Na: Violet John.
(DACICO TANZANIA).
Wakazi wa Mbagala Kuu na Maeneo ya jirani, mwishoni mwa juma
na mwishoni mwa mwezi huu Bendi ya Muziki wa Taarabu ,Mashauzi classic, chini
yake, Aisha Mashauzi, siku ya juzi jumamosi tarehe 30/8/2014 katika Ukumbi wa
Kisasa wa Nawina Resort uliopo Mbagala kuu
ilipowapa raha Mashabiki kwa kibao kipya cha Asiyekujua Akuthamini.
Mwimbaji nyota wa muziki wa Mwambao, Bi, Aisha Mashauzi, akipagawisha katika Ukumbi wa Nawina Resort.
Safu yetu ilipata kuongea
na Meneja wa Mashauzi
Classic Bw. Ismail Rashid (Suma Ragar) baada ya kushindwa kuzungumza na Aisha
Mashauzi kutokana na hali yake kutokuwa nzuri.
Ismail Rashid alisema kuwa malengo makubwa ya bendi hiyo ni
kuwapa watu ajira, kumiliki vitendea kazi, na kujiendeleza kimuziki .
Aidha pia alisema kwamba kwa sasa tayari wamekamilisha
nyimbo kadhaa zinazotarajiwa kuingizwa hivi karibuni kwenye soko la muziki.
Nyimbo zinazotarajiwa kuingizwa sokoni ni pamoja na Sura
siyo Roho, ulioimbwa na Isha Ramadhani, Wema hauuzwi na Ubaya haulipizwi,
ulioimbwa na Asia Hamisi Mzinga.
Vile vile alisema kuwa katika bendi ya Mashauzi kuna
waimbaji thelathini na mbili(32), ambao ni Isha Ramadhani ambaye pia ndiye
mkurugenzi katika bendi hiyo , Rukia Juma ambaye ni mama mzazi wa Isha, Hashimu Saidi, Zubeida
Malicky,Abdulmali Shakani Malicky pamoja na Wengineo.
Mwimbaji nyota wa muziki wa Mwambao, Bi, Aisha Mashauzi, akipagawisha katika Ukumbi wa Nawina Resort.
“Na vile vile napenda kuwakumbusha mashabiki wetu kuwa kila
alhamisi tunakuwa pale Mango Gareden Kinondoni kwa ajili ya kuwaburudisha
mashabiki wetu kwa kiingilio cha shilingi elfu tano tu” alisema Suma.
Safu hii pia ilipata fulsa ya kuzungumza na Mkurugenzi wa
Nawina Resort, Bi, Mery Komba, ambaye alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa hatua
aliyoweza kufikia katika kuandaa Burudani katika Ukumbi wa Nawina Resort “
Namshuru Mungu kwa kuwa ameweza kunisimamia katika kuandaa tamasha hili, kwani si
kitu rahisi na wateja wangu waendelee kutegemea vitu vizuri zaidi kwani
nawapenda wote, na napenda kuchukua fulsa hii kuwakaribisha wakazi wa mbagala
na vitongoji vyake katika ukumbi wa Nawina Resort mbagala kuu, kwani
tunaendelea kuwaandaliwa vitu vingi vizuri vitakavyozidi kuwapa raha”alisema
mary Komba.
Aidha ukumbi huo ambao unapatikana katika Eneo la mbagala
kwa sasa umeendelea kuwa gumzo kutokana na maboresho yaliyofanyika baada ya
kupata ajali ya moto hivi karibuni.
Kutokana na hivyo umeweza kuboreshwa na kuwa na eneo pana
kwa ajili ya usalama, eneo la maegesho Parking za magari, pikipiki na baiskeli.
Kuhusu suala la usumbufu kwa wateja kwa sasa katika ukumbi
huo hakuna kwani wateja wanaendelea kupata huduma inayostahili ikiwa ni pamoja
na vinywaji na Chakula.
“Natarajia kuendelea kuukarabati ukumbi huu wa Nawina
Resort, na matarajio makubwa ni kuwawekea wakazi wa mbagala Ukumbi wa kisasa
wenye hadhi ya kimataifa itakayowatikisha watu mbali mbali ususani vijana wa
hiki yaani wapenda burudani, (NIGHT CLUB) itakayo kuwa pamoja na
ukumbi”aliongeza Mary Komba.
Hata hivyo aliwataka
wapenzi wote wa Nawina kukaribia kila siku kupata vinywaji na chakula
vinavyoandaliwa kwa kiwango cha hali ya juu ukilinganisha na maeneo mengine .
Vibao vingine vinavyoendelea kutikisa ndani ya Mashauzi ni
pamoja na kibao cha ropokeni yanayowahusu kilichoimbwa na Saida Ramadhani, Haya
ni Mapenzi tu kibao kilichoimbwa na Zubeida Malicky, Bonge la Bwana kibao
kilichoimbwa na Hashim Saidi.
Burudani hiyo ilianza mapema saa 2:00 usiku na kuendelea.
Burudani hiyo ilianza mapema saa 2:00 usiku na kuendelea.
Mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni