Jumanne, 25 Machi 2014

BREAKING NEWS: MKUU WA MKOA WA MARA MHE JOHN TUPA AFARIKI DUNIA WILAYANI TARIME MAPEMA LEO


  
Mkuu wa mkoa wa Mara Mhe. John Gabriel Tupa 
(pichani, enzi za uhai wake) amefariki dunia asubuhi ya leo akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Tarime.  

Habari zilizothibitishwa zinasema Marehemu Tupa alianguka na kupoteza fahamu akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. John Henjewele,  alikokuwa akipokea taarifa kabla ya kufunga mafunzo ya mgambo wilayani humo.

Mara baada ya kuanguka juhudi za haraka zilifanyika za kumkimbiza hospitali ya Wilaya ya Tarime ambako alitangazwa kuwa ameshafariki mara alipofikishwa hapo.

Mwili wa Marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Mara ili kuhifadhiwa wakati taratibu za m,aziko zikiandaliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni