Jumapili, 28 Julai 2013

HATARI TUPU


Na Mwandishi wetu
UJENZI wa majengo marefu jijini Dar es Salaam unazidi kuleta hofu baada ya kubainika jengo la ghorofa zaidi ya saba lenye nyufa kiasi cha kutishia maisha ya wanaolitumia na wapitanjia.Uchunguzi uliofanywa na Majira umebaini kuwa jengo hilo lipo mtaa wa Asia na Mali karibu na kituo cha mafuta Barabara ya Samora jijini Dar es Salaam. Jengo hilo lina nyufa nyingi kiasi cha kutishia wapita njia na baadhi ya watumiaji wake.

Mmiliki wa jengo hilo alipotakiwa kutolea ufafanuzi hali hiyo na sababu ya kuruhusu liendelee kutumika alijibu kuwa; "Kama unataka kuandika habari kuhusu ufa kuna majengo zaidi ya 10 ambayo yana nyufa hapa Dar es Salaam kama upo tayari nikupeleke ili nikuoneshe hayo majengo na ukitaka kuandika uanze na hayo," alisema.
Alisema kila baada ya siku wakaguzi kutoka manispaa ya Ilala hufika katika jengo hilo kulikagua, hivyo majibu yote yanapatikana manispaa hiyo."Mimi sina jibu la kukwambia zaidi ya wewe uende manispaa ndio watakupa majibu yote unayotaka... sawa?"Alisema mmiliki wa jengo hilo.
Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni iliyojenga jengo hilo (jina tunalo) alisema jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2006 na kukamilika 2008 hivyo lina miaka zaidi ya sita sasa.Alisema kama lingekuwa na matatizo basi wasingepewa vibali vya kuruhusu kutumika. Alisema tangu lilipoanza kujengwa lilikuwa linakaguliwa na mamlaka husika hadi lilipomalizika kujengwa, kwani lina vibali vyote na ndio maana watu wanalitumia.
"Ukitaka kufuatilia basi lazima uende kwenye mamlaka husika utapata hicho unachokitafuta," alisema ofisa huyo. Baadhi ya wapangaji katika jengo hilo walisema wao wamekuwa wakimuona mmiliki wa jengo hilo na mhandisi wa kampuni iliyolijenga wakifika katika jengo hilo mara kwa mara na kulikagua, lakini hawaelewi ni kwa nini wanafanya hivyo.
"Huwa tunawaona mmiliki wa jengo hili na injinia ambaye amelijenga jengo hilo mara kwa mara wanakuja mbele ya jengo na kisha kuelekezana kuelekea juu kwa kuwa hatuelewi basi huwa tunawaangalia tu, lakini kumbe kuna ufa sasa ndio tumejua ni kwa nini wanafanya hivyo," alisema mmoja wa wapangaji na kuongeza kuwa kipindi cha milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi Mbagala, jengo hili lilitikisika sana hadi wakaamriwa wafunge maduka watoke.Juhudi za kumtafuta Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ili kuzungumzia suala hilo zilishindikana kwa kile kilichoelezwa na Katibu Muhutasi wake kwamba ana siku maalum ya kumuona.
Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, alijibu kwamba yupo kwenye kikao, hivyo atume ujumbe mfupi wa simu. Pamoja na kutumiwa ujumbe huo tangu Jumatatu na gazeti hili kuzidi kumfuatilia, alijibu suala hilo atampa injinia wa manispaa ya Ilala afuatilie.
P amo j a n a a h a d i h i y o alipofuatiliwa zaidi aliahidi kutoa namba za simu za injinia huyo kwa mwandishi wa gazeti hili ili awasiliane naye, lakini hakufanya hivyo na alipopigiwa simu ilikuwa haipokelewi.Gazeti hili pia lilimtafuta Msajili wa Bodi ya Wahandisi (ERB) Injinia Steven Mlote, ambapo alisema kwamba yuko mkoani Arusha, lakini amewaagiza baadhi ya wafanyakazi kufuatilia jengo hilo mara moja.
Alipotafutwa tena ili atoe ufafanuzi kuhusu jambo hilo, Mlote alisema alikuwa hajapata taarifa zozote kutoka kwa wasaidizi wake, hivyo alimtaka mwandishi wa habari hii kufika ofisini kwake ili akapate taarifa.
Licha ya mwandishi kufika ofisi za ERB hakupata ushirikiano wowote na Mlote alipotafutwa tena simu yake haikupatikana.
Kwa upande wa Ofisa Uhusiano wa Wakala wa Majengo (TBA), aliyejulikana kwa jina moja la Mariam alipotakiwa kuzungumzia jengo hilo, alitaka aandikiwe maswali ili ayajibu kimaandishi
  • AHAMASISHA MAANDAMANO KUPINGA VIONGOZI MAFISADI
  • HARAMBEE ZA MAMILIONI YA FEDHA KILA WIKI ZAMTISHA

 Na Waandishi Wetu
WA Z I R I w a A f r i k a Mashariki, Samuel Sitta, ameunga mkono Tanzania kuwa na mfumo wa Serikali tatu lakini sio marais watatu na kwamba wanaopigania jambo hilo wanataka kugombania madaraka.Sitta alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana wakati wa ufunguzi wa majadiliano ya Rasimu ya Katiba Mpya lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Vijana la Katiba nchini.

Alisema mfumo wa kuwa na marais watatu utaongeza gharama, hivyo ni vyema ziwepo Serikali tatu ambazo zitaongozwa na rais mmoja. Alisema fedha ambazo zingetumika kuhudumia Serikali yenye marais watatu zitatumika kwenye sekta za afya, elimu na kilimo."Leo tukiwa na marais watatu, mmoja aende China, mwingine Uingereza sijui wapi sasa hizo gharama zitatoka wapi?"Alihoji.

Ubinafsi wa viongozi
Katika hatua nyingine, Waziri Sitta amewataka Watanzania kuandamana kupinga viongozi walafi na wabinafsi wanaotaka kujilimbikizia mali.Alisema kwa hata Tanzania iwe na Katiba nzuri namna gani bila wananchi kupigania maadili ikiwa ni pamoja na kuandamana kupinga viongozi wa aina hiyo.

"Katika nchi yetu tumekuwa na viongozi wengi wa kijamii ambao ni walafi sana na wabinafsi, kama vijana hamtakuwa mstari wa mbele kuwapinga basi nchi yetu haitatawalika,"alisema, Sitta.Akifafanua zaidi alisema haiwezekani baadhi ya watu wachache wawe matajiri wakubwa huku wananchi wengi wakiwa masikini kupitiliza. "Kama ni suala la akili watu wote wanazo akili, inakuwaje wao tu ndio wawe matajiri?" Alihoji.

Alisema ni vema katiba mpya ielekeze utungaji wa sheria zitakazozuia ubinafsi, udikteta, ubaguzi, ikiwa ni pamoja na kuzuia kiongozi kufanya kazi kwa masilahi yake binafsi.Alifafanua zaidi akisema ili nchi ipate maendeleo, Serikali inatakiwa kupunguza fedha katika utawala na kuzielekeza katika miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu.

Alisema kuna baadhi ya viongozi (bila kuwataja) wameanzisha kampuni hewa kwa lengo la kujipatia fedha, lakini uchunguzi unafanyika dhidi yao bila matokeo kutangazwa.Alihoji uchunguzi wa aina hiyo utafanyika hadi lini? "Kumebainika kuwa kuna kampuni tatu hewa ambazo zinajipatia fedha kwa njia isiyo halali, uchunguzi unafanyika ili kutafuta ukweli, japokuwa hatuambiwi matokeo ya uchunguzi mara baada ya kukamilika, nchi yetu itaendelea kuwa ya uchunguzi hadi lini?"Alihoji Bw.Sitta.

Katika hatua nyingine, Sitta amewashangaa baadhi ya viongozi nchini wanaohifadhi fedha zao nchi za nje na kuhoji lengo lao ni nini?Alisema siku hizi vyombo vya habari vinafanya kazi nzuri ya kuwafichua viongozi wabadhirifu h i v y o k u s a i d i a wa n a n c h i kuwafahamu.

Harambee makanisa
Waziri Sitta alipoulizwa na waandishi wa habari maoni yake kuhusiana na watu wanaotoa misaada makanisani, alijibu kuwa hata yeye kipindi cha nyuma aliwahi kusimamia kujenga msikiti wilayani Mirambo, lakini haikuwa shida.
"Lakini kwa sasa viwango vinatisha mtu anachangisha mamilioni ya fedha kila wiki...hii inatisha," alisema na kuhoji kuwa watu hao fedha wanazipata wapi? Alisema kuwa inawezekana nyuma yao kuna watu wanaowasaidia.
Mrema anena
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, Augustino Mrema, alisema mfumo wa Serikali tatu gharama kubwa kiuendeshaji na utasababisha migogoro nchini.Akizungumza na Majira, Mrema alisema kuwa Serikali tatu zinafaa kinadharia na sio kiutekelezaji kwani zitaweza kuhitaji gharama kubwa katika uendeshwaji wake.

“Maoni yangu binafsi juu ya rasimu mpya ya uundwaji wa Katiba Mpya, kuwa Serikali tatu inafaa kinadharia na sio kiutekelezaji, mfano kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Tanzania na Serikali ya Zanzibar nani atagharamia hizo Serikali?" Alihoji.
Aliendelea kuhoji; " Huku kuwe na mabunge matatu na la muungano, pia kuwe na Ikulu ya muungano, Ikulu ya Tanzania na Zanzibar, nani atakayeweza kugharamia Serikali zote tatu‚“ alihoji Mrema.
Imeandikwa na Kassim Mahege, Frank Monyo Penina Malundo na Neema Malley
  MBOWE AWATUNISHIA MSULI POLISI

Na Stella Aron
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ameendelea kuliwekea ngumu Jeshi la Polisi nchini kwa kukataa kukabidhi mkanda wa video unaoonesha tukio la mlipuko wa bomu uliotokea kwenye mkutano wa CHADEMA, mkoani Arusha wakati wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa kata nne za madiwani.
Mbowe aliripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam jana kufuatia barua aliyoandikiwa na jeshi hilo likimtaka afike na kuwasilisha mkanda huo, anaodai anao. Akizungumza na gazeti hili Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa CHADEMA, John Mnyika, alisema barua hiyo ya Polisi ilikuwa ikieleza kuwa endapo atashindwa kuwasilisha mkanda huo atakuwa ametenda kosa la jinai.

Mnyika alisema Mbowe alienda mwenyewe Polisi akiwa na wakili wa CHADEMA, Peter Kibatala na viongozi wengine wa chama. Mnyika alisema Mbowe aliwaambia Polisi kuwa ushahidi wa mkanda huo hataukabidhi kwao, kwani wao ni miongoni mwa watuhumiwa. "Amewaambia kama ni kosa la jinai libaki hivyo, lakini hawezi kuwakabidhi mkanda huo kwa kuwa na wao ni miongoni mwa watuhumiwa," alisema Mnyika.
Kwa mujibu wa Mnyika, Mbowe ameendelea na msimamo wake kuwa mkanda huo ataukabidhi kwa Tume ya Kijaji itakayoundwa na si vinginevyo. Aliongeza kuwa baada ya maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA iliyokutana hivi karibuni, Mbowe alimwandikia Rais Jakaya Kikwete, barua ya kumtaka aunde Tume ya Kijaji ya kuchunguza tukio hilo, lakini hadi sasa bado haijajibiwa.
Katika tukio hilo la mlipuko wa bomu watu wanne walifariki na wengine wengi kujeruhiwa. Tangu wakati huo, Mbowe amekuwa akidai kuwa ana ushahidi wa video wa tukio hilo, lakini amekataa kuukabidhi kwa polisi kwa kile anachodai kwamba na wao ni miongoni mwa watuhumiwa. "Kwa hiyo amewaambia Polisi kuwa bado jambo hilo ameandikiwa Rais Kikwete na bado hajajibu hivyo hawezi kufanya hivyo," alisema Mnyika akimnukuu Mbowe.
Alisema baada ya mazungumzo ya kina kati yake na Polisi, walikubaliana kwamba Mbowe aeleze msimamo wake huo kwa maandishi na kuwapelekea Polisi kesho na baada ya hapo watajua la kufanya.
Alisema baada ya mazungumzo hayo Mbowe aliondoka na yupo huru
Prince William na mkewe Kate wakitabasamu huku wakitoka ndani ya Hospitali ya Mt. Mary iliyopo Magharibi mwa London juzi,ambako Kate alijifungua mtoto wa kiume aliyempakata.

Na Rehema Mohamed
ALIYEKUWA Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Ukonga, G 5226 PC Ramadhani Selemani (27), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu kazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 120.Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi ni mkazi wa Mbagala Zakhem, Hamis Mwanya (22).

Mbele ya Hakimu Nyigulila Mwaseba, ilidaiwa na Wakili wa Serikali Mwanaisha Komba, kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 19, mwaka huu Tazara Wilaya ya Temeke.Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alikutwa na meno manne ya tembo pamoja na vipande 12 vya meno hayo mali ya serikali. Mshtakiwa huyo hakutakiwa kujibu kosa hilo.Upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kwamba shauri hilo litatajwa tena Agosti 7, mwaka huu.

 Na Eliasa Ally, Iringa
WANAFUNZI 12 wa Shule ya Sekondari ya Mlowa iliyopo Wilaya ya Iringa Vijijini wamenusurika kufa baada ya bweni walilokuwa wamelala kuungua kwa moto na kuteketeza vitu ambayo vilikuwemo ndani. Tukio hilo linadaiwa lilitokea baada ya hitilafu ya umeme wa nishati ya jua (Sola) iliyosababishwa na wanafunzi ambao walikuwa wamelala katika bweni hilo kuunganisha nyaya kienyeji kwa ajili ya kusikiliza redio na kusababisha hasara ambayo inakadiriwa kufikia sh. milioni 1.8.

Akizungumzia jana ofisini kwake juu ya tukio hilo la kuungua kwa bweni na kunusurika kwa wanafunzi, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mlowa, Mwalimu Frank Mahai alisema wanafunzi wa l i o n u s u r i k a awa l i walikuwa wanaishi nje ya shule. Alisema, mipango ya kuishi katika bweni hilo ilifanywa katika kikao cha wazazi na walimu kwa ajili ya wanafunzi ambao wanatoka mbali na shule ili wapate mahali pa kuishi katika muhula wa mitihani ya mwisho.
Mkuu huyo alisema kuwa, wanafunzi wengine wa shule hiyo wakati inaungua walikuwa wamekwenda kucheza mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana katika Shule ya Sekondari ya Kalenga na kubakia wanafunzi 12 katika bweni ambapo saa 1:30 jioni moto ulianza kuunguza bweni hilo.
“Wanafunzi waliohusika na kuunguza ni baada ya kuunganisha nyaya kienyeji na kusababisha shoti hadi kuunguza bweni hilo,” alisema Mkuu huyo. Alivitaja vitu vilivyoungua kuwa ni pamoja na nguo za wanafunzi, mabegi, madaftari, magodoro pamoja na paneli za sola ambazo zimeteketea moja kwa moja pamoja na dari ya chumba cha bweni ambapo jumla ya gharama zake zinafikia kiasi hicho cha fedha.
Hata hivyo Diwani wa Kata ya Mlowa, Charles Nyagawa (CCM) akizungumzia tukio hilo alisema kuwa amesikitishwa na kuungua kwa bweni hilo ambalo wazazi walishiriki kujenga na walitumia gharama kubwa.
Diwani huyo alisema, amesikitishwa na tabia za wanafunzi kuunguza bweni hilo kutokana na kujiingiza kwenye ufundi ambao hawaujui na wala hawana utaalamu nao.
Al i s ema k uwa , p i a anawashukuru wazazi na wananchi ambao walifika katika kijiji hicho na kuuzima moto na kuwa i n g awa h awa k uwe z a kufanikiwa anawashukuru kwa ushirikiano ambao w a l i u o n e s h a k a t i k a kuhakikisha moto huo unazimika na kuokoa baadhi ya mabweni mengine yasiendelee kuungua moto na kuteketea mali zingine zikiwemo za wanafunzi ambao walikwenda kwenye michezo na vitabu vya shule

 Na Goodluck Hongo
AGIZO l a Wa z i r i wa Uj e n z i Dk t . John Magufuli la kujengwa Barabara ya Jangwani-Kigogo jijini Dar es Salaam litaanza kutekelezwa kuanzia Agosti 6 mwaka huu licha ya kuwepo kwa kesi mahakamani.Kesi ambayo ilifunguliwa na wamiliki wa nyumba wapatao sita katika eneo hilo
. A k i z u n g u m z a n a mwandishi wa habari hizi jana jijini Dar es Salaam, Mkurungenzi wa Kampuni ya Heri Sigh tawi la Dar es Salaam ambayo ndiyo ilipata tenda ya ujenzi wa barabara hiyo, Jospal Sigh alisema ujenzi wa kipande hicho kilichobaki kitaanza kujengwa rasmi mwezi huo.
Awali Waziri wa Ujenzi Dkt.Magufuli alifanya ziara katika Mkoa wa Dar es Salaam kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Barabara ya Jangwani hadi Ubungo ambapo licha ya kukamilika sehemu kubwa ya barabara hiyo lakini hakukuwa na lami katika kipande cha kuanzia Jangwani hadi Njiapanda ya Daraja kuelekea Kigogo.
Baada ya kukagua barabara hiyo, Waziri Dkt. Magufuli ndipo alipotaka kujua sababu za kushindikana kukamilika kwa barabara hiyo na mkandarasi kukaa eneo la mradi kwa zaidi ya miaka miwili bila kazi.Akitoa maelezo mbele ya Waziri Magufuli mhandisi mshauri wa kampuni hiyo, Musa Ally alisema sababu za kushindwa kumalizika kwa kipande hicho ni kutokana na wananchi sita kufungua kesi mahakamani hivyo hadi kesi hiyo itakapokwisha ndipo wataendelea na ujenzi wa kipande hicho.
B a a d a y a k u p a t a maelezo hayo ndipo Waziri Ma g u f u l i a l i p o i a g i z a kampuni hiyo kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo kama ulivyopangwa lakini wasibomoe nyumba hizo hata kama lami itapita pembeni mwa nyumba hizo
"Fidia wamechukua lakini hapo hapo wamefungua tena kesi mahakamani na ujenzi ulitakiwa kukamilika siku nyingi zilizopita sasa Watanzania wajue kuwa wanaochelewesha maendeleo ni baadhi ya watu wachache kwani fedha zipo za utekelezaji wa miradi hiyo, nakuagiza mkandarasi ujenge barabara hii mara moja hata kama lami itapita pembeni mwa nyumba hizo wewe weka lami, lakini usibomoe nyumba hata moja na pia mtendaji mkuu wa TANROADS nakuagiza ukafungue kesi kwa watu hawa kwa kuitia hasara serikali kwani hilo linawezekana,"alisema Dkt. Magufuli.
Katika ziara hiyo Dkt. Magufuli alikagua barabara zote zinazojengwa Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi wa (DART).


 Na Mwandi shi We tu, Morogoro
WAKULIMA nchini wamependekeza k u w a p o k w a k i p e n g e l e k i n a c h o h u s u h a k i z a wakulima katika Rasimu ya Katiba. Ma p e n d e k e z o h a y o yalitolewa mjini Morogoro jana na mkulima kutoka mkoani Kilimanjaro, Freddy Nyakaka wakati akichangia mada katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA)
. Alisema, katika rasimu ya katiba iliyopo sura ya nne sehemu ya kwanza katika kipengele cha haki za binadamu, rasimu imetambua haki za makundi mbalimbali, lakini haijatambua haki za mkulima mdogo.Ma p e n d e k e z o h a y o yaliungwa mkono na wajumbe wote waliohudhuria mkutano huo. Akijibu hoja hiyo, mtoa mada, Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anord Sungusia, aliwashauri wakulima kuisoma rasimu ya katiba na kuielewa ili waweze kuijadili, ili kuwasilisha mapendekezo yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
"Ni vyema mtumie fursa hii ya kutoa maoni kwenye rasimu ya katiba, ili haki za wakulima zitambuliwe kikatiba," alisema. Aliwataka kutumia fursa hiyo ili kuondoa uonevu na dhuluma kwa wakulima ambayo imekuwapo kwa miaka mingi nchini.
Alisema wakulima ni waathirika wakubwa wa haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni pamoja na haki ya kumiliki mali.Alisema ingawa haki hazibagui, lakini kuna tofauti kubwa za huduma za jamii katika maeneo ya mijini na vijijini ambako asilimia 80 ya wananchi wanaishi huko.
Mwanasheria huyo alisema ingawa haki za binadamu zimeainishwa katika katiba iliyopo, lakini hakuna nia ya dhati ya kuzilinda haki hizo.Alishauri wakulima kwenda Mahakama Kuu wanapobaini haki zao z i n a v u n jwa , i n g awa mahakama hizo zipo katika mikoa 11 nchi nzima.  

. Na Theophan Ng'itu
MTU mmoja amefariki dunia papo hapo mara baada ya kugongwa na gari katika Barabara ya Nyerere eneo la Panasonic Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Engelbert 

Kiondo alisema kuwa mtu huyo mwanaume ambaye jina lake halikufahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45-50 aligongwa na gari lenye namba T 288 AZB aina ya Nisani Civilian Min-Bus.
Kiondo alisema kuwa, gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Abraham Said (39) mkazi wa Tandika mji mpya, ambapo alimgonga mtu huyo aliyekuwa akivuka barabara na maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke na dereva anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

 Na Mwandishi Wetu
KAMPUNIy a VodacomTanz ania imeendeleakuboresha m aishayaWatanzaniakwak uw awezes ha kujishindiakititac hash.milion i10kupitia promosheni ya ‘Cheka Plus.’M enejaUhusian owa UmmawaKamp uni hiyoB w.Matina Nkurlu,alisema kuwaKitit ahichokimenya kuliwan a was hindiw atano ambapo kila mmoja amejishindia kiasich ash.milioni2 kilammojakupit iaPr omosheni y a‘Che ka Plus’ iliyofanyika Julai 20m wa kahuu.

Aliwatajawashind ihaoni Musa Hussei nEllmyambayenimk aziwa Karatu- Arusha , Vumi J osh uaMt eru(Kiliman jaro), Joseph GodfreyKyando(Tunduma,Mbeya), AnatoriEmm anuel Chogol o (Dar es Salaam) , naAminaJosephMmbaga(Arusha).Alisema kuwa zaidi ya wateja 6,000wa mefaidikana ofahiyokabam beinayoende leahivi sasa nchinzi maa mbapozaidi y ash. milio ni100 zilikab idhiwak wawatejambalimbaliw ali oshindakupitia Promoshen iya‘Cheka Plus.’
Nkurlu alisema kuwa, tayari watejambal imbal inchiniwame wezakujishi ndiakiasik inacho fikiazaidi ya sh.milioni 10 0:“Tu mekuwatukipata washindi 100kilasikuam bapo wame kuwa wak ijis hind iash.10,000kilammojanawash indi wengin e10wakijin ya kuliash.50,000k ila siku, sambamba na droo kubwa ya mwezi ambapo katika washindi watano kila mmoja wao amekuwa akijinyakulia kitita cha shilingi milioni mbili."
Alisema Nkurlu promosheni hiyo bado inaendelea hivyo anawasihi wateja wa mtandao wa Vodacom kuendelea kufaidika na huduma zao ikiwemo promosheni ya “Cheka Plus” na kuweza kujishindia zawadi kemkem sambamba na kuendelea kuwasiliana na wapendwa wa

 MHAD HIRI w aCh uoKikuuchaKilimoc haSo koine (SUA), Dkt . DamianGabagambi,amesema ina hitajimi aka240kua nziasasailikuwe zakuto kom ezauma skini uliokithirikwawananchinchini,anaripoti Mw anadishi Wetu, Morogoro.
Ha yoyalibainishwamji ni hapajanana Dkt. Gabagam bi,wakati wamkut anom kuuwaMtandaowa Vik undivya Wak ulim a Tanza nia(MVIWATA).Alisema hali hiyo inachangiwa na kiwango kidogo cha kupunguza umaskini nchini tangu mwaka 1992 hadi mwaka 2011. “Tangu mwaka 1997 hadi mwaka 2011 umasikini umepungua kwa asilimia 2.1, hivyo kwa mtindo huu tukitaka kupunguza umaskini hadi asilimia 10, tutahitaji miaka 169 na kuutokomeza kabisa ni inahitaji miaka 240,” alisema.

Alisema ili nchi iondokane na hali hiyo, ni lazima kuwapo na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika sekta husika. A l i s e m a w a k u l i m a hawashirikishwi katika kuandaa mipango ya kupambana na , hivyo kusababisha changamoto zilizopo kwenye kilimo kuendelea kubaki zile zile pamoja na kuwapo kwa juhudi mbalimbali.

Dkt.Gabagambi, aliishauri Serikali kubadili mtindo wa ushirikishaji wa wadau ubadilishwe ili washirikishe wengi zaidi, kwani kushirikisha watu wachache ni ulaghai.Naye Profesa Amon Mattee, kutoka SUA aliwashauri wakulima na wafugaji kuzingatia sera katika masuala yote yanayohusu kilimo pamoja na kujitambua katika kukuza maslahi yao katika mchakato wa sera.

“Wakulima na wafugaji kutokuwa na ajenda na kutegemea viongozi wa serikali au kuwasema ni tatizo, kukosa sauti na msukumo wa pamoja katika mambo yanayowahusu ni tatizo, hivyo mnapaswa kuondokana na dhana hizi ili kulima kilimo chenye tija,” alisema.
Aliwataka wakulima watambue kuwa, wana haki na wajibu katika mchakato wa kuandaa sera pamoja na kuainisha mambo yanayowagusa, kwani wao ni kundi maalum ambalo lina tija kwa maslahi ya taifa.

Na Rashid Mkwinda, Mbeya
ASILIMIA 7.7 ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ndio waliosajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa kati ya asilimia 14 ya watoto wote nchini ikiwa ni asilimia 23 tu ya wananchi wote ambao wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) katika uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili wa vizazi kwa watoto waliochini ya miaka mitano, ni kwamba takwimu hizo zimekuwa haziridhishi kwa kutambua umuhimu wa usajili na utunzaji wa kumbukumbu muhimu za vizazi mwaka 2011.

Akizungumza katika uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili kwa watoto waliochini ya miaka mitano kwenye viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Vicent Mrisho alisema kudorora kwa mfumo wa usajili kumechangia serikali kukosa takwimu muhimu kwa mipango ya maendeleo ya Taifa.
Mrisho alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa takwimu zisizoridhisha za kumbukumbu za vizazi mwaka 2011 RITA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ilibuni mkakati wa usajili wa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano wenye lengo la kuboresha hali ya usajili nchini na kuweka kipaumbele kwa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano.
Alisema kuwa kundi hili la watoto chini ya miaka mitano lilichaguliwa kwa sababu ya kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa anapata cheti kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani na pia kundi ambalo hutumika kama kipimo katika mkataba wa Kimataifa kuhusu haki za Mtoto na Malengo la Milenia.
Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema mfumo mpya wa usajili ni sehemu ya ugatuaji wa madaraka kupeleka huduma katika ngazi ya serikali za mitaa.
Alisema awali usajili ulikuwa ukifanyika katika ofisi za Mkuu wa wilaya hali ambayo ilichangia kujitokeza kwa idadi ndogo na hivyo kuleta changamoto inayohitaji mipango mahsusi na kwamba mkakati huu utatoa suluhisho kwa mpango wa maendeleo ya Taifa.
Uzinduzi huu wa usajili wa vizazi na vifo utafanyika katika mikoa mitano ya Mbeya, Mwanza, Simiyu, Shinyanga na Geita ambapo kwa mkoa wa Mbeya kutakuwa na vituo 333 vya usajili katika ngazi ya ofisi za watendaji wa kata na vituo vya afya.

Na Rehema Mohamed
SHAHIDI wa 10 katika kesi ya wizi wa tani 26 za madini aina ya shaba inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani, (COREFA), Hassan Othman 'Hassanoo' na wenzake wawili, Rahim Jeta (38) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa shaba hiyo ya wizi ilihifadhiwa katika yadi ya mshtakiwa wa pili, Dkt. Najim Msenga baada ya Hassanoo kumuomba.

Shahidi huyo ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafirishaji wa Mizingi ya Libert Express iliyohusika kusafirisha shaba hiyo, alieleza hayo mahakamani hapo jana wakati akitoa ushahidi wake mbele ya hakimu Devotha Kisoka.Huku akiongozwa na Wakili wa Serikali Tumaini Kweka, Jeta alidai kuwa baada ya kupata taarifa za gari lao, T 821 DCL Scania lililobeba shaba hiyo kutofika bandarini walilifuatilia kupitia njia ya mtandao na kubaini lilipitia barabara ya Bagamoyo hadi eneo la Bahari Beach katika Yadi ya Najim.
Alisema walipofika katika yadi hiyo, wakiwa na polisi kutoka kituo cha Oysterbay kabla ya kufanya ukaguzi, ndipo mmoja wa mapolisi hao walipompigia simu Msenga, kumtaka afike hapo lakini hakufika kwa sababu alikuwa Tanga katika msiba.Shahidi huyo alisema kwa mujibu wa polisi hao, mshtakiwa wa tatu (Msenga) alikana kuhusika na shaba hiyo, ila anachokifahamu ni kwamba Hassanoo alimuomba ahifadhi mzigo huo katika yadi yake.
Alidai kuwa shaba hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Solowezi, Zambia kuja jijini Dar es Salaam na ilitakiwa kushushwa katika bandari kavu ya Tanzania Road Haulage (TRH).Naye shahidi wa tisa ambaye ni Ofisa Utumishi wa Kampuni ya Libert - Express, Solomon Makogo (47) alidai kuwa walipofika katika yadi ya Najim, walikuta shaba hiyo imefunikwa kwa turubai jekundu na kwamba aliipiga picha.
Mbali na Hassanoo, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara Wambura Kisiroti (32) na Dkt. Msenga (50).Inadaiwa kuwa Agosti 26, 2011 Bahari Beach washtakiwa hao waliiba tani 26 za madini ya shaba yenye thamani ya sh. milioni 400, mali ya Kampuni ya Liberty Express Tanzania Ltd yaliyokuwa yakisafirishwa kutoka Zambia kwa lori kuja Dar es Salaam. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 6, mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni