Jumatatu, 17 Machi 2014

kumekucha kesho uwanja wa taifa- YANGA kuwavaa azam f.c, mashabiki wakesha kusubiri mtanange huo.

Na Zuhura Masoud, DACICO F. M -RADIO , Dar es salaam
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara,Young Africans, ya jijini Dar es Salaam, kesho inashuka dimba la Uwanja wa Taifa kuwakabili Azam F.c, wana Lamba-lamba, katka mchezo unaotazamiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na timu zote mbili kuwa kwenye nafasi ya kuwania Ubinwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Wana Lamba-lamba Azam fc waliopo kileleni, mpaka sasa tayari imekusanya pointi 43 na ikiwa inaendelea kushika usukani wa ligi hiyo, wanaendelea na mipango mbalimbali kuhakikisha wanapata ushindi mbele ya Yanga inayotajwa kuwa na kikosi bora zaidi msimu huu.
wakizungumzia mchezo huo mashabiki watani wa jadi-jijini Dar s Salaam, wamesema kuwa ni Yanga msimu huu imesheheni majina ya wachezaji wenye majina makubwa na zaidi yakiwa na mvuto nje na ndaniya uwanja, japokuwa ndani ya uwanja bado kuna matatizo yanayopaswa kutatuliwa kwa haraka.
aidha wadau wa soka Dacico pia wameongeza kuwa, Ukitaja majina kama kina, Emmanuel Anord Okwi, Hamis Friday Kiiza `Diego`, Didier Kavumbagu `Kavu`, Mrisho Khalfan Ngasa `Anko`, Simon Msuva , Said Bahanuzi, Jeryson John Tegete ambao huongoza safu ya ushambuliaji, inachangia kuwatia hofu wachezaji wa timu wa timu pinzani.
33Pia wanadacico hao wamesema kuwa wachezaji wa dimba la kati, katika timu ya yanga ni wakali wakiwapo, Haruna Niyonzima `Fabregas`, Frank Domayo `Chumvi`, Athuman Idd `Chuji` , Hassan Dilunga na wengineo ambao hawana namba za kudumu katika kikosi cha kwanza.
wakati kwenye safu ya ulinzi wamedai kuwa, imesukwa kwa mabeki visiki wakiwemo Kelvin Patrick Yondan, Nadir Haroub `Canavaro`, Mbuyu Twite, Oscar Samwel Joshua, David Luhende na wengineo.
Hata hivyo, Ukiangalia tofauti ya majina baina ya Yanga na Azam fc, Wanajangwani inaonyesha kwenye rekodi kuwa ni chama kubwa zaidi kwa maana ya kuwa na mtaji mkubwa wa wanachama, mashabiki na hata ukongwe wa ligi kuu soka Tanzania bara.
1236000_631243993582627_1970842772_nna kwamba mpaka sasa timu ya yanga imejihakikishia utajiri mkuu katika mipango ya uwekezaji katika anga za kimichezo , ukilinganisha na Azam fc ambao wameingia kwenye ushindani miaka ya ivi karibuni.
habari za kuhaminika zinasemakwamba , Wakati mashabiki wakisubiri mechi hiyo kwa hamu kubwa, tayari kikosi cha Yanga kimeingia chimbo(mafichoni) Fukwe za Bagamoyo,Pwani kujiwinda na mechi hiyo ya kesho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni