Na:Zuhura Masoud,DACICO FM.COM,Dar es salaam.
MCHEZAJI ghali zaidi duniani, Gareth Bale kesho katika mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Schalke 04 dimba la Santiago Bernabeu atavaa viatu vipya `njumu` kutoka kampuni ya Adidas.
Viatu hivyo vya `adidas F50 crazylight`, vina uzito wa gramu 135 na vimebuniwa kwa ufundi mkubwa.
Gareth Bale alionekana leo hii akijaribu viatu hivyo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mazoezi ya Real Madrid na atakuwa wa kwanza pekee kuvaa viatu hivyo.
Viatu vipya: Gareth Bale atavaa viatu vyake vipya kutoka kampuni ya adidas
Jinsi viatu hivyo vilivyobuniwa, lazima mabeki wachanganyikiwe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni