IKONDOLELO HOTELI YAENDELEZA BURUDANI JIJINI DAR ES SALAAM.
Na:zuhura Masoud.
Hoteli ya Kimataifa ya Ikondolelo ya Kibamba jijini Dar es Salaam, imeendelea kuwa gumzo kutokana na kuweka burudani mbali mbali ndani ya Kumbi zinazopatikana katika hoteli hiyo ambayo ni ya kisasa na yenye adhi ya kimataifa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Maeneo hayo ya Kibamba, wamesema kuwa wanampongeza mkurugenzi wa IKONDOLELO HOTELI kwa kuweka miundombinu kabambe ya kuhakikisha wakazi wa maeneo hayo wanapata fursa ya kushiriki Kimichezo pamojana kwamba walisahauliwa kwa muda mefu.
Aidha Hoteli hyo ambayo imejengwa kwa ustadi mkubwa, imewekewa manzali za kuvutia kwa wageni wote wanaopata fursa ya kwenda kutembelea maeneo hayo ikiwamo wakazi wa jiji wanaokwenda kwa lengo la kujiburudisha kwa njia mbali mbali ikiwamo, Kuogelea, kucheza Poltable,Burudani ya Muziki na mengine mengi.
Hata hivyo wameogeza kusema kuwa, hapo awali kabla ya hoteli hyo kujengwa maeneo hayo, kwao burudani zilikuwa zikionekana tu kama ni kwa baadhi ya watu kutokana na kuwa kimya kwa muda mrefu kitendo kilichokuwa kinawaweka katika Dunia ya giza na kuwaondoa katika utandawazi wa Dunia ya Sayansi na Teknolojia.
IKONDOLELO ambayo kwa ujumla imejengwa kwa Ustadi mkubwa, imefanikiwa kuwekewa Bwawa la kuogela la kisasa ambalo linakidhi mahitaji ya vijana wengi wa jimbo la Ubungo kwa ujumla ikiwemo na maeneo ya Kibaha wilaya ya Pwani.
mbali na bwawa hilo pia IKONDOLELO ni moja ya Hoteli ambayo inamazingira ya kupendeza ususani kuna maeneo ya kupendeza kwa ajili ya mapumziko kwa watu wanaopata fulsa ya kwenda kupata vinywaji pamoja na wale wanaopata fulsa ya kwenda kufanya Sherehe, Mikutano, Maharusi na mengine mengi.
katika Hoteli ya IKONDOLELO kati ya vitu ambavyo pia vinaonekana kuwavutia wakazi wa maeneo hayo ni pamoja na Eneo la Maegesho ya Magari(Parking) ambayo ni ya kipekee kutokana na kila mgeni mwenye usafiri kuwa na uhakika na Ulinzi wa Mali ama vifaa wanapokuwa ndani ya Hoteli hiyo .
Nilipata fulsa pia ya kuzungumza na Meneja wa Hoteli hiyo bwana..Mnyika..ambaye aliweka wazi kuwa kutokana na kutambua hali ya maisha na mahitaji ya watu, waliamua kuweka burudani kwa lengo la kuwaweka watoto na vijana karibu na mazingira ya nyumba zao pasipokutoka kwenda mbali ususani wakati wa sikukuu ambazo burudani zinakuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuwafurahisha watu wote waoapata fulsa ya kuingia ndani ya IKONDOLELO.
Aidha amesema kuwa pamoja na hali hiyo pia wamezingatia ubora wa gharama kwa wahitaji, ambapo alisemakuwa garama zao ni nafuu kwa wale wanaokwenda kwa ajili ya kukodi Ukumbi kwa ajili ya Maharusi na sherehe alimbali.
naye Mkurugenzi wa Hoteli hiyo bwana..Humbiye.alisema kuwa anawashukuru wote wanaoendelea kumpa ushirikiano katika kuijenga upya Hoteli hiyo ambayo kwa sasa inaonekana kuwa ndiyo Hoteli kubwa kuliko zingine inayopatikana maeneo ya Jimbo la Ubungo, ikiwa CCM Kibamba, njia ya Kibwegele.
"Binafsi ninawakaribisha sana wateja wangu ambao wanapata muda na kuweza kuja hapa, kwa hiyo niseme kuwa nawapenda kwa kuwa wanapata fulsa pia ya kuniunga mkono, na hata nyinyi wandishi pia nawakaribisha, hapa kwangu kuna kumbi nyingi, mnaweza hata kuja kubadilisha manzali kwa ajili ya sherehe zenu, au hata mje mpate kuogelea kama unavyoona jinsi watu walivyowengi yaani wanaendelea kufurahi kila mmoja kwa nafasi yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni