Jumapili, 23 Machi 2014

VYUO mbalimbali nchini Vyashauriwa kujenga mahusiano ya kirafiki ili kubadilishana uzoefu katika kufanya kazi zao.

 Mtembeza wageni wa Kidishi Multi Spices Farm Bwana. Mur- tala Rashid akiwaonyesha mmoja wa mmea wa Spice na kuwafahamisha matumizi yake, mmea huo unaotambuliwa kwa jina la mchaichai katika chamba hilo.
 Wanafunzi wakifurahiya maelezo kutoka kwa Mtembeza wageni wa Kidishi Multi Spices Farm Bwana. Mur- tala Rashid (hayupo pichani). 
Baadhi ya wanafunzi wakionyeshana Spices walipokuwa wamepumzika katika shamba la Kidishi Multi Spices Farm lililopo Kidichi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. (Picha zote na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

========  =======  ========
Na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.

VYUO mbalimbali nchini, vimeshauriwa kujenga mahusiano ya kirafiki kati yao ili kubadilishana uzoefu katika kufanya kazi zao.
Ushauri huo umetolewa na mkuu wa msafara wa wanafunzi 70 kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii Dar es Salaam, Dawson Kyungai, wakati wakiwa katika ziara kuwatembelea viongozi wenzao wa Chuo cha Elimu Zanzibar (Zanzibar Education College).
Kyungai ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa ujasiri wao wa kutafuta njia za kujenga mahusiano na vyuo mbalimbali nchini. Naye Mkuu wa Zanzibar Education College Ussi Said Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari katika Kanisa la Mkunazini walikotembelea, alisema suala la urafiki wa vyuo linawasaidia walimu na wanafunzi kubadilishana mawazo na kujifunza kwa ufanisi zaidi.
Wanafunzi hao 70 wako katika ziara ya siku tatu kuwatembelea wenzao wa Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu pamoja na kuzuru sehemu mbalimbali za kihistoria za Zanzibar.
Kwa upande wao, wanafunzi na walimu wa Zanzibar Education College, wanatarajia kufanya ziara kama hiyo Mkoani Dodoma mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.
  Mtembeza wageni wa Kanisa la Mkunazini akiwafahamisha kitu wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii kutoka Dar es salam walipokuwa wakitembelea Kanisa hilo.
 Wanafunzi wakipata maelezo kwa Mtembeza wageni juu sehemu walipokuwa wakihifadhiwa watumwa Kanisani hapo.
 Wanafunzi wakitoka nje kwa furaha mara baada ya kutembelea Kanisa la Mkunazini liliopo Mjini Unguja. 
 Hapa wanafunzi wakijichagulia katika moja ya maduka ya vinyago na nguo za Kiswahili yaliopo Ngome kongwe Mjini Unguja. 
 Wanafunzi wakionyeshana Spices.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni