Na:Zuhura Masoud, WWW.DACICO FM RADIO.COM
KOCHA wa timu ya vijana ya Everton chini ya miaka 18, Kevin Sheedy ameandika ujumbe mzito katika akaunti yake ya Twite akimkosoa kocha wa Manchester United, David Moyes kuwa katika maisha yake akiwa Merseyside alikuwa hapendelei kuwatumia vijana wake.
Sheedy alifanya kazi kwa zaidi ya miaka saba akiwa kocha wa Akademi ya klabu hiyo wakati Moyes akiwa kocha mkuu wa timu ya wakubwa kabla ya kutimkia Man United kurithi mikoba ya Alex Ferguson.
Moyes na Man United yake jana waliangukia pua baada ya kulala kwa kipigo kizito cha mabao 3-0 kutoka kwa majogoo wa jiji, Liverpool, katika dimba lao la Old Trafford
Kocha wa vijana chini ya miaka 18 wa Everton Kevin Sheedy amemkosoa David Moyes kwa kutokuwa na tabia ya kuwatumia vijana
wakati akifanya naye kazi Everton
Kakata tamaa: Moyes akionekana kukata tamaa baada ya kipigo cha mabao 3-0 jana dhidi ya Liverpool
Akirudi kazini: Moyes akiwasili katika uwanja wa mazoezi wa Man United, Carrington jana
Mechi imekwisha: Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez akifurahia bao la tatu hapo jana huku mpira ukielekea kumalizika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni