki.
Safu yetu iliweza
kuongea na meneja wa Bendi hiyo bwana Ismail Rashid “Suma Rager”kwa niaba ya
Mkurugenzi wake Aisha Ramadhani maarufu kwa jina la Aisha Mashauzi, ambaye pia
alisema kuwa aisha hakuwa katika hali nzuri Kiafya hivyo hakuweza kupatikana
baada ya kumaliza onyesho hilo .
Suma Rager ambaye
alizungumza kwa kirufu alisema kuwa malengo ya Bendi hiyo ni kuwapa ajira watu
mbali mbali katika bendi hiyo kwa kuzingatia uwezo na ufanisi wa kazi ya kila
mmoja.
Pia alisemam kuwa lengo
linguine ni kuhakikisha kwamba bendi hiyo inafikia hatua ya kuwa na vitendea
kazi vyake ambavyo vitasaidia kuifanya bendi hiyo kujiendeleza zaidi katika
suala zima la muziki wa hapa nyumbani.
Akizungumzia historia
yak undo hilo kwa ufupi alisema kuwa, ni hatua za kujivunia mpaka sasa kwa
hatua waliofikia, kwani pamoja na kuwa na ushindani wa Miziki hiyo ya Mwambao,
lakini wameshafanikiwa kuwateka baadhi ya mashabiki wa miziki hiyo kutokana na
vibao vyao kuwa vya kuwaridhisha mashabiki wake.
Jumla ya wanamuziki 32
wanajumuhisha kundi hilo akiwamo kiongozi wa kundi ambaye pia ndiye mkurugenzi
mkuu na mwimbaji nyota anayetikisa katika vibao mbali mbali ukiwemo wimbo mpya
wa asiyekujua akuthamini ulioitikisa mbagala kuu Aisha Ramadhani maarufu kama
aisha Mashauzi.
Akizungumzia nyimbo
mpya zinazotarajiwa kutoka hivi karibuni suma rager alisema kuwa “Sura siyo
Roho” wimbo huo unaimbwa na mwimbaji nyota Aisha Ramadhani, na kwamba
wanatarajia kuzindua wimbo wa “Wema hauuzwi na Ubaya Haulipizwi” wimbo ambao
unaimbwa na mwanamuziki Asia Khamis Mzinga.
Kuhusu changamoto
wanazokutana nazo ni kubwa, lakini kwao hakuna changamoto hizo kutokana na hapo
awali muziki wa taarabu ulikuwa kama starehe tofauti na miaka hii ya sasa
ambapo muziki huo umekuwa ni biashara inayoingiza pato kubwa na kukidhi
mahitaji ya wanamuziki ndani ya kundi hilo.
Kuhusu ratiba ya
maonyesho ya burudani wana mashauzi, Suma rager alisema kuwa siku za kupata burudani zao ni Jumanne,
alhamisi na ijumaa ambapo siku ya alhamisi inakuwa ni siku mama ya kuwapa
burudani mashabiki wa kinondoni katika ukumbi wa Mango Gardeni.
Aliitimisha kwa kusema
kuwa, kabla ya uzinduzi wa nyimbo hizo Mashauzi Classic wameandaa shoo kubwa
mashabiki wasubiri siku watakayotangaziwa na wameahidi kufanya onyesho kabambe
kabla ya uzinduzi huo wa nyimbo zao mpya.
Safu
hii pia ilipata fulsa ya kuzungumza na Mkurugenzi wa Nawina Resort, Bi, Mery
Komba, ambaye alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa hatua aliyoweza kufikia katika
kuandaa Burudani katika Ukumbi wa Nawina Resort “ Namshuru Mungu kwa kuwa
ameweza kunisimamia katika kuandaa tamasha hili, kwa si kitu rahisi na wateja
wangu waendelee kutegemea vitu vizuri zaidi kwani nawapenda wote, na napenda
kuchukua fulsa hii kuwakaribisha wakazi wa mbagala na vitongoji vyake katika
ukumbi wa Nawina Resort mbagala kuu, kwani tunaendelea kuwaandaliwa vitu vingi
vizuri vitakavyozidi kuwapa raha”alisema mary Komba.
Aidha
ukumbi huo ambao unapatikana katika Eneo la mbagala kwa sasa umeendelea kuwa
gumzo kutokana na maboresho yaliyofanyika baada ya kupata ajali ya moto hivi
karibuni.
Kutokana
na hivyo umeweza kuboreshwa na kuwa na eneo pana kwa ajili ya usalama, eneo la
maegesho Parking za magari, pikipiki na baiskeli.
Kuhusu
suala la usumbufu kwa wateja kwa sasa katika ukumbi huo hakuna kwani wateja
wanaendelea kupata huduma inayostahili ikiwa ni pamoja na vinywaji na Chakula.
“Natarajia
kuendelea kuukarabati ukumbi huu wa Nawina Resort, na matarajio makubwa ni
kuwawekea wakazi wa mbagala Ukumbi wa kisasa wenye hadhi ya kimataifa
itakayowatikisha watu mbali mbali ususani vijana wa hiki yaani wapenda
burudani, (NIGHT CLUB) itakayo kuwa pamoja na ukumbi”aliongeza Mary Komba.
Hata hivyo aliowataka wapenzi wote wa Nawina
kukaribia kila siku kupata vinywaji na chakula vinavyoandaliwa kwa kiwango cha
hali ya juu ukilinganisha na maeneo mengine .
Vibao
vingine vinavyoendelea kutikisa ndani ya Mashauzi ni pamoja na kibao cha
ropokeni yanayowahusu kilichoimbwa na Saida Ramadhani, Haya ni Mapenzi tu kibao
kilichoimbwa na Zubeida Malicky, Bonge la Bwana kibao kilichoimbwa na Hashim
Saidi.
Burudani hiyo ilianza mapema saa 2:00 usiku na kuendelea.
Burudani hiyo ilianza mapema saa 2:00 usiku na kuendelea.
Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni