Jumanne, 25 Machi 2014

BREAKING NEWS: MKUU WA MKOA WA MARA MHE JOHN TUPA AFARIKI DUNIA WILAYANI TARIME MAPEMA LEO


  
Mkuu wa mkoa wa Mara Mhe. John Gabriel Tupa 
(pichani, enzi za uhai wake) amefariki dunia asubuhi ya leo akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Tarime.  

Habari zilizothibitishwa zinasema Marehemu Tupa alianguka na kupoteza fahamu akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. John Henjewele,  alikokuwa akipokea taarifa kabla ya kufunga mafunzo ya mgambo wilayani humo.

Mara baada ya kuanguka juhudi za haraka zilifanyika za kumkimbiza hospitali ya Wilaya ya Tarime ambako alitangazwa kuwa ameshafariki mara alipofikishwa hapo.

Mwili wa Marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Mara ili kuhifadhiwa wakati taratibu za m,aziko zikiandaliwa.

IDADI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA MAPOROMOKO MAREKANI YAFIKIA 14

Waokoaji wakitafuta watu waliopotea katika maporomoko.


MAOFISA wa utawala katika jimbo la Washington nchini Marekani, wamepata miili sita zaidi baada ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea siku ya Jumamosi.
Hii imefikisha idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko hayo hadi 14.
Watu 176 bado hawajapatikana baada ya ukuta wa matope wenye urefu wa futi 177 kuporomoka karibu na mji wa Oso, Kaskazini mwa Seattle.
Zoezi la uokoaji bado linaendelea kwa kutumia helikopta na miale ya Laser, japo maofisa wanakiri kuwa wana matumaini madogo sana ya kupata majeruhi katika tukio hilo..
Rais Barack Obama ametangaza hali ya hatari katika jimbo hilo na kuwaamuru maofisa wote wa serikali ya jimbo hilo kushirikiana kutoa msaada wa dharura.
Gavana wa jimbo hilo ameitaja hali kuwa mbaya na ambayo haikutarajiwa.
Watu 176 bado hawajapatikana.
Jamaa na marafiki pamoja na wafanyakazi wa kujitolea, wanatumia misumeno na mikono mitupu kuondoa vifusi ili kutafuta wale waliopotea.
CHANZO: BBCSWAHILI

Jumapili, 23 Machi 2014

CHELSEA YATOA KIPIGO TAKATIFU KWA ARSENAL

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia baada ya kuifunga Arsenal bao la tano leo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London
Mchezaji wa Arsenal Kieran Gibbs (kushoto) akipewa kadi nyekundu kipindi cha kwanza.
 Na: Zuhura Masoud, DACICO.
============================== 
 
CHELSEA imeifanya kitu kibaya Arsenal baada ya kuichapa mabao 6-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya England ‘Premiership’, leo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London.
Arsenal ambayo iliingia uwanjani katika mechi ya 1,000 tangu kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger alipoanza kuinoa timu hiyo, imekutana na kipigo hicho lakini kukatokea tukio la kushangaza la kadi nyekundu.
Mabao ya Chelsea kwenye mchezo huo yamepatikana kupitia kwa Samuel Eto'o dakika ya 5, Andre Schürrle (7), Eden Hazard (17), Oscar (42 na 66) na Mohamed Salah (71). 
Tukio la kushangaza ni kuwa mwamuzi alimpa kadi nyekundu Gibbs wa Arsenal wakati aliyetenda kosa la kuunawa mpira kwa makusudi ni Oxlade-Chamberlain katika dakika ya 15. 

Chelsea Line-up: 1Petr Cech, 2Branislav Ivanovic, 24Gary Cahill, 26John Terry, 28César Azpilicueta, 4David Luiz, 11Oscar,14Andre Schürrle, 17Eden Hazard, 21Nemanja Matic,29Samuel Eto'o 
Substitutes: 23Mark Schwarzer, 33Tomas Kalas, 8Frank Lampard, 12John Mikel Obi, 15Mohamed Salah, 9Fernando Torres, 19 Demba Ba

Arsenal Line- up: 1Wojciech Szczesny, 3Bacary Sagna, 4Per Mertesacker, 6Laurent Koscielny, 28 Kieran Gibbs, 7Tomas Rosicky, 8 Mikel Arteta, 9 Lukas Podolski, 5 Thomas Vermaelen, 15 Alex Oxlade-Chamberlain, 19 Santi Cazorla, 12 Olivier Giroud

Substitutes: 21Lukasz Fabianski, 5Thomas Vermaelen, 25Carl Jenkinson, 20Mathieu Flamini, 29Kim Kallstrom, 22Yaya Sanogo,44Serge Gnabry

Tamasha la Bagamoyo Marathon lazinduliwa

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel (kushoto) akishikana mikono na Mkurugrenzi wa Kampuni ya 4Beli, Gilbert Herman baada ya kuzindua  Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo Wilayani  Bagamoyo, Pwani .  Anayeangalia ni,  Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel akizungumza katika hafla ya uzinduzi  wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo uliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani.  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala,  Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo,  Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali na Mkurugenzi wa 4Beli, Gilbert Herman. 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali alizungumza katika hafla ya uzinduzi  wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo iliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani .  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala, Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel na Mkurugenzi wa 4Beli, Giulbert Herman.
Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf  Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo katika uzinduzi wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo uliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel, Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali na Mkurugenzi wa 4Beli, Gilbert Herman.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya 4Beli, Deogratius Soka (kulia) akisoma hotuba wakati wa uzinduzi  wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo uliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala,  Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel, Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali na Mkurugenzi wa 4Beli, Gilbert Herman.
Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi.

WIKI YA MAJI YA MAADHIMISHO MKOA WA NJOMBE YAFANA KATIKA VIWANJA VYA MABEHEWANI

Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi akipata maelekezo kwenye banda la idara ya maji kuhusu bili za maji, katika wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani Makete mjini.
Mkuu wa mkoa Kapt. Msangi akisikiliza maelekezo toka kwa mtaalamu wa maji, katikati ni mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro.
Mkuu wa mkoa akipata maelekezo kuhusu mfumo mzima wa maji Makete mjini unavyofanya kazi.
 Kikundi cha sanaa cha SUMASESU kikitumbuiza kwenye maadhimisho hayo ya wiki ya maji.
 Kikundi cha sanaa kijulikanachoa kama Mchana Hasarani kikikonga nyoyo za washiriki wa maadhimisho hayo.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani Makete mjini.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe kapteni Mstaafu Aseri Msangi akihutubia wananchi waliofika kumsikiliza katika maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani makete mjini.
Mkuu wa mkoa akihutubia wananchi.Picha zote na Edwin Moshi, Makete.

IKONDOLELO HOTELI YAENDELEZA BURUDANI JIJINI DAR ES SALAAM

IKONDOLELO HOTELI YAENDELEZA BURUDANI JIJINI DAR ES SALAAM.
Na:zuhura Masoud.

Hoteli ya Kimataifa ya Ikondolelo ya Kibamba jijini Dar es Salaam, imeendelea kuwa gumzo kutokana na kuweka burudani mbali mbali ndani ya Kumbi zinazopatikana katika hoteli hiyo ambayo ni ya kisasa na yenye adhi ya kimataifa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Maeneo hayo ya Kibamba, wamesema kuwa wanampongeza mkurugenzi wa IKONDOLELO HOTELI kwa kuweka miundombinu kabambe ya kuhakikisha wakazi wa maeneo hayo wanapata fursa ya kushiriki Kimichezo pamojana kwamba walisahauliwa kwa muda mefu.

Aidha Hoteli hyo ambayo imejengwa kwa ustadi mkubwa, imewekewa manzali za kuvutia kwa wageni wote wanaopata fursa ya kwenda kutembelea maeneo hayo ikiwamo wakazi wa jiji wanaokwenda kwa lengo la kujiburudisha kwa njia mbali mbali ikiwamo, Kuogelea, kucheza Poltable,Burudani ya Muziki na mengine mengi.

Hata hivyo wameogeza kusema kuwa, hapo awali kabla ya hoteli hyo kujengwa maeneo hayo, kwao burudani zilikuwa zikionekana tu kama ni kwa baadhi ya watu kutokana na kuwa kimya kwa muda mrefu kitendo kilichokuwa kinawaweka katika Dunia ya giza na kuwaondoa katika utandawazi wa Dunia ya Sayansi na Teknolojia.

IKONDOLELO ambayo kwa ujumla imejengwa kwa Ustadi mkubwa, imefanikiwa kuwekewa Bwawa la kuogela la kisasa ambalo linakidhi mahitaji ya vijana wengi wa jimbo la Ubungo kwa ujumla ikiwemo na maeneo ya Kibaha wilaya ya Pwani.


mbali na bwawa hilo pia IKONDOLELO ni moja ya Hoteli ambayo inamazingira ya kupendeza ususani kuna maeneo ya kupendeza kwa ajili ya mapumziko kwa watu wanaopata fulsa ya kwenda kupata vinywaji pamoja na wale wanaopata fulsa ya kwenda kufanya Sherehe, Mikutano, Maharusi na mengine mengi.

katika Hoteli ya IKONDOLELO kati ya vitu ambavyo pia vinaonekana kuwavutia wakazi wa maeneo hayo ni pamoja na Eneo la Maegesho ya Magari(Parking) ambayo ni ya kipekee kutokana na kila mgeni mwenye usafiri kuwa na uhakika na Ulinzi wa Mali ama vifaa wanapokuwa ndani ya Hoteli hiyo .

Nilipata fulsa pia ya kuzungumza na Meneja wa Hoteli hiyo bwana..Mnyika..ambaye aliweka wazi kuwa kutokana na kutambua hali ya maisha na mahitaji ya watu, waliamua kuweka burudani kwa lengo la kuwaweka watoto  na vijana karibu na mazingira ya nyumba zao pasipokutoka kwenda mbali ususani wakati wa sikukuu ambazo burudani zinakuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuwafurahisha watu wote waoapata fulsa ya kuingia ndani ya IKONDOLELO.

Aidha amesema kuwa pamoja na hali hiyo pia wamezingatia ubora wa gharama kwa wahitaji, ambapo alisemakuwa garama zao ni nafuu kwa wale wanaokwenda kwa ajili ya kukodi Ukumbi kwa ajili ya Maharusi na sherehe alimbali.

naye Mkurugenzi wa Hoteli hiyo bwana..Humbiye.alisema kuwa anawashukuru wote wanaoendelea kumpa ushirikiano katika kuijenga upya Hoteli hiyo ambayo kwa sasa inaonekana kuwa ndiyo Hoteli kubwa kuliko zingine inayopatikana maeneo ya Jimbo la Ubungo, ikiwa CCM Kibamba, njia ya Kibwegele.

"Binafsi ninawakaribisha sana wateja wangu ambao wanapata muda na kuweza kuja hapa, kwa hiyo niseme kuwa nawapenda kwa kuwa wanapata fulsa pia ya kuniunga mkono, na hata nyinyi wandishi pia nawakaribisha, hapa kwangu kuna kumbi nyingi, mnaweza hata kuja kubadilisha manzali kwa ajili ya sherehe zenu, au hata mje mpate kuogelea kama unavyoona jinsi watu walivyowengi yaani wanaendelea kufurahi kila mmoja kwa nafasi yake.

VYUO mbalimbali nchini Vyashauriwa kujenga mahusiano ya kirafiki ili kubadilishana uzoefu katika kufanya kazi zao.

 Mtembeza wageni wa Kidishi Multi Spices Farm Bwana. Mur- tala Rashid akiwaonyesha mmoja wa mmea wa Spice na kuwafahamisha matumizi yake, mmea huo unaotambuliwa kwa jina la mchaichai katika chamba hilo.
 Wanafunzi wakifurahiya maelezo kutoka kwa Mtembeza wageni wa Kidishi Multi Spices Farm Bwana. Mur- tala Rashid (hayupo pichani). 
Baadhi ya wanafunzi wakionyeshana Spices walipokuwa wamepumzika katika shamba la Kidishi Multi Spices Farm lililopo Kidichi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. (Picha zote na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

========  =======  ========
Na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.

VYUO mbalimbali nchini, vimeshauriwa kujenga mahusiano ya kirafiki kati yao ili kubadilishana uzoefu katika kufanya kazi zao.
Ushauri huo umetolewa na mkuu wa msafara wa wanafunzi 70 kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii Dar es Salaam, Dawson Kyungai, wakati wakiwa katika ziara kuwatembelea viongozi wenzao wa Chuo cha Elimu Zanzibar (Zanzibar Education College).
Kyungai ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa ujasiri wao wa kutafuta njia za kujenga mahusiano na vyuo mbalimbali nchini. Naye Mkuu wa Zanzibar Education College Ussi Said Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari katika Kanisa la Mkunazini walikotembelea, alisema suala la urafiki wa vyuo linawasaidia walimu na wanafunzi kubadilishana mawazo na kujifunza kwa ufanisi zaidi.
Wanafunzi hao 70 wako katika ziara ya siku tatu kuwatembelea wenzao wa Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu pamoja na kuzuru sehemu mbalimbali za kihistoria za Zanzibar.
Kwa upande wao, wanafunzi na walimu wa Zanzibar Education College, wanatarajia kufanya ziara kama hiyo Mkoani Dodoma mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.
  Mtembeza wageni wa Kanisa la Mkunazini akiwafahamisha kitu wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii kutoka Dar es salam walipokuwa wakitembelea Kanisa hilo.
 Wanafunzi wakipata maelezo kwa Mtembeza wageni juu sehemu walipokuwa wakihifadhiwa watumwa Kanisani hapo.
 Wanafunzi wakitoka nje kwa furaha mara baada ya kutembelea Kanisa la Mkunazini liliopo Mjini Unguja. 
 Hapa wanafunzi wakijichagulia katika moja ya maduka ya vinyago na nguo za Kiswahili yaliopo Ngome kongwe Mjini Unguja. 
 Wanafunzi wakionyeshana Spices.

Jumamosi, 22 Machi 2014

Na:Dacico Matukio

Swala la kuapishwa kwa Raisi mteule wa Dar-es-salaam city college Bw. Goodluck Kajuna limezua gumzo kubwa chuoni humo kwani zoezi la kuapishwa kwake limekuwa kizungu mkuti pasipo mwanachuo yeyote kufahamu ataapishwa lini. Tume ya uchaguzi imeachwa njia panda kwani siku waliyopanga kumwapisha/kumlisha kiapo kuhahirishwa . wanachuo wengi chouni humo kwani hawajui nani wamfute ili kufikisha matatizo yao yaki elimu na mengine yaki binafsi ambayo huwezi kumwambia mwalimu bali kiongozi wa chuo.
Like ·  ·  · 23 hours ago ·


  • 2 people like this.
  • Maria Chausi Wana2boa bana!
    20 hours ago · Like · 1
  • Albert Kenedy kama chuo kikubwa kinakuwa na matatizo hayo mataw itakuaje ebu fanyien kumwapisha kuepusha tatizo mnakuwa kama sio wasomi au hamkulizika na uteuz wake mpaka mnaamuwa kufanya hayo muwe m,fano wa kuigwa nyie mkiwa ivo wa mbeya/sumbwanga watafika wap rekebishen utaratibu uwe sawa jaman sio vizuri
    12 hours ago · Like · 1
  • Mwambazi Martini Haina maana manegment kuwepo oficn coz hawana msaada kwa wanachuo
  • Mpalule Shaban